image

Changamoto za ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu

CHANGAMOTO ZA UAJAUZITO NA DALILI ZENYE KUENDELEA:

Ni vyema sana kutambuwa hili, kwani itakusaidia katika klujuwa changamioto za ujauzito. Katika dalili hizi za ujauzito zipo ambazo nio zenye kuendelea. Na katika kuendelea hko wengi katika wajawazito wanapatwa na changamoto kadhaa. Hapa nitakueleza nini cha kufanya.

 

1.KichefuchefuKichefuchefu kinaweza huweza kuchelewa kujitokeza lakioni kinaweza kuwa ni chenye kuendelea. Kwa baadhi ya wanawake kinaweza kwenda mpka miezi kadhaa mbele, ila kwa wengi kinaweza kukata kufikia wiki ya 28. Hii ni changamoto kwakweli kwa wajawazito. Maana kichefuchefu kinaweza lumkoseshea amani wakati mwingine.hali ya kutema mate, kuhisi kutapika ama kichefuchefu kwa ujumla huwasumbua wajawazito. Wataalamu wanaeleza kuwa hasa chanzo cha kichefuchefu ni mabadiliko ya homoni mwilini. Na huwenda pia kuna sababu nyingine.

 

Kama utakuwa unasumbuliwa na hali hii fanya hivi. Epuka kukaa maeneo yenye joto sana. Epuka kunywa maji wakati unakula. Tumia tangawizi, kwenye chai ama tafuna. Unaweza kuiweka kama unga ama vipande vidogovidogo. Unaweza kutumia bigjii maalumu kwa ajili ya wajawazito.

 

2.Maumivu ya tumbo:Kwa wajawazito maumivu ya tumbo mara kwa mara ni hali ya kawaida na yenye kuendelea. Maumivu haya yanaweza kuchukuwa muda mchache na kuondoka. Pia ni yenye kuvumilika yaani mwanamke anaweza kuendelea kufanya shughuli zake. Ila endapo yatakuwa ni makali sana kutovumilika inaweza kuashiria kuna shida kwenye afya ya mwanamke huyu. Ni vyema kufika kituo cha afya kupata ufafanuzi wa hali.

 

Katika hali ya maumiovu haya ya tumbo mwanamke anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia zipo tiba mbadala kupunguza maumivu. Ila mwanamke awe makini sana maana anaweza kuingia katika hatari endapo atatumia dawa kiholela.

 

3.Kutokwa na damu:Kama ilivyo dalili nyingine huendelea basi si jambo ;la kushangaza kwa mwanamke mjamzito kujikuta nguo yake ya ndani kuwa na vitone vya damu. Damu hii si yenye kuchuruzika ama yenye kutoka kwa wingi kama damu ya hedhi. Endapo mjamzito atakuwa anatokwa na damu nyingi eidha iambatane na maumivu makali ya tumbo ama isiambatane ni vyema awahi kituo cha afya kupata uthibitisho juu ya mabadiliko hayo. Maana wakati mwingimne damu inaweza kuashiria shida katika ujauzito.

 

4.Mabadiliko katika hisia, matakwa na matamanio katika vyakula na vitu vingine.Haswa mwanamke anaweza kujishangaa mwenyewe inakuweje hali hii. Mwanamke anaweza kuona kuwa nachukia vitui ama kuna watu anawachukia ghafla. Wakati huo huo anaweza kupenda mtu flani sana. Pia kuna wakati atakuwa anachukia baadhi ya vyakula na vitu vingine. Yaani kwa ufupi ni mabadiliko tu katika saikolojia yake. Huu si ugonjwa hivyo hali hii isimpe mawazo saana mwanamke. Watu walio karibu na wajawazito wawe makini pia maana wanaweza kufanya makosa makubwa kama kumpiga na vinginevyo.

 

5.Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu.Yes hii ni changamoto kwa kweli. Hii haiwapati wenye mimba ya miezi ya mwanzo, hali hii hutokea wakati mimba imesha komaa miezi ya mbeleni. Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu kwa wajawazito sio jambao la ajabu. Hali huweza kukaa sawa atakapojifungua. Kama mwanamke anasumbuliwa na hali hii, ahakikishe anapumzika katika maeneo yenye utulivu na yaliyopa yaani aepuke kukaa maeneo yenye joto. Pia aepuke kubvaa nguo za kabana. Aepuke kukaa chini katika mkao mmoja kwa muda mrefu.

 

6.Kuenda haja ndogo mara kwa mara.Hii ji changanmoto hasa kwa wale ambao ndio ujauzito wao wa kwanza.Hapa pia kuna wajawazito wanajitahidi kujizuia eti wapunguze kuenda haja ndigo. Hii sio sawa kabisa. Mjamzito anatakiwa anaposikia haja kakaitoe wala asihofu kitu huu si ugonjwa na ni kawaida kabisa. Kwa kuwa moyo wake umeongeza utendaji wa kazi hivyo uchujwaji wa damu ni mkubwa. Kwa maendeleo mema ya afya yake na afya ya ujauzito wake, mjamzito asihofu kitu, aende tu haja.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1574


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Faida za Uzazi wa mpango
Posti hii inazungumzia Faida za Uzazi wa mpango kwa watoto, mama, wanandoa, na jamii au JUMUIYA. Soma Zaidi...

Malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama.
Posti huu inahusu zaidi malengo ya huduma za uzazi kwa akina Mama, ni huduma muhimu ambazo zimetolewa kwa akina Mama ili kuweza kuepuka hatari mbalimbali zinazowakumba akina Mama wakati wa ujauzito, kujifu na malezi ya watoto chini ya miaka mitano. Soma Zaidi...

Dalili za kujifungua hatua kwa hatua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kujifungua hatua kwa hatua Soma Zaidi...

Ni zipi njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukuletea njia za kutatua tatizo la nguvu za kiume Soma Zaidi...

Dalili za mimba katika mwezi wa kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza Soma Zaidi...

Dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.
Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi. Soma Zaidi...

Mimi imepita miezi mitatu sioni hedhi na wala sioni dalili ya kuwa na mimba unaweza ukaniambia tatizo la kuwa na hali hii
Kama na wewe una tatizo la kupitiliza siku zako za hedhi hli ya kuwa huna ujauzito, soma post hii ina majibu yako. Soma Zaidi...

dalili za uchungu kwa mama mjamzito
Makala hii itakwenda kukufundisha baadhi ya dalili za uchungu kwa mama mjamzito. Soma Zaidi...

Njia za kuongeza nguvu za kiume
Somo hili linakwenda kukueleza njia za kuongeza nguvu za kiume Soma Zaidi...

Dalili za uvimbe kwenye kizazi
Posti hii inahusu zaidi Dalili za uvimbe kwenye kizazi,hizi ni Dalili ambazo ujitokeza kwa akina mama ambao wana uvimbe kwenye kizazi kwa hiyo endapo mama ameona Dalili kama hizi anapaswa kuwahi hospitali mara moja kwa uangalizi zaidi. Soma Zaidi...

Njia za kumsafisha Mama aliyetoa mimba.
Post hii inahusu njia safi za kumsafisha Mama ambaye ametoa mimba au mtoto amefia tumboni. Soma Zaidi...

Magonjwa ya kwenye ovari na Dalili zake.
Post hii inahusu zaidi Magonjwa yanayoshambulia sana ovari na Dalili zake, haya ni magonjwa ambayo yanashambulia sana ovari ni kama ifuatavyo. Soma Zaidi...