Athari za mkojo mwilini.

Posti hii inahusu zaidi athari za mkojo mwilini, kwa kawaida tunafahamu kwamba mkojo ni matokeo ya mkusanyiko wa uchafu wa maji maji yanayokusanyika kutoka mwilini ikiwa mkojo umebaki mwilini usababisha madhara mbalimbali kama tutakavyoona.

Athari za mkojo mwilini.

1. Kitendo cha mkojo kubaki mwilini ninmatokeo ya Figo kushindwa kufanya kazi kwa hiyo mkojo ujaa kwenye damu, yaani ni kama vile umejikojolea kwenye damu, kwa hiyo uchafu wote ukaa mwilini na kuchanganyikana na damu hali inayopelekea mwili mzima kujaa mkojo.

 

2. Hali hii ya mkojo kujaa kila sehemu kwenye damu usababisha kuhathiri kila kiungo kwenye mwili, kwa sababu damu ikisafiri usafiri na mkojo kwa hiyo viungo vyote uathiriwa kama vile moyo, ubongo, tumbo na sehemu zote za mwili ambapo damu upita uathiriwa na Sumu ya mkojo.

 

3. Kwa hiyo kila kiungo cha mwili ujaa maji, yaani kuvimba, utakuta miguu imevimba macho yamevimba, tumbo limejaa maji,na pia mapafu nayo ujaa maji hali inayosababisha mwili wa mgonjwa kuwa na hali mbaya zaidi, pia mgonjwa huwa na kichefuchefu  kwa sababu ya mwili kujaa maji na kwa wakati mwingine kutapika damu.

 

4. Kwa hiyo mgonjwa hasipopota matibabu mapema anaweza kufikia pabaya , baada ya kuona dalili kama hizi ni vizuri kabisa kuwahi hospital Ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kutokea.

 

5. Na pia ni vizuri kuanza mahudhulio kwenye kuosha Figo kwa sababu pamoja na dawa ndiyo njia pekee ya kuondoa Sumu ya mkojo kwenye damu.

 

6. Pamoja na hayo no vizuri kabisa kutumia maji mengi kabla haujaugua pamoja na kujiepusha na vyakula vya kemikali ambavyo ndicho chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Figo ni vizuri kabisa kulinda afya zetu kwa sababu gharama ya kuosha Figo ni kubwa mno ambayo ni Wachache wanaweza kupata.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/11/Monday - 01:05:11 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 895


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-