SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA (sababu za kuharibika kwa ujauzito)
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka.
SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Yaani karibia robo ya mimba zinazopatikana hutoka. Kitendo hiki cha kutoka kitaalamu huitwa misscarriage. Hiki ni kitendo cha kupotea kwa ujauzito kabla ya wiki ya 20.
Sababu za kutoka kwa mimba:
- Sababu za kurithi (genetics): hutokea mwanamke akarithi hizi sabau kutoka kwenye familia yake. Sababu hizi huenda zikapelekea matatizo ambayo baadaye huchangia mimba kutoka. Matatizo haya ni kama
- Mtoto kutokuendelea kukuwa tumboni
- Kiini tete (embriyo) kutokutengenezwa
- Placenta kuwa kubwa zaidi tofauti na kawaida.
- Afya ya mama; hutokea mwanamke mjamzito afya yake ikawa ni sababu ya ujauzito wake kutoka. Mwanamke akiwa na maradhi yafuatayo ujauzito wake unaweza kuwa hatarini:
- Kisukari
- Maradhi ya moyo
- Presha ya kupanda (hypertension)
- Maradhi ya figo
- Maambukizi; mwanamke mjamzito anweza kuweka ujauzito wake hatarini kama atakuwa na maambukizi ama mashambulizi ya maradhi kama:
- Chlamydia
- Gonoria
- Syphilis
- Malaria
- Ukimwi
- Udhaifu wa cervix; cervics ni mlango wa nyumba ya mimba.
- PCOS (Polycystic Ovary Syndrome). hii hupelekea ovary kuwa kubwa tofauti na kawaida. Ovary ndio sehemu ambayo mayai ya mwanamke hutengenezwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 web hosting 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 ai web app 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Yajue mazoezi ya kegel
Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti.
Soma Zaidi...Ni zipi njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukuletea njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume
Soma Zaidi...Faida za uzazi wa mpango kwa watu wenye ugonjwa wa Ukimwi
Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi, ni faida wanazozipata waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi.
Soma Zaidi...Vyakula vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa
Posti hii inahusu zaidi vyakula mbalimbali vya kuongeza tendo la ndoa, kwa kawaida kuna vyakula mbalimbali ambavyo watu ukitumia ili kuweza kuongeza tendo la ndoa vyakula hivyo ni kama tutakavyoona hapo baadaye
Soma Zaidi...Kifafa Cha mimba husababishwa na nini
Katika makala hii utakwenda kujufunza kuhusu sababu za kifafa Cha mimba.
Soma Zaidi...