Aina za hijjah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
- Aina za Hijjah.
- Kuna aina kuu tatu za Hijah ambazo Hajj ana uhuru wa kuchagua kulingana na uwezo wake.
- Ifraad.
- Ni aina ya Hijja amapo Hajj anavaa Ihram kwa nia ya kufanya Hijjah tu bila ya Umrah.
- Huanza kwa Talbiya; “Allaahumma labbaykal-Hijja” – ‘Nimeitika kwa Hijjah’
- Hajj huvaa Ihram mpaka amalize matendo yote ya Hija mwezi 10, Dhul-Hijjah.
- Hajj halazimiki kuchinja siku ya mwezi 10, Dhul-Hijah.
- Qiran.
- Ni aina ya Hija ambapo Hajj hunuia kufanya Hija na Umrah pamoja.
- Hajj huitika kwa Talbiya; “Allaahumma labbaykal-Hijja wal-Umrata” – ‘Nimeitika kwa Hijjah na Umrah.’
- Hajj huwa katika Ihram mpaka alenge mawe minara mitatu, atufu Tawaful-Ifaadha na kunyoa mwezi 10, Dhul-Hijjah.
- Hajj analazimika kuchinja mnyama.
- Aina hii ya Hija hufanywa na wakazi wa Makka na wale waliokuja na wanyama.
- Tamattu.
- Ni aina ya Hijah ambapo Hajj hunuia kufanya Umrah tu, kwa kuitika; “Allaahumma labbaykal-Umrah” – ‘Nimeitika kwa Umrah.’
- Hajj huvua Ihram baada ya kufanya matendo yote ya Umrah na kunyoa na kuwa huru na miiko ya Ihram.
- Hajj huvaa tena Ihram siku ya mwezi 8, Dhul-Hija na kuitika; “Allaahumma labbaykal-Hijjah” – ‘Nimeitika kwa Hijjah.’
- Hajj atavua tena Ihram baada ya kutupa mawe na kunyoa mwezi 10, Dhul-Hija.
- Hajj atalazimika kuchinja mnyama siku ya mwezi 10, Dhul-Hija kwa kununua mnyama kama hakuja nayo. Qur’an (2:196).
- Aina hii ya Hija ni bora na nafuu kwa wanaotoka mbali na hawana wanyama wa kuchinja
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Siku zilizoharamishwa kufunga Sunnah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Jukumu la serikali katika kuzuia dhuluma
Serikali ina nafasi kubwa katika kuzuia dhulma na kufanya uchumibuwe huru kuyokana na dhulma.
Soma Zaidi...