Athari za kumuamini mwenyezi Mungu katika maisha ya kila siku

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Muumini wa kweli huishi katika kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w), na hii kama ifuatavyo;

 

  1. Kupata ukombozi kutokana na utumwa wa aina zote;

Huu hupatikana baada ya mtu kuwa huru na kuishi kwa kufuata taratibu na kanuni alizoweka Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.

Rejea Qur’an (12:39).

 

       (ii)  Mwanaadamu huwa mwadilifu katika utendaji wa maisha yake ya kila siku;

Muumini wa kweli hufanya mema na kuepuka maovu bila hata ya kusimamiwa au      kuonekana na watu, kwa kujua kuwa mjuzi pekee ni Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (50:16).

 

        (iii)  Humfanya mwanaadamu kuwa mpole, mvumilivu na mwenye huruma;

Mwanaadamu huwa mpole hasa kwa wenye shida na matatizo na pia kuwa na subra anapofikwa na mitihani na kujiepusha na kibri, majivuno na kujiona.

Rejea Qur’an (6:165).

 

     (iv)  Humfanya mja kuwa jasiri katika kusimamia haki, uadilifu na usawa katika jamii;

Muumini wa kweli huwa shujaa katika kupambana na dhulma na ukandamizaji wa aina yeyote na kupigania haki bila kumchelea mtu yeyote.

Rejea Qur’an (4:74), (5:45) na (9:111).

 

        (v)  Humfanya mja kuwa na mtazamo mpana na sahihi juu ya maisha;

Muumini wa kweli kamwe hawi na fikra na mtazamo finyu katika kuyaendea maisha yake ya kila siku kwa kujua lengo, thamani na nafasi yake juu ya maisha ya Akhera.

Rejea Qur’an (15:9).

 

        (vi) Humuwezesha mja kuwa mwenye kukinai na kutosheka;

Muumini wa kweli hutosheka na kuridhika na kile alichokadiriwa na Mwenyezi Mungu (s.w) iwe kwa kupungukiwa au kuzidishiwa, yote kwake anashukuru.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/15/Saturday - 07:29:36 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1359

Post zifazofanana:-

Vita vya uhudi
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Elimu Yenye Manufaa
Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa. Soma Zaidi...

Sababu za Quran kuwa mwongozo sahihi wa maisha ya mwanadamu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Swala ya jamaa.
Kipengele hiki tutajifunza kusimamisha swala ya jamaa,swala za ijumaa. Soma Zaidi...

Kutoa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kumuamini mwenyezi Mungu..
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sababu za kushuka kwa surat al qariah
Surat Al qariah, ni moja katika sura zilizochuka miaka ya mwanzoni mwa utume. Soma Zaidi...

Kwanini lengo la funga halifikiwi na wafungaji wengi
Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Nguzo za imani
Zifuatazo Ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Viraa saba na herufi saba katika usomaji wa quran
Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran Soma Zaidi...