Muhammad hakufundishwa quran na padri Bahira
(a)Dai la Kufundishwa na Padri Bahira:
Baadhi ya makafiri wanadai kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alijifunza Uyahudi na Ukristo katika safari zake mbili za biashara alizofanya Sham (Syria), hasa katika safari yake ya kwanza alipokutana na Padri Bahirah, alipokuwa na umri wa miaka 12. Tunavyojifunza katika historia ni kuwa Bahirah alikutana na Mtume (s.a.w) njiani na kuashiria kwa Ami yake Abutwalib, kuwa anamkisia kijana wake (Muhammad) ana sifa za yule mtume aliyetabiriwa katika Injili (Rejea Qur-an 61:6).
Je, inamkinika kuwa mazungumzo haya ya njiani ya muda mfupi yawe ndiyo yaliyompelekea Mtume (s.a.w) kuandika Qur-an miaka 28 baada ya makutano hayo? Ikumbukwe kuwa Mtume (s.a.w) alianza kushushiwa wahy wa Quran alipokuwa na umri wa miaka arobaini ambapo alikutana na Bahirah akiwa na umri wa miaka kumi na mbili.
Safari ya pili ya Mtume (s.a.w) kwenda Syria kwa biashara ni pale alipokodiwa na Bibi Khadijah alipokuwa na umri miaka ishirini na tano. Katika kumbukumbu za historia, Mtume (s.a.w) hakufanya mkutano wowote na Wakristo wala Mayahudi kabla ya Utume.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 ai web app 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 web hosting 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Suratul-takaathur (102) imeteremshwa makkah Ina aya nane
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Maana ya Idgham na aina zake katika usomaji wa Quran tajwid
Aina za idgham ni idgham al mutamathilain, na idgham al mutajanisain
Soma Zaidi...Amri ya Kuchinja Ng'ombe
Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.
Soma Zaidi...ASBAB-NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN
ASBAB NUZUL SABABU ZA KUSHUKA AYA NA SURA KWENYE QURAN Quran imeteremka kwa muda wa miaka 23 kidogokido.
Soma Zaidi...