NAMNA ZA ZAKA (AINA NA MGAWANYIKO WA ZAKA) ZAKA IPO MAKUNDI MANGAPI?
Namna za Zaka
Zaka ni namna mbili:
Ya Kwanza, Zaka yenye kukhusu kiwiliwili, nayo ni Zakatu-l-fitri.
Ya Pili, Zaka yenye kukhusu mali, kama vile wanyamahoa, vitu vya thamani - dhahabu na fedha, Zaka ya mazao na matunda, na Zaka ya mali ya biashara.
Nyamahoa - nao ni ngamia, n'gombe kondoo/mbuzi; wote hawa ni waajibu kutolewa Zaka kama walivyokubaliana wanazuoni. Sababu ya kukhusishwa wanyama hawa kutolewa Zaka na si wengineo ni kwa vile kuweko kwao kwa wingi na kukua kwa kuzaliana kwa wingi, na kwa wingi wa manufaa walionayo khasa katika kuliwa; na asili ya hali ni vile kutowajibika kutolewa Zaka wasiokuwa wanyama hawa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai
Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa.
Soma Zaidi...Jinsi ya kujitwaharisha Najisi hafifu na najisi ndogo
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kujitwaharisha kutokana na najisi hafifu na najisi ndogo.
Soma Zaidi...Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawa mirathi
Haya ni mamno muhimu yanayozingatiwa kabla ya kuanza zoezi la kugawa mirathi ya marehemu.
Soma Zaidi...