image

Zijue sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji

Post hii inahusu zaidi sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji kina sehemu kuu nne na sehemu hizo ufanya kazi tofauti tofauti kama ifuatavyo.

Sehemu kuu nne za chumba cha upasuaji.

1.sehemu ya kwanza ni sehemu ambayo kila mtu anaweza kuingia kwa kitaalamu huitwa unrestricted zone, hiii sehemu hata ndugu wa mgonjwa wanaweza kukaa na kusubiria mgonjwa wao na nguo za nyumbani uweza kutumika katika sehemu hii  na watu hawakatazwi kuingia kwenye sehemu huu kwa ujumla huitwa sehemu ambayo haijafanyiwa usafi  unaopaswa  kitaalamu.

 

2.Sehemu ya pili ni sehemu ambapo  wahudumu wa afya wanaohusika na upasuaji ubadilisha mavazi yao na kuvaa mavazi rasmi ya kwa ajili ya kazi ya upasuaji kwa hiyo watu wengine hawapaswi kufika sehemu hii  sehemu hii huwa karibu sana na uelekea sehemu ya upasuaji kwa hiyo hii sehemu imetengwa na watu hawapaswi kuingia kwa sababu ya kuweza kuingiza wadudu kwenye chumba cha upasuaji na kusababisha madhara mengine ambayo hayakutarajiwa.

 

3.Sehemu inayofuata ni sehemu ya chumba cha upasuaji chenyewe, katika chumba hiki wahudumu wa afya  ndio wanapaswa kuingia na wakiwa wamevaa mavazi rasmi na pia mgonjwa mwenyewe anakuwa na mavazi  rasmi na vyombo vyote vya kwenye chumba hiki huwa kwenye hali ya usafi, hiki chumba kinatengewa kwa sababu ya kuzuia wadudu na uchafu mwingine kuingia kwa mgonjwa na kusababisha madhara yasiyotarajiwa kwa mgonjwa.

 

4.Chumba kingine na cha mwisho ni chumba cha kuhifadhia uchafu , sehemu hii huwa na ndoo tatu na box moja kwa ajili ya kuhifadhia uchafu mbalimbali ndoo ya kwanza huwa na uchafu wa karatasi za kawaida ambayo ina rangi ya kijani, ndoo ya pili ina rangi ya njano ambayo ina uchafu wenye maji maji na ndoo ya tatu ni nyekundu yenye uchafu uliochanganyika na damu na box linakuwa na takataka zenye ncha kali kama vile sindano.

 

5.Tunapaswa kujua sehemu hizo nne za chumba cha upasuaji ili kuepuka kuingilia chumba hiki endapo tuna wagonjwa na kujua kuwa wanafunzi wanaojifunza mambo ya afya wanapaswa kujua sehemu hizo ili kuepuka hali ya kuleta wadudu na vitu vingine kwa wagonjwa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 664


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

UPUNGUFU WA PROTINI NA FATI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

VIJUE VITAMINI, CHAZNO CHAKE, NA KAZI ZA VITAMINI MWILINI
Soma Zaidi...

Kauli za wataalamu wa afya
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu kauli mbalimbali za wataalamu wa afya Soma Zaidi...

MAANA YA AFYA, ni nani aliye na afya?
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

MAAJABU YA MBU
7. Soma Zaidi...

MZUNGURUKO WA DAMU
6. Soma Zaidi...

kitabu cha afya
Soma Zaidi...

kitabu cha afya
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

KITABU CHA MATUNDA
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

hathari zitokanazo na uvutaji wa sigara ,pombe na madawa ya kulevya na mbinu za kujikinga nayo
Posti hii inahusu zaidi utumiaji wa pombe na sigara pamoja na madawa katika jamii. Soma Zaidi...

MINYOO NA HATARI YEKE KWA AFYA: kuwashwa matako, kupungua uzito, kukosa hamu ya kula, kupungua damu
MINYOO NA HATARI YEKE KWA AFYA Utangulizi Karibu tena kwenye makala zetu za afya. Soma Zaidi...