Posti hii inahusu zaidi athari za ugonjwa wa Dondakoo,hali hii utokea iwapo ugonjwa haukutibiwa mapema au umetibiwa lakini bado Kuna matokea hasi ambayo yanaweza kujitokeza kama ifuayavyo.
1. Kupumua vibaya kwa mtoto na pengine mtoto anashindwa kumeza au anameza kwa shida.
Ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtoto zinaweza kuwa za kudumu au kwa mda tunajua kuwa ugonjwa huu ushambulia Koo mara nyingine Koo linapata maambukizi makubwa ambayo usababisha mtoto kushindwa kabisa kumeza au wengine wanafaulu kumeza Ila kwa shida kwa hiyo tunapaswa kutibu ugonjwa huu mapema na Tiba yenyewe ni kumpeleka mtoto kupata chanjo kwa kufanya hivyo tutapunguza shida kwenye jamii na watoto tunawaandalia maisha mazuri na yenye natumaini.
2. Kupooza kuanzia kwenye paji la uso mpaka shingoni, kwa sababu ya kuenea kwa bakteria katika sehemu mbalimbali za mfumo wa hewa maambukizi hayo ufanya sehemu hizo kupooza yaani kuanzia kwenye sehemu ya paji la uso mpaka shiy kwa hiyo tunaona hali hii ni ya kuuumiza hasa kwa mtoto na kumsababishis ulemavu wa kudumu kwa sababu zisizi za msingi kama vile Imani potofu juu ya chanjo au kufanya uzembe katika kumpeleka mtoto kupata chanjo kwa hiyo mtoto anakosa furaha na kupata ulemavu wa kudumu katika maisha yake.
3. Maambukizi yanaenea sana .
Kama ugonjwa huu haujadhibituwa usababisha maambukizi kwa watu wengine na kuleta madhara makubwa ambayo yanawaletea wengine ulemavu wa kudumu ambapo kama na wenyewe hawajatambua dalili mapema wanaweza kuendelea kuishi nao, basi jamii inapaswa kujua wazi dalili za ugonjwa huu wa Donda Koo na kujiadhari mapema kuhusu ugonjwa huu.
4. Kwa Sababu ya kuwepo kwa maumivu makali kwenye shingo, kushindwa kumeza na kupumua kwa mtoto, kuvimba shingo kwa mtoto na kupooza kwa mtoto kifo kinaweza kutokea ikiwa mamb o haya haya kutibiwa mapema, kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua kuwa Dondakoo ni hatari kwa watoto na kuhakikisha kuwa kila mtoto anapata chanjo na kama Kuna Imani potofu kuhusu chanjo jamii inabidi kuwa macho Ili kuondoa Imani hizi potofu.
5. Chanjo ambayo utolewa ni mchanganyiko wa chanjo ya kuzuia kifaduro, Pepopunda, Homa ya inni, hima ya uti wa mgongo, kwa Jina Moja huitwa pentavalent. Kwa hiyo mama au walezi wanaweza kuuliza wataalamu wa afya Ili kuhakikisha kama watoto wao wamepata chanjo ya Dondakoo Ili kuepusha madhara mbalimbali katika jamii yetu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa kipindupindu.Ni dalili zinzojitokeza kwa magonjwa wa kipindupindu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo VVU huambukizwa
Soma Zaidi...Hivi umeshawahi kuwazakuwa jekipimo cha HIV ni sahihi kwa kiasi gani. Unadhani huwa kinakoseaga kutoa majibu?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi juu ya ugonjwa wa Bawasili, ni ugonjwa unaotokea kwenye njia ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa uvimbe au nyama ambazo uonekana hadi nje, kwa lugha ya kitaalamu ujulikana kama haemorrhoid au pokea.
Soma Zaidi...Huu ni ugonjwa wa fangasi wanaosababishwa na mashambulizi ya fangani aia ya yeast waitwao candida.
Soma Zaidi...DAWA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO Dawa za kukabiliana na zaidi ambazo zina calcium carbonate (Tums, Rolaids), zinaweza kusaidia kutibu vidonda vya tumbo lakini hazipaswi kutumiwa kama matibabu ya msingi.
Soma Zaidi...Manung'uniko ya moyo ni sauti wakati wa mzunguko wa mapigo ya moyo wako kama vile kutetemeka inayotolewa na damu yenye msukosuko ndani au karibu na moyo wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa usafi katika maisha ya mwanadamu au mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za kupunguza maumivu na kazi zake, ni dawa ambazo upunguza maumivu kwenye mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Magonjwa ya kuambukiza, ni magonjwa ambayo yanaweza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kuweza kusababisha madhara yale yale kwa mtu aliyeambukizwa au anayeambukiza kwa hiyo Maambukizi yanaweza kuwa ya moja kwa moja au yasi
Soma Zaidi...