Adabu za kuomba dua kuifanya dua yako ikubaliwe kwa haraka

Post hii inakwenda kukugundisha adabu zinazotakikana kwa mwenye kuomba dua.


ADABU ZA KUOMBA DUA.
1.kuelekea qibla. Amesimulia Abdallah Ibn Zayd رضىالله عنه kuwa “alitoka Mtume صلّي الله عليه وسلّم kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla”. (amepokea Bukhari).

2.Kunyanyua mikono miwili juu. Amesimulia Abuu Musa رضىالله عنه kuwa “aliomba Mtume صلّي الله عليه وسلّم dua akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa lake” (amepokea Bukhari). Na amesimulia Ibn ‘Abas kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema ‏ "‏ إِذَا دَعَوْتَ اللَّهَ فَادْعُ بِبُطُونِ كَفَّيْكَ وَلاَ تَدْعُ بِظُهُورِهِمَا فَإِذَا فَرَغْتَ فَامْسَحْ بِهِمَا وَجْهَكَ “muombeni Allah kwa matumbo ya viganya vyenu, wala msimuombe kwa migongo ya viganja vyenu.…”. (amepokea Abuu Daud na Bayhaqiy).

3.Kuanza dua kwa kwa kumsifu Allah na kumshukuru (kama kusema alhamdu lillah ….) na kumswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم. Amesimulia ‘Abdullah Ibn Mas’ud رضىالله عنه kuwa nilikuwa nikiswali, wakati Mtume yupo na Abuubakar na ‘Umar, basi nilipokaa nikaanza kumshukuru Allah na kumsifu na nikamswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha nikajiombea dua, akasema mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘omba utapewa, omba utapewa’”. (amepokea tirmidh kwa isnad sahih). Na katika masimulizi ya Fudailah Ibn ‘Ubayd رضىالله عنه amesema “hakika amefundisha mtume صلّي الله عليه وسلّم uma wake jinsi ya kuomba dua akasema ‘pindi anapoomba dua mmoja wenu basi aanze na tahmid (kumshukuru Allah) na thanaai (kumsifu Allah) kisha amswalie Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha aombe chochote anachotaka’” ‏"‏ إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ اللَّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ لِيُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لِيَدْعُ بَعْدُ بِمَا شَاءَ ‏"‏ (amepokea Abuu Daud, tirmidh, Ibn Hiban na baihaqy).

4.Kuanza kuomba dua kwa kujiombea mwenyewe. Kwa anayetaka kumuombea mtu mwingine dua anatakiwa aanze na kujiombea mwenyewe. Amesimulia Ubaiya Ibn K’ab رضىالله عنه kuwa عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ “alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم anapomkumbuka mtu na akataka kumuombea dua huanza kwa kujiombea mwenyewe kwanza.” (amepokea tirmidh kwa isnad sahih).

5.Kurudia rudia katika kuomba na kusisitiza maombi yako. Ila usiharakishe majibu kutaka kujibiwa haraka hata ukawa unamlaumu Allah. Amesimulia Abdallah ibn Ms’ud رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapenda kuomba mara tatutatu na (akawa) anaomba istighfar (msamaha) mara tatutatu. (amepokea Abu Daud kwa isnad salih).

6.Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa na kujiepusha na yaliyo haramu. Mtu anatakiwa asiwe na shaka juu ya kujibiwa dua yake. Amesimulia Abuu Hurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ ادْعُوا اللَّهَ وَأَنْتُمْ مُوقِنُونَ بِالإِجَابَةِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ لاَ يَسْتَجِيبُ دُعَاءً مِنْ قَلْبٍ غَافِلٍ لاَهٍ ‏"‏ “muombeni Allah mkiwa na yakini juu ya kujibiwa na jueni kuwa Allah hakubali dua ya mtu ambaye moyo wake umeghafilika naye. (amepokea Tirmidh na Alhaakim).

7.Usiharakishe kujibiwa. Isitokee mtu akawa na haraka ya kutaka maombi yake yajibiwe kama anavyotaka yeye kwa haraka hata akawa analaumu. Amesemulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي ‏" “atajibiwa (dua yake ) mmoja wenu maadam hajaharakisha (kujibiwa) akawa anasema nimeomba na wala sijajibiwa”. (amepokea Bukhari na Muslim). Na katika masimulizi mengine ya Abuuhrairah kuwa mtume amesema “hataacha mja kujibiwa dua yake maadam hajaomba madhamdhi au kukata udugu”. (amepokea Muslim na Abuu Daud). Hii ina maana dua itajibiwa tu ila isiwe ya kuomba madhambi au kukata udugu.

8.Kuitikia “aamiin”. Mwenye kuomba dua basi aitikie “aamiin” eidha awe mwenyewe pekee au yupo na kundi la watu. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم “atakapoomba dua mmoja wenu basi na aitikie ‘aamiin’ mwenyewe’”. (amepokea Ibn ‘Adiy).


 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sunnah Main: Dini File: Download PDF Views 2626

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

hadithi ya 8

عَنْ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم قَالَ: "أُمِرْتُ أَنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى ?...

Soma Zaidi...
BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU

BAADHI YA DUA ZA KILA SIKU.

Soma Zaidi...
Hadithi inayotaja nguzo tano za uislamu

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ بْنِ الْخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صل?...

Soma Zaidi...
Matamshi ambayo ukimwambia Allah kwenye dua yako basi hujibiwa kwa haraka dua hiyo

Post hii inakwenda kukufundisha matamshi ambayo mtu akiyatamka Allah hujibu dua hiyo kwa urahisi.

Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu na wenye elimu katika Uislamu

Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika uislamu inaonkana katika maeneo yafuatayo: Kwanza, Elimu ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.

Soma Zaidi...
Hukumu ya kukusanyika kwenye dua na umuhimu wa dua ya watu wengi

Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kukusanyika katika kuomba dua.

Soma Zaidi...
Hadithi ya tatu:ukarimu na kusaidiana

Sunnah na hadithi (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...