Aasbab Nuzul surat Ash sharh: sababu za kushuka alam nashrah (surat Ash sharh)

Makala hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa alam nasharah yaani Surat Ash sharh.

Surat Ash sharh, imeteremka Makkah na ina aya 8. Sura hii ni miongoni mwa sura za mwanzo kushuka. Sura hii ni ya 94 katika mpangilio wa Quran jinsi ilivyoandikwa kwenye mashaf. Sura hii ni sura iliyotangulia yaani surat dhuhaa zinafanana maudhui zao, na zinakadiriwa kushuka katika nyakati sawa. Wakati mwingine sura hizi huchanganywa kwenye kusoma.

 

Sura hii inasimulia kisa cha kupasuliwa kifua mtume. Tukio hili inasemekeana limetokea mara mbili. Moja alipokuwa mtoto na mara nyingine ni pale alipokuwa katika safari ya Israa na Miraj. Sura hii na iliyofuata zinataja baadhi ya neema ambazo Allah amempa Mtume s.a.w.

 

Sababu za kushuka sura hii:

Katika historia hakuna sababu maalumu za kushuka sura hii kama ambavyo tumeona sura zilizopita. Lakini ipo hivi. Sura hii na iliyotangulia zilishuka katika wakati ambao ndio Mtume s.a.w amepewa Utume. bado ni mgeni wa kazi ya utume. Wakati ambao vikwazo, fitina kutoka kwa makafiri vilikuwa vimeanza kupamba moto. Sura hizi zilishuka kwa lengo la kumfariji Mtume s.a.w. Na ndio maana sura hizi zinataja baadhi ya neema ambazo Allah amempa Mtume Muhammad, ambazo miongoni mwazo hakuna Mtume mwingine aliyepewa. Kwa mfano kupasuliwa kifu na kuondolewa uzito ambao ambao ungemfanya kazi ya utume iwe ngumu. Pia neema nyingine ni kutukuzwa utajo wake. Yaani huwezi shahadia kwa kusema laa ilaaha Illa Llha, mpaka umalizie Muhammad rasulullah. 

 

Kisha sura ikaendelea kumfariji kuwa hakika kila utakapopata uzito basi kuna wepesi pia ndani yake. Yaani baada ya taabu utakayoipata basi ujuwe kuna neema zinafuata mbele. Aya ikaendelea kuwa utakapopa faragha fanya juhudi ya kutafuta radhi za Allah kwa ibada na adhkar na mambo mengine.

 

Ufupi wa maneno ni kuwa sura hii imeshuka kwa lengo la kumfariji Mtume s.a.w kutokana na yale aliyoyakuta katika kazi ya utume, na ktokana na yatakayokuja kutokea kama matokeo ya kazi ya Utume. Allah ndiye anajuwa zaidi



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/05/09/Monday - 09:37:24 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1557


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-