MAJIMAJI YA UKENI, PIA MIWASHO YA UKENI, FANGASI WA UKENI, UCHAFU UNAOTOKA UKENI, SARATANI AU KANSA YA KIZAZI
MAJIMAJI YA UKENI YANATUELEZA NINI
SIFA ZA CERVICAL MUCUS
Majimaji haya pia huwenda kuambatana na dalili za mashambulizi ya bakteria na fangani endapo yatakuwa na harufu mbaya na rangi ya kijani.
Majimaji haya yasichananywe na uchafu utokao kwenye uke kwa sababu ya bakteria, fangasi ama saratani ya kizazi.
Baada ya hedhi uke huwa mkavu hivyo majimaji haya yanakuwa ni macgache na si yenye mtelezo wowote. Hayana rangi yeyote na wala huwezi kuyapata kwa wingi. Hii huashiria kuwa muda huu mwanamke hawezi kupata ujauzito.
Siku chache baadaye majimaji yataanza kuonekana yakiwa na muonekano wa kuweza kunatanata, majimaji haya sio mepesi kabisa. Huu ni mwanzo wa kuandaliwa mazingira ya kupevushwa kwa yai.
Baada ya siku chache tu yai linakaribia kutolewa, muda huu majimaji haya yanakuwa mepesi, laini, mengi na yenye rangi nyeupe. Haya maji ni kiashiria kuwa sasa yai lipo njiani kutolewa. Huu ni muda muafaka zaidi kwa wanaotafuta mtoto.
Siku moja ama mbili kabla ya yao kutolewa majimaji haya yanafanana sana na majimaji ya weupe wa yai, yaani kama yale majmaji meupe yanayooekana pindi linapopasuliwa yai. Majimaji haya yanaweza kuvutika kwenye vidole na yanateleza sana. Hii ni ishara kuwa yai limekaribia kutolewa eidha kwa siku moja ama mbili.
Punde baada ya yai kutolewa majimaji haya yanaanza kuwa makavu na kupoteza mtelezo. Ama uke unakauka na kuwa mkavu na kurudi katika hali ya kawaida. Na kama mimba ilitungwa majimaji haya yanakuwa na rangi ya maziwa. Hivyo ni vyema kuchunguza vizuri ili kujuwa kama mimba ilitungwa au laa.
Pia ijulikane kuwa kuna wanawake wengine hawana majimaji haya na pia kuna wengine ambao majimaji haya ni mengi sana zaidi ya kawaida. Hivyo katika kuchunguza hali hizi wanawake wa aina hii ni ngumu sana kwao.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 ai web app 👉3 web hosting 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Je kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo?
Nimesoma makala yenu, sasa nina swaliJe kitunguu saumu kina madhara kwa Mgonjwa wa figo?
Soma Zaidi...Yajue madhara ya kutoa mimba mara Kwa mara
Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wale wenye tabia ya kutoa mimba mara Kwa mara .
Soma Zaidi...Habari, naomba kuulizia, nimadhara gani atayapata mwanamke akitolewa bikra bila kukusudia
Je unawaza nini endapo bikra itatolewa bila wewe kukusudia, je imetolewa kwa njia ya kawaida yaani uume ama ilikuwa ni ajali?
Soma Zaidi...Vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya mwanamke kushindwa kupata ujauzito, kwa sababu kuna sababu nyingi ambazo Usababisha mwanamke kushindwa kupata ujauzito kama tutakavyoona hapo mbeleni
Soma Zaidi...Namna ya kumpima mtoto uzito
Posti hii inahusu namna ya kumpima mtoto uzito, ni njia ambayo utumika kujua uzito wake na maendeleo ya mtoto.
Soma Zaidi...Faida na hasara za Kufunga kizazi kwa wanawake.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Kufunga kizazi kwa wanawake.
Soma Zaidi...