image

Binti huyu Ni Nani?

Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan

BINTI HUYU NI NANI?

Siku iliyofuata nilioga mapema, kisha nikavaa ngu zangu safi na kuelekea pale dukani. Loo! Yule binti akaja tena, alipokuja moja kwa moja akakaa karibu nami na kutoa kitambaa kilichofungwa bundu. Kisha akaniambia “ Chukuwa hii malipo yako kwa bidhaa yako siku ya jana”. nikachukuwa na kumpatia muuzaji wangu ahifadhi. Sikuwa na haja ya kuhakiki kama pesa imetimia ama laa.

 

Basi nikaendelea kuzungumza naye maneno ya hapa na pale. Kisha nikaanza kuchomekea maneno ya ishara. Bila shaka alizifahamu vyema ishara zangu. Kwa ghafla alionyesha kukasirika na ndipo alisimama na kuondoka zake. Nilijijutia nafsi yangu kwa nini nimeongea naye kwa ishara za mapenzi. Aliondoka tena bila hata kuniambia anaitwa nani na wapi anakaa. Aluondoka hata sijazungumza hasa nini kipo moyoni kwangu.

 

Hakika siku hiyo niliiona ndefu sana na sikuweza kula chochote. Nilipata pia kujiwazia huenda binti yule sio mtu wa kawaida, huenda ni jini ama malaika ametumwa kuja kunijaribu. Siku ya tatu yake nikaamua kutembea mjini nkiamini huenda nikakutana naye kwa bahati mbaya. Loo! Sikuiliisha bila hata kukutana na sura yake.

 

Siku ya nne nilikaa kenye duka lile na ghafla akanijia bibi mmoja. Akanieleza kuwa ameagizwa na bosi wake aje anichukuwe ana mazungumzo. Bibi alikuwa ni mjakazi katika jumba la kitajiri. Nilifahamu hilo baada ya kuona mavazi yake. Nilikubali wito kwa kuamini atakuwa ni yule mrembo aliyeteka hsia zangu, aliyechukuwa moyo wangu, aliyenikosesha hamu ya kula wala kulala.

 

Niliongozana na bibi yule hata tukafika kwenye nyumba ya wageni. Hap akanieleza niingie kwani bosi wake yumbo ndani. Nilipoingia tu nikakaribishwa na manukato yanayonukia kwa uzuri sana, Loo! Alikuwa ni yule mrembo, alikuwa amependeza sana siku hii. Alvaa mavazi marefu yenye rangi za kuvitia kama tausi. Akanikaribisha kwnye busati lililotandika katikati ya chumba.

 

Hapo wakaja mabinti wengine wawili vigori, wakaleta vinywaji na kukaa pembeni. Akanieleza kuwa hawa pia ni wafanya kazi wake. Hawezi kukaa peke yake kwani faragha ya mwanaume na mwanamke wasio oana hairuhusiwi kwenye dini. Basi tulianza kuzungumza hapa na pale wakati huo mabinti wale wapo. Mwisho niamueleza uhalizi wa moyo wangu juu yake, ni kiasi gani ninampenda, ni taabu gani nimeipata kwa siku tatu hizi toka niutane naye.

 

Nilimueleza vyeote kuhusu kuwa sikuwa na usingizi wala sikuona tamu ya chakual. Wakati wote niliokuwa nachungumza yeye alikuwa akitokwa na machozi tuu. Moja wa mabinti wale akachukuwa kitambaa cha hariri kilicho zungushiwa na dhahabu nyekundu, na kutiwa manukato yanayonukia kama miski nyekundu ya kutoka india. Alimfuta machozi kisha akasema “ kwa hakika unayoyasema ndiyo yaliyomkuta bosi wetu, toka majuzi anakazi ya kukuwaza, kukutaja, kukufikiria, hali, halali, hanywi kwa upendo alionao kwako”.

 

Nilitamani kumfuta machozi ila nikaogopa kumvunjia heshima mbele ya wafanyakazi wake. Ndipo akasema kuwa “ kwa hakika walioyasema ndugu zangu ni sahihi, wewe ni mtu wa kwanza kukupenda, na amini nakupenda kweli, naomba tuoane. Kwani siwezi kukukosa tena, siwezi kuonja tena adhabu ya kuwa mbali nawe, uso wako kama lulu kwangu, katu sichoki kukutazama, tabasamu lako…… mmmhmmh nakupenda sana.”

 

Basi aliendelea kuzungumza kisha tukakubaliana kuwa tuoane ila ndoa iwe kwa siri kwa sababu, mimi ni mtu ambaye bado ni mgeni hivyo haitakuwa vyema kutangaza harusi yetu, na mimi ninatambulikamkwa utajiri nilio nao, hivyo wanaweza kukufanyia fitina, na hata kukuumiza. Siku ilofata ilikuwa ni ijumaa. Basi akanielekeza kwake ili niende baada ya kuswali ijumaa ili ndoa ikafanyike. Basi tukaagana pale na mimi nikaondoka na wao wakaelekea zao.

 

Sikuwa na haja tena ya kulijuwa jina lake maana niliamini kuwa nitalijuwa siku ya harusi. Nilijuwa kuwa yeye ni tajiri na ni mtoto wa tajiri. Niliamini ili niweze kuishi naye ni lazima nitumie pesa vyema. Basi siku hiyo sikuweza tena kulala kwa kuisubiri asubuhi ifike, ili nikamuoe kipenzi maridhawa.           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-11-07 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1041


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Viatu vya ajabu
VIATU VYA AJABU VYAONDOKA NA MKONO WANGU Aliponieleza sifa za viatu anavyotaka nikamsogelea kwa ukaribu na kumkazia macho kama nataka kumpiga vile kisha nikamuuliza “wewe ni nani, na ni nani amekutuma, vina nini hasa viatu hivi” alibakia kimya ... Soma Zaidi...

JARIBIO LA KWANZA LA ALADINI
Soma Zaidi...

Hadithi ya aliyekatwa vidole gumba
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Historia ya pango, aladini na kitabu
Soma Zaidi...

Siri ya kifo yafichuka
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

HADITHI YA TUNDA EPO
Soma Zaidi...

Hadithi ya Kaka wa nne wa kinyozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

Hatma ya kijana mchonganishi
Soma Zaidi...

Ujumbe wa Siri kwenye kitabu cha ajabu
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Harusi ya aladini na binti sultani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Jaribio la tatu la aladini
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

Penzi la Mitihani
MTIHANI PENZINI Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Soma Zaidi...