picha

FANGASI SEHEMU ZA SIRI: DALILI ZAKE, CHANZO CHAKE NA NJIA ZA KUPAMBANA NAO

FANGASI SEHEMU ZA SIRI: DALILI ZAKE, CANZO CHAKE NA NJIA ZA KUPAMBANA NAO

FANGASI

Fangasi huweza kuishi na kuathiri maeneo mbalimbali ndani ya mwili. Fangasi ni hatari sana, kwani wanaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya na kiakili kama wasipitibiwa mapema. Kuna aina nyingi za fangasi ambao wanaweza kuathiri mwili wa binadamu.

 

Kuna mamilioni ya aina hizi za fangasi, katika hawa kuna kuna mamia ya aina za fangasi ambazo huweza kumfanya mtu kuumwa. Fangasi wanaweza kuathiri makwapa, vidole, sehemu za siri kwenye tumbo na maeneo mengine.

 

Fangasi wa sehemu za siri husababishwa na fangasi waitwao candida. Hawa wanaweza kuathiri sehemu za siri kuzungukia uume ama uke. Kunatafiti zinaonesha kuwa fangasi hawa wanaweza kuambukizwa kwa kufanya mapenzi. Japo tafiti zaidi zinahitajika ili kuthibitisha hili.

 

FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI DALILI ZAO KWA WANAUME

  1. Kuvimba kwa kichwa cha uume
  2. Kuwasha kwa sehemu za siri, hususan kichwa cha uume
  3. Uume kuwa mwekundu kwa kuchubuka ama kuvumba ama kwa mashambulizi ya fangasi hawa.
  4. Kuota kwa mapele na maruturutu kwenye uume
  5. Kuwasha uume ama kuungua moto kwa uume.
  6. Kutokwa na majimaji meupe kwenye uume, majimaji haya huwa na harufu mbaya.
  7. Maumivu wakati wa kukojoa na kufanya tendo la ndoa.

DALILI ZA FANGASI WA SEHEMU ZA SIRI KWA WANAWAKE

  1. Maumivu na miwasho kwenye mashavu ya uke na sehemu ya juu ya uke
  2. Maumivu wakati wa kukojoa ama kufanya tendo la ndoa
  3. Uuke kuwaka moto kwa ndani
  4. Kuvimba kwa mashavu ya uke na kuwa mekundu
  5. Kuot mapele na maruturutu kwenye uke
  6. Kutokwa na majimaji kwenye uke
  7. Kutokwa na majimaji mazito meupe na yenye harufu mbaya kwenye uke.

 

WATU WALIO HATARINI KUPATA FANGASI HAWA

  1. Wachafu
  2. Kuwa na mikunjomikunjo kwenye ngozi kama kitambi
  3. Wenye kisukari
  4. Wenye HIV
  5. Wenye saratani
  6. Wenye kutumia baadhi ya madawa ya kuzuia mimba
  7. Wajawazito

 

NJIA ZA KUPAMBANA NA FANGASI HAWA

  1. Kuwacha kutumia madawa ya kusafishia ama kuunga uke
  2. Kutokuvaa nguo mbichi
  3. Kutokuvaa nguo za kubana hususani za mpira
  4. Kuwa msafi muda wowote
  5. Kuosha kichwa cha uume na ngozi ya govi mara kwa mara
  6. Kuosha uke mara kwa mara
  7. Kutumia pedi zilizo kavua na safi na kubadilisha mara kwa mara
 


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 6000

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Bongolite - Game zone - Play free game    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 web hosting   

Post zinazofanana:

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu.

Soma Zaidi...
Dalili za Ugonjwa wa mapigo ya moyo

Mapigo ya moyo ni hisia za kuwa na moyo wa haraka, Kupepesuka au kudunda. Mapigo ya moyo yanaweza kuchochewa na mafadhaiko, mazoezi, dawa au, mara chache, hali ya kiafya. Ingawa mapigo ya moyo yanaweza kuwa ya kutisha, kwa kawaida hayana madhara. Katik

Soma Zaidi...
Kifuwa kinaniuma katikati kinaambatana nakichwa

Maumivu ya kifuwa yanaweza kutokea baada ya kubeba kitu kizito, ama kupata mashambulizi ya vijidudu vya maradhi. maumivu ya viungo na hata vidonda vya tumbo. Lakini sasa umesha wahi fikiria maumivu ya kifuwa kwa katikati?

Soma Zaidi...
Dawa za kutuliza vvu zinaongeza damu

Hakuna dawa ya UKIMWI ya kutibu kuondoa virusi mwilini, lakini zipo dawa za kuweza kupunguza makali ya virusi hawa. Hivi unesha jiuliza kuwa je zile dawa zinaongeza damu?

Soma Zaidi...
Tatizo la Kikohozi Cha muda mrefu

Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kikohozi cha muda mrefu ni zaidi ya kero. Kikohozi cha muda mrefu kinaweza kuharibu usingizi wako na kukuacha unahisi uchovu. Matukio makali ya kikohozi cha muda mrefu yanaweza kusababisha kutapika, kizunguz

Soma Zaidi...
Sababu za Maambukizi kwenye mifupa.

Post hii inahusu zaidi Maambukizi kwenye mifupa ambayo kwa kitaalamu huitwa Osteomyelitis, ni Maambukizi ambayo hutokea kwenye mifupa kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha ugonjwa huu.

Soma Zaidi...
Namna magonjwa ya koo yanavyosambaa

Posti hii inahusu zaidi namna ya magonjwa ya koo yanavyosambaa, magonjwa haya usambaa kutoka sehemu Moja kwenda nyingine kwa njia tofauti kama ifuayavyo

Soma Zaidi...
Habari nasumbuliwa na tumbo upande wakilia adi nikikojoa mkojo wa mwisho uwa wa kahawia tiba take nini?

Maumivu ya tumbo yanaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo typhod, vidonda vya tumbo na shida nyingine kwenye mfumo wa chakula.

Soma Zaidi...
Dalili za Dengue.

Posti hii inahusu zaidi dalili za Dengue,ni Dalili ambazo huwa kwenye makundi matatu na kuwepo kwa makundi hayautegemea kuongezeka kwa tatizo kwa sababu tatizo likiongezeka bila kutibiwa na dalili uongezeka na kufikia kwenye sehemu isiyo ya kawaida kwa mg

Soma Zaidi...
Dalili za saratani (cancer)

Posti hii inahusu zaidi dalili za kansa, ni dalili ambazo utokea kwa mtu Mwenye tatizo la ugonjwa wa Kansa ingawa sio lazima dalili hizi kutokea tukadhani kuwa ni Kansa Ila zilizonyingi huwa ni kweli dalili za kansa.

Soma Zaidi...