Athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa wajawazito

Post inahusu zaidi athari za Ugonjwa wa herpes simplex kwa wajawazito au ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri.ugonjwa huu uleta madhara kwa wajawazito kama tutakavyoona

Athari za Ugonjwa wa herpes simplex  kwa  wajawazito au ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri 

1.Ugonjwa huu usipotibiwa unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na kusababisha  madhara kwa wajawazito kama hawataweza kuutibu mapema.

 

2.Ugonjwa huu Usababisha mimba kutoka kwa wajawazito, tunajua wazi kwamba Ugonjwa huu usababishwa na virusi kwa hiyo kama hautatibiwa mapema unaweza kuingilia kwenye sehemu ya mfuko wa uzazi na kuufanya ukalegea na mimba ikatoka.

 

2. Pia ugonjwa huu Usababisha Mama kujifungua mtoto ambaye hajafikisha umri kwa sababu virusi wakishambulia kwenye plasenta na kusababisha mfuko wa uzazi mtoto anaweza kuzaliwa kabla ya wakati.

 

3. Pia kwa wajawazito mtoto tumboni anaweza kuchelewa kukua hali ambayo upekea mtoto kuzaliwa na umri wa miezi tisa lakini ana ka umbo kadogo sana kwa hiyo hali hii ikitokea ni lazima kupima ugonjwa huu na baadaye kuendelea kumhudumia mtoto.

 

4. Pia ugonjwa huu unaweza kutoka kwa mama mwenye mimba na kwenda kwa mtoto akiwa tumboni kwa hiyo kama mama ana mimba ni vizuri kufanya vipimo vya afya mara kwa mara kuangalia kama kuna Maambukizi yoyote kwa kufanya hivyo tunaweza kuokoa watoto kwa sababu watoto ni kama malaika Magonjwa haya uwashika kwa sababu ya uzembe wa wazazi kushindwa kuchukua vipimo muhimu wakati wa ujauzito.

 

5.Kwa hiyo baada ya kujua kwamba Ugonjwa huu unaleta matatizo mbalimbali kwa watoto hasa wanapokuwa tumboni ni vizuri kuelimisha jamii namna ya kujikinga na kusababisha kufanya vipimo vya mara kwa mara kwa wanawake wajawazito



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/02/24/Thursday - 04:25:08 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 800


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-