NAMNA YA KUITAMBUA SIKU HATARI YA KUPATA MIMBA (UJAUZITO)
SIKU YA KUPATA UJAUZITO Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote.
SIKU YA KUPATA UJAUZITO
SIKU YA KUPATA UJAUZITO
Mimba hutokea pindi mbegu ya kiume (sperm) inapokutana na yai la mwanamke (ova) na kuungana kwa pamoja kutengeneza selli moja iitwayo zygote. Seli hii hukuwa na kujakuwa mtoto kamili. Kawaida kitendo hiki hufanyika ndani ya masaa 12 toka yai kukomaa na kuletwa kwenye mirija ya falopian. Baada ya mimba kutungwa itabakia pale kwa masaa kama matatu, kisha huanza kusafirishwa na kupelekwa kwenye tumbo la mimba ambapo huku litabakia mpaka mtoto kuzaliwa.
Mwanamke hutoa yai moja kila mwezi kutoka katika ovari moja. Kuna wakati mwanamke huenda akatowa mayai zaidi ya moja, hali hii si kawaida. Yai hili linaweza kuwa hai ndani ya masaa 12 mpaka 24. hutokea pia likaweza kuwa hai mpaka masaa 48. ndani ya muda huu yai ni lazima likutane na mbegu ya kiume ili mimba itungwe. Kipindi hiki kitaalamu kinajulikana kama fertile window.
Mbegu ya mwanaume huweza kudumu kuwa hai ndani ya siku 5, ndani ya siku hizi mbegu hizi huwa zipo hai hivyo zinaweza kurutubisha yai. Mwanaume huto zaidi ya mbegu milioni 300 ejaculation moja. Katika mbegi hizi mbegu moja ndio hutakiwa kuungana na yai.
Siku za mwanamke kuweza kuwa kati ya 21 mpaka 35 inategeme na mwanamke. Kikawaida walio wengi siku zao ni 28. katika siku hizi zipo siku 6 tu ambazo mwanamke anaweza kupata ujauzito. Siku hizi huanzia siku ya 11,12,13,14,15 na 16. katika siku hizi siku ya 14 ndio ambayo huaminika zaidi kuwa yai hutolewa ziku hii. Ni vyema kukutana kimwili katika siku hizi kwa wanaotafuta ujauzito. Sio lazima pia kufululiza inawezekana kuruka ila nivyema kutoikosa siku ya 13 na 14.
Pia kuna dalili kadha za kuijua siku hii kama kuzidi kwa joto la mwanamke siku moja kabla na siku ile ya kutolewa kwa yai. Pia kuongezeka kwa utelezi kwenye shingo ya uzazi. Pia mwanamke anapenda sana kukutana kimwili kukaribia siku hii. Vipo vifaa pia vya kuitambua siku hii. Siku hizi huhesabiwa kutoka kupata hedhi na kuendelea. Pia siku hisi kutofautiana kwa wanawake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Kitau cha Fiqh π2 Bongolite - Game zone - Play free game π3 Kitabu cha Afya π4 Simulizi za Hadithi Audio π5 kitabu cha Simulizi π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Dalili za PID
Posti hii inahusu zaidi dalili za PID maana yake ni maambukizi kwenye pelvic kwa kitaalamu huitwa pelvic infection disease, ni ugonjwa unaoshambulia sana wanawake na wasichana
Soma Zaidi...Je ?kipimo kikionyesha misitar miwili mmoja hafifu mwingine umekolea ni mimba au sio
Kipimo chamimba cha mkojo, huonyesha nestory miwili kuwa una mimba, na mmoja kuwa huna mimba. Sasa je ukitokea mmoja umekoleana mwingine hafifu? Endelea na pasti Γ’ΕΒΓ―ΒΈΒ hadi mwisho
Soma Zaidi...Mwenye ujauzito wa wiki moja na ana u.t.i anaweza kutumia dawa za aina gani ambozo zitakua salama kwa kiumbe kilichoanza kukua?
Ujauzito unaweza kutoka kwa sababu nyingi kama maradhi, madawa, vyakula na ajali. Unawezakutoa mimba bila kujuwa amakwakujuwa. Damu kutoka ni moja ya dalili za kutoka kwa mimba hata hivyo maumivu ya tumbo huweza kuandamana na damu hii.
Soma Zaidi...Sababu za kuongezeka uzito wa wajawazito.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua.
Soma Zaidi...Ukifanya mapenzi siku hatari na ukameza P2 unaweza pata mimba?
Je umeshawahi kujiukiza kuwa, dawa ya P2 ni kweli inaweza kuzuia mimba, ukifanya mapenzi siku hatari?
Soma Zaidi...