Asbab nuzul surat at Tin,  Sababu za kushuka surat at Tin (watin wazaitun)

Asbab nuzul surat at Tin, Sababu za kushuka surat at Tin (watin wazaitun)

Post hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa surat at Tin (watin wazaitun).

Surat at Tin ni sura ya 95 katika mpangilio wa Quran kama ilivyoandikwa kwenye Mashaf. Sura hii ina aya 8 na imeshuka Makkah. Mtume s.a.w alikuwa akiisoma sura hii wakati anaposwali swala ya safari. 

 

Amesimulia Ala Baraa bin Azib kuwa alikuwa Mtume s.a.w akisoma katika swala za safa katika moja ya rakaa mbili alikuwa akisoma surat at Tin (watin wazaytun)…… 

 

Sababu za kushuka kwake. 

Hakuna nukuu hasa za kuonyesha kama kulikuwa na tukio maalumu lililopelekea kushuka sura hii. Kuna baadhi ya kauli ni kuwa kuna swahaba alimfuata Mtumr s.a.w navkumuuliza kuhusu watu ambao ni wazee, na wana matatizo ya kusahau, ama ya akili, vipi amali zao je wataendelea kulipwa? Hapo ndipo ikashuka sura hii. 

 

Sura hii imrjibu vyema swali hilo. Allah anasema wale waliokuwa na imani na kufanya matendo mema basi wana wao malipo yasiokatika. 

 

Maana ya tin, zaitun na mlima sinai

Wametofautiana wafasiri kuhusu maana ya tin na zaitun. Wapo waliosema kuwa hii ni misikiti, yaani msikiti wa Damaska na wa palestina Bayt al Maqsid. 

 

Ila uhakika wa maneno na kaulicyenye nguvu makusudio hapa ni matunda mawili haya yani tunda Tini na tunda Zaituni. Matunda haya yanafahamika kwa kuwa navladha nzuri na manufaa makubwa kwa afya. Allah anaapia kwa kitu chochote kile akitakacho. 

 

Makusudio ya mlima sinai, huu ni mlima ambao Nabii Musa alikuwa akizungunza na Allah. Na Mji wa amani uliotajwa makusudio ni Makkah ambapo kuna msikito mtukufu zaidi.  

 

Ujumla wa sura hii

Sura hii Allah ameanza kuapa kisha akatupa masingatio kuwa hakika mwanadamu ameumbwa katika umbo zuri. Kisha akatupa mazingatio kuwa mwanadamu huyu aliyekuwa katika umbo zuri endapo atafanyavmatendo mema atabakia katika hadhi yake ya juu. Na endapo atamuasi Allah atushushwa awe na hadhi ya chini kabisa katika wenye hadhi za chini. 

 

Allah akatupa mazingatio menginr kuwa wale wanaomuamini Allah ana kufanya matendo mema wana wao malipo yasiokatika. 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Views: 4776

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Sababu za kushuka surat Ikhlas

Surat Ikhlas ni katika sura za kitawhid ambazo zilishuka miaka siku za mwanzoni mwa utume. Sura hii imekuja kujibu maswali mengi kuhusu Allah ikiwemo, Allah ni nani?

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Darsa za Quran

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat al bayyinah

Asbab nuzul surat al bayyinh. Sura hii imeteremka Madina na ina aya nane.

Soma Zaidi...
Fadhila za kusoma surat al Fatiha (Alhamdu)

Post hii inakwenda kufundisha fadhila na faida za kusoma Alhamdu.

Soma Zaidi...
Makundi ya Id-ghamu katika usomaji wa Quran Tajwid

Kama tulivyoona kuwa id-ghamu ipo katika aina kuu mbili ambazo ni id-ghamu bighunnah na id-ghamu bighair ghumnah. Sasa hapa tutajifunza makundi mengine ya idhgamu.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa surat Dhuha

Sura hii imetermka Makkah na ina aya 11. Sura hii ni moja ya sura ambazo zimeshuka mwanzoni wakati ambapo Mtume ameanza kazi ya utume.

Soma Zaidi...