ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRI


image


Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu


ALADINI KATIKA PANGO LA UTAJIRI

Mzee akampatia pete Aladini na akamueleza Aladini kuwa utaingia kwenye pango hili, usiguse chochote na elekea mbele zaidi. Utakutana na baraza kubwa sana, mbele yake kuna bostani la mauwa mazuri ya thamani. Katikati utakuta mshumaa. Uchukuwe kwa polepole uje nao.” kisha mzee akaendelea kuzungumza maneno na huku anazidi kukoleza moto kwa maneno yake, ardhi ikaadha utetemeka na Aladini akaanza kuingia. Mwanzoni Aladini alikuwa anaogopa lakini kadiri alivyozidi kuingia ndivyo uoga ulivyo mtoka. Kauli ya kutogusa chochote iliendelea kujirudia masikioni mwa Aladini.

 

Aladini aliendelea kungia katika pango lenyekiza. Baada ya kufika mbele alishangazwa sana kukuta kuna mwangaza asioujuwa nini chanzo chake. Baraza kubwa sana lililosakafiwa kwa madini ya kupendeza sana. Mchanganyika wa madini ulioonyesha sura nzuri sana. Baraza lilikuwa likiwaka kwa ubora wa mpangilio wa rangi zake. Aladini kijana mpumbavu wa mtaani leo yupo sehemu ya ajabu. Baraza liliwa zuri kwa sakafu na dari, ila hali hiyo haikumfanya Aladini asite kuendelea na safari yake.

 

Mbele kidogo Aladini akakuta bostani zuri sana. Bostani lenye matnda na mauwa ya kupendeza. Aladini alishangwazwa sana kuona kuwa yale mauwa na matunda yalikuwa ni madini yanayong’aa na kuning’inia kwa mpangilio wa kupendeza. Madini ya Almasi kwenye mti wa mdizi, yamejipanga kwenye mkungu kama ni ndivi. Hali hii ilitengeneza sura ya ajabu sana na ya kupendeza. Midizi hii ya Almasi ilikuwa na rangi za kupishana zilizo nzuri. Haikuwacha kuwaka, na kuongeza mwangaza kwenye bustani hili.

 

Hali haikuwa kwenye midizi tu bali machungwa yalikuwa ni mawe ya dhahabu yenye kupangiliwa katika miduara yenye kumemeta na kutoa nuru ya kupendeza. Hakika Aladini alipatwa na jambo kubwa sana. Alitamani kuchuma tunda moja lamda aonje aone kama ni dhahabu kweli ana ni matunda tu. Ila kwa muonekano iliweza kuthibitisha kuwa ni dhahabu, kila tunda lilikuwa na rangi zke za kupendeza. Aladini alitamani siku moja aweze kuishi katika sehemu hii. Michungwa iliyojipanga vyema kwenue mistari ilifuatiwa na mauwa mazuri.

 

Mauwa haya nayo yalikuwa ni madini yenye rang tofauti tifauti za kupendeza. Aladini alishangazwa na kuona kuwa hata nyuki waliokuwa wakipepea kwenye mauwa walikuwa ni dhahabu tupu. Aladini ilibidi aangalie vyema hapo akagunduwa kuwa mzinga wa nyuki uliopo jirani nao ni dhahabu tubu. Mwangaza mzuri ulikuwa ukiwaka katikati ya mzinga ule. Vitone vyenye rangi za kupendeza vilikuwa vikishuka kutoka kweye mzinga. Aladini masikini na njaa aliyo nayo alitamani kwenda kukinga ulimi. Ila sauti ya mzee ilijirisia “usiguse chochote”.

 

Hali haikuwa kwenye mauwa na nyuki pia Aladini alishuhudia kabati kubwa lililopo katikati ya bustani. Kabati ilo lilikuwa na bilauri nzuri na za kupendeza. Bilauri zenye maji yenye rangi ya fedha (silva). visahani vyenye rangi ya hudhurungi na mauwa ya kupendeza. Birika tatu kubwa zenye rangi nzuri, maandishi ya kiarabu yaliyopangiliwa vyema yaliandikwa kwenye mabirika hayo. Aladini alishikwa na butwaa ana asijuwe nini afanye.

 

Aladini aliendelea mbele kidogo akakuta kuna meza lingine kubwa. Meza hilo lilikuwa na taa ya mchumaa. Taa hiyo ilikuwa ikiwaka bila kutoa moshi. Moto wake ulikuwa na rangi zenye kupishana na za kupendeza. Aladini aligunduwa kuwa mwanga wote unaopatikana humu ndani ulitokana na kamshumaa hako. Aladini akauendea mshumaa na kuunyakuwa kwa upole sana. Alipoushika mshumaa mwangaza wote pale ndani ukazima. Na rangi nzuri na ya kupendeza aliyokuwa akiiona ikageua kuwa kiza la kutisha.

 

Mwangaza mdogo uliotokana na pete yake ndio uliokuwa ukimsaidia. Aldini akaanza kutoka kwa araka na kwa umakini zaidi. Alipokaribia kutoka tu yule mzee akataka Aladini ampatie ule mshumaa kwa kuurusha. Aladini alikataa kwa sababu ya kuwa mpaka atoke salama ndipo ampatie. Jambo hili lilikuwa ni kinyume na alivyotarajia huyu mzee. Ukweli ni kuwa mzee alitaka amtumie Aladini kupata mshumaa kisha amuuwe humohumo. Mzee alivyoona hapa atakosa yote akaamuwa afunge pango ili aladini afio humohumo. Mzee bila ya kuchukuwa pete yake kwa Aladini alifunga pango kwa uchawi na kutimua zake. Na kumuacha Aladini kwenye pango lenye giza, akiwa na njaa kali. Aladini aliendelea kulia, kujuta na asiwe na njia ya kutoka nje.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    2 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Jifunze fiqh       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image NIMLAUMU NANI ( sehemu ya tatu)
Post hii inahusu mwendelezo wa hadithi ya kijana Frank na Amisa pia na wapenzi wawili ambao ni James na Amina. Soma Zaidi...

image Hadithi ya mvuvi na jini
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image NIMLAUM NANI? (Sehemu ya pili)
Post hii ni mwendelezo wa hadithi iliyopita ambapo Frank aliwakuta Amina ambaye ni mpenzi wake ameumbatiana na James ambaye ni rafiki yake ,kwa hiyo tuendelee kusikia yaliyotokea baada ya Amina na James kukutwa na Franki. Soma Zaidi...

image NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na kusalitiwa mara kwa mara. Soma Zaidi...

image Kifo cha mtoa burudani wa sultani
Posti hii inakwenda kukusimulia kuhusu hadithi ya kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Familia mpya baada ya harusi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Ndoto ya mgonjwa, binti mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme
Posti hii inahusu zaidi mwendelezo wa hadithi ya Binti mfalme, tunajua kuwa mama yake na binti alimtorisha yule binti mbali kabisa ila kijana naye aliamua kutoroka na kumfuata binti mfalme na hatimaye akampata alipo. Soma Zaidi...

image Mtoto wa tajiri na mtoto wa maskini ( sehemu ya nne)
Post hii inahusu zaidi watoto Hawa wawili wakiwa kwenye kituo cha mapumziko ambapo mtoto wa tajiri anabugia soda aliyopewa na yule mwalimu pia tumbo linaanza tena na anaanza kuendesha Soma Zaidi...

image Usuluhishaji wa walio dhurumiwa
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...