MAJIMAJI YA UKENI (CERVICAL MUCUS)
Kuna mabadiliko yanayotokea kwenye mwili wa mwanamke katika mzunguruko wa siku zake. Cervical mucus ni majimaji yenye sifa tofauti tofauti yanayopatikana kwenye njia ya uzazi yaani uke. Majimaji haya yanabadilika kulingana na siku ama maradhi. Miongoni mwa sifa hizi ni kama kinata, kuteleza, kufutika, ukavu na rangi yake.
Majimaji haya yanasaidia katika kutujulisha siku ambazo ni mujarabu kwa wale ambao wanatafuta ujauzito. Pia majimaji haya ni taarifa kuwa yai lipo karibu ktolewa hivyo ni vyema kujiandaa. Majimaji haya pia yanaweza kutujulisha kama mimba imeingia ama laa. Tofauti na kazi hizi majimaji haya yana kazi zifuatazo:-
1.Kuzuia bakteria na wadudu wengine wasiingie ndani kwenye tumbo la uzazi
2.Kusafirisha mbegu za kiume (sperm) kuelekea ndani
3.Kulainisha njia ya uke na kuwa katika hali iliyo bora zaidi.
Majimaji haya huweza kutofautiana muonekano kutokana na mabadiliko ya siku. Siku hizi huanza kuhesabiwa punde tu baada ya kumalizika kwa hedhi. Ili kuchunguza majimaji haya inahitaji muda na ni vyema kutokukutana kimwili kama unataka kuchunguza mabadiliko haya katika mwezi wote hii husaidia kwani kukutana kimwili kunaweza kuathiri muonekano wa majimaji haya.
Kama unataka kuchunguza kwa baadhi ya siku tu kama kutaka kujua kama yai linakaribia basi unaweza kukaa mkao wowote ambao utafanya uke uwe wazi, kisha tumia kitambaa laini cheupe na kiingize ndani na fanya kama unapangisa kitu kwa ndani ili kuweza kuyapata majimaji haya kwa wingi. Ia unaweza kutumia kidole, baada ya hapo chunguza vyema rangi na muinekano wa majimaji haya kama kuteleza, kunata, kuvutika na uzito.
Umeionaje Makala hii.. ?
Je unasumbuliwa na maumivu ya tumbo. Unadhani ni dalili za mimba na ukapima hakuna mimba.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Ugonjwa wa kifafa cha mimba ambapo kwa kitaalamu huitwa eclampsia, utokea pale ambapo Mama anapokuwa na degedege wakati wa mimba na baada ya kujiunga.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kuondoa tatizo la nguvu za kiume
Soma Zaidi...Utajifunza sababua zinazopelekea kuhisi maumivu makali ya tumbo baada ya kumaliza tendo la ndoa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo mtu anapaswa kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili kisiweze kutokea na pia kama jamii ikishirikiana kwa pamoja tunaweza kuepusha kwa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Post huu inahusu zaidi utaratibu wa chakula kwa Mama mjamzito, ni chakula anachopaswa kutumia na ambavyo hapaswi kutumia kwa Mama mjamzito mzito, kwa sababu Mama mjamzito anapaswa kuwa makini katika matumizi ya chakula ili kuweza kuongeza vitu muhimu mwil
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sifa za Ute wa ovulation, ni Ute ambao utokea siku za ovulation yaani siku ambazo ni tayari kwa kubeba mimba, yaani siku za upevishaji wa yai.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zilijitokeza zinaweza kusababisha ugumba hasa kwa wanawake, kwa hiyo ni vizuri kabisa kuwa makini kwa Dalili hizi hasa kwa wadada, kama kuna uwezekano wa matibabu tibu mapema ili kuepuka tatizo la kuwa mgumba.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mapendekezo muhimu kwa wajawazito, haya ni mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu wa afya ili wajawazito waweze kule mimba zao vizuri na kuweza kujifungua vizuri na kupata watoto wenye afya njema na makuzi mazuri pasipokuwepo na ule
Soma Zaidi...