Adhkari unazoweza kuomba kila siku
Hapa nitakuletea baadhi tu ya adhkari ambazo ni muhimu kwa muislamu
ADHKARI MBALIMBALI NA DUA
Hapa tutajifunza dua mbalimbali ambazo ni adhkari. Tutajifunza pia na faida zake kama Mtume صلّي الله عليه وسلّم alivyozungumza na masahaba zake. 1.amesema Mtume" أَفْضَلُ الذِّكْرِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَفْضَلُ الدُّعَاءِ الْحَمْدُ لِلَّهِ " “bora ya dhikir ni kusema Lā ilāha illallāh na bora ya dua ni kusema Al-ḥamdulillāh” (amepokea Tirmidh).
2.Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " مَا مِنْ عَبْدٍ يَقُولُ فِي صَبَاحِ كُلِّ يَوْمٍ وَمَسَاءِ كُلِّ لَيْلَةٍ بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لاَ يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ فِي الأَرْضِ وَلاَ فِي السَّمَاءِ وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ فَيَضُرُّهُ شَيْءٌ " “Mja yeyote atakayesema ‘Bismillāh, alladhi lā yaḍurru ma`a ismihi shai'un fil-arḍi wa lā fis-samā', wa huwas-Samī`ul `Alīm’ mara tatu kila asubuhi na jioni hatadhuriwa na kitu chochote” (Amepokea Tirmidh).
3.mtume amesema " مَنْ قَالَ حِينَ يُمْسِي رَضِيتُ بِاللَّهِ رَبًّا وَبِالإِسْلاَمِ دِينًا وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا كَانَ حَقًّا عَلَى اللَّهِ أَنْ يُرْضِيَهُ " “Mwenye kusema jioni ‘Raḍītu billāhi rabban wabil-Islāmi dīnan wa bi-Muḥammadin nabiyyan’ itakuwa ni haki kwa Allah kumridhia” (Amepokea tirmidh).
4.Mtume alimwambia al-baraa IBN ‘Aazib kuwa “أَلاَ أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ تَقُولُهَا إِذَا أَوَيْتَ إِلَى فِرَاشِكَ فَإِنْ مُتَّ مِنْ لَيْلَتِكَ مُتَّ عَلَى الْفِطْرَةِ وَإِنْ أَصْبَحْتَ أَصْبَحْتَ وَقَدْ أَصَبْتَ خَيْرًا تَقُولُ اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْلَمْتُ نَفْسِي إِلَيْكَ وَوَجَّهْتُ وَجْهِي إِلَيْكَ وَفَوَّضْتُ أَمْرِي إِلَيْكَ رَغْبَةً وَرَهْبَةً إِلَيْكَ وَأَلْجَأْتُ ظَهْرِي إِلَيْكَ لاَ مَلْجَأَ وَلاَ مَنْجَا مِنْكَ إِلاَّ إِلَيْكَ آمَنْتُ بِكِتَابِكَ الَّذِي أَنْزَلْتَ وَبِنَبِيِّكَ الَّذِي أَرْسَلْتَ "
“je nikufundishe maneno utakayoyasema pindi atakapoliendea tandiko lako (kulala) na kama utakufa utakufa katika fitrah (uislamu) na ukiamka asubhi utakuwa umepambaukiwa katika kheri? Utasema ‘'Allāhumma innī aslamtu nafsī ilaika wa wajjahtu wajhī ilaika, wa fawwaḍtu amrī ilaika, raghbatan wa rahbatan ilaika wa alja'tu ẓahrī ilaika, lā malja'a [wa lā manjā] minka illā ilaik. Āmantu bikitābikal-ladhī anzalta wa binabiyyikal-ladhī arsalt’ (Amepokea Tirmidh).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Hadithi Muhimu Kuhusu Ndoa Katika Uislamu
Ndoa katika Uislamu ni mkataba mtakatifu (mithaqan ghaliza) unaounganisha watu wawili kwa lengo la kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, utulivu wa nafsi, na kuendeleza kizazi. Makala hii inachambua Hadithi muhimu za Mtume Muhammad (S.A.W) zinazotoa mwongozo kuhusu vigezo vya kuchagua mwenzi, haki za wanandoa, na umuhimu wa kuhifadhi mahusiano haya kwa upendo na busara.
Soma Zaidi...Jinsi ya kuzuru makaburi na dua unazotakiwa kuzisoma ukiwa makaburini.
Posti hii inakwenda kukufundisha maneno unayotakiwa kuyasema unapozuru makaburi.
Soma Zaidi...