picha

Bawasili usababishwa na nini?

Posti hii inahusu zaidi visababishi vya ugonjwa wa Bawasili,kuna watu wengi wanapenda kujua kabisa chanzo cha kuwepo kwa ugonjwa wa Bawasili kwenye jamii na kuna maswali mengi yanayoulizwa kuhusu visababishi vya Bawasili.

Visababishi vya ugonjwa wa Bawasili.

1. Kufunga choo au kukosa choo kwa mda mrefu.

Hii ni sababu ya kwanza kabisa kwa sababu kuna watu ambao hawapati choo au wanabana choo kwa mda mrefu na usababisha kuwepo kwa Bawasili.

 

2. Wakati wa ujauzito.

 Wakati wa ujauzito kuna uwezekano wa kupata ugonjwa wa Bawasili kwa sababu ya kuwepo kwa mgandamizo wa mtoto kupelekea kwenye na sehemu ya haja kubwa , na pia wakati wa kujifungua mtoto anakandamiza sana sehemu ya haja kubwa.

 

3. Kufanya mapenzi kinyume cha maumbile.

Kuna kipindi watu wanapenda kufanya mapenzi kwenye sehemu ya haja kubwa hali ambayo upelekea kuwepo kwa Bawasili.

 

4. Uzee.

Pia nao wana uwezekano wa kupata tatizo hili la Bawasili kwa sababu mtu akiweka na kinga za mwili zinashuka hali ambayo Usababisha kupata ugonjwa huu.

 

5. Pia kuna sababu za kurithi.

Kwa kawaida kuna familia ambayo upata ugonjwa huu mara kwa mara kutoka kwa babu , baba na majukumu kwa hiyo kuna uwezekano wa kupata kama ugonjwa umo kwenye familia.

 

6. Kuharisha sana na kwa mda mrefu.

Kuna watu ambao wanapatwa na tatizo la kuharisha sana na kwa mda mrefu nao wana uwezekano wa kupata ugonjwa huu wa Bawasili.

 

7. Matumizi ya vyoo vya kukalia.

Kuna uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa huu kwa sababu ya matumizi ya vyoo vya kukalia kwa mda mrefu ingawa sio wote wanaotumia vyoo hivi kupata Bawasili.

 

8. Kunyanyua vitu vizito.

Kuna wakati mwingine watu wenye tabia ya kunyanyua vitu vizito wamo hatarini kupata ugonjwa huu wa Bawasili.

 

9. Kuwepo kwa mfadhaiko au stress.

Kwa kuwepo kwa mfadhaiko wa mara kwa mara usababisha magonjwa mbalimbali ikiwemo na Bawasili.

 

10. Kuwepo kwa uzito mkubwa na unene wa kupitiliza, kwa kawaida watu wanene na wenye uzito uliopitiliza usababisha kuwepo kwa magonjwa mbalimbali na wako hatarini kupata Bawasili.

 

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2022/07/09/Saturday - 03:14:22 pm Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 2224

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 web hosting    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Koo langu limekauka yaweza kuwa ni muadhirika?

kuwashwa na koo ni katika dalili za kuwa na maambukizi mwilini. Kuwa na maambukizi haimaanishi ni HIV ama UKIMWI laa hili ni neno pana. Hapa nitakujuza kwa ufupi kuhusu swali hilo la muulizaji kuwa anawashwa na koo.

Soma Zaidi...
Sababu za Kutokwa Damu moja kwa moja bila kuganda (hemophilia).

Posti hii inaelezea kuhusiana na Damu kutokuganda ambalo hujulikana Kama Hemophilia, ni ugonjwa nadra ambapo damu yako haigandi kawaida kwa sababu haina protini za kutosha za kuganda. Ikiwa una tatizo la Damu kutokuganda, unaweza kuvuja damu kwa muda mre

Soma Zaidi...
Dalili za kisukari na njia za kuzuia kisukari

Posti hii inaelezea ugonjwa wa kisakari, dalili zake,na namna ya kujikinga usipate kisukari au Kama tayari unakisukari ukijikinga madhara yanapungua au kupona kabisa.Kisukari au bolisukari (jina la kitaalamu: diabetes mellitus) ni ugonjwa unaoonyesha viwa

Soma Zaidi...
MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO Matibabu ya vidonda vya tumbo inategemea sababu.

Soma Zaidi...
Homa ya ini Nini Nini, na husababishwa na nini

Katika post hii utajifunza maana ya homa ya ini. Pia utajifunza chanzo kinachosababisha homa ya ini. Makala hii itakuwa endelevu hivyo usikose muendelezo wake.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo

Posti hii inaonyesha namna ya kujizuia,Mambo ya Hatari,na na Mambo yanayopelekea Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo

Soma Zaidi...
Dalili za malaria

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya dalili za maralia

Soma Zaidi...
Madhara ya kuwepo Kwa usaha kwenye mapafu

Post hii inahusu Zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea Kwa mgonjwa mweye usaha kwenye mapafu.

Soma Zaidi...
Kichwa kinaniuma mbele sielewi nini

Zijuwe sababu za kuumwa nankichwa upande mmoja wa kichwa.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa kisonono, sababu zake nanjia za kujilinda.

Kisonono husababishwa na bakteria. Bakteria ya kisonono mara nyingi hupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine wakati wa kujamiiana, ikiwa ni pamoja na kujamiiana kwa mdomo, mkundu au uke.

Soma Zaidi...