Post hii inahusu zaidi vyanzo vya kuwepo kwa kiungulia, kiungulia ni kitendo cha kupanda kwa gesi kutoka kwenye tumbo mpaka kwenye mdomo,hali uwasumbua wengi na kusababisha hali isiyo rafiki.
1. Kudhoofika kwa utendaji kazi wa kizuizi cha juu cha tumbo kwa kitaalamu huitwa (lower esophagus sphincter) sehemu hii uhakikishe kuwa kila kitu ambacho kinaenda mwilini hakirudi ila sehemu hii ikiharibika usababisha kurudi kwa vyakula na vitu vingine kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye mdomo.
2. Mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula.
Kuna wakati mwingine kunakuwepo na mfumo dhaifu wa mmeng'enyo wa chakula .
Kwa sababu ya kuwepo kwa vyakula mbalimbali ambavyo uleta shida kwenye mmeng'enyo wa chakula kama vyakula vya mafuta, sukari, vyakula vya caffeine, chocolate na vyakula vya aina hiyo Usababisha mmeng'enyo wa chakula kutoenda sawa na hatimaye kusababisha kiungulia.
3. Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha tindikali kwenye mmeng'enyo wa chakula,
Kwa kawaida tindikali ni lazima kwenye mmeng'enyo wa chakula ila ikizidi inaleta kiungulia aina hii ya tindikali ambayo ukaa tumboni kwa kitaalamu huitwa hydrocholic asidi, ikiwa nyingi upanda mpaka kwenye mdomo na kusababisha kiungulia.
4. Kuwepo kwa baadhi ya madini kwenye mwili .
Kwa sababu kwenye mwili wa binadamu kuna madini mbalimbali na kila aina ya madini ufanya kazi tofautitofauti na yakikosa usababisha matatizo mengi mwilini . Kwa mfano ukosefu wa madini ya magnesium na potassium, yakikosa usababisha kuongezeka kwa kiungulia.
5. Kuwepo kwa uzito mkubwa na kitambi.
Kwa kawaida uzito mkubwa ni chanzo cha magonjwa mengi kwa sababu kuna watu wanene na hawafanyi mazoezi usababisha na wanaopenda kula sana usababisha chakula kupanda juu na kusababisha kiungulia.
6. Wamama wajawazito na wenye umri mkubwa.
Kuna wakati mwingine wamama wajawazito wanakuwa na kiungulia kwa sababu ya hali zao na wengine wenye umri mkubwa kwa sababu ya kushuka kwa immunity upate kiungulia.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri ambao kwa kitaalamu huitwa herpes zoster. Kwa hiyo ili kugundua kubwa mtu ana Ugonjwa huu Dalili kama hizi zifuatazo zinaweza kutokea kwa mgonjwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za Homa ya uti wa mgongo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye maambukizi kwenye uti wa mgongo.
Soma Zaidi...Ukimwi ni upungufu wa kinga mwilini.unasababishwa na virusi ambavyo hutokea kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali
Soma Zaidi...Karibia fangasi wote hawa wanatibika bila ya ugumu wowote maka mgonjwa atakamilisha dozi.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunz akuhusu ugonjwa wa Bawasiri na dalili zake. Pia utajifunza njia za kujilinda nao.
Soma Zaidi...Minyoo ni katika parasite, yaani ni viumbe wanaokaa kwenye mwili na kujipatia chakula chake humo. Katika miili yetu minyoo huishi na kula kuzaliana na kukuwa. Kama unahitaji kujuwa wapi hasa wanakaa mwilini mwetu, endelea na makala hii
Soma Zaidi...Tambuwa kiungulia, sababu zake, dawa za kiungulia na namna ya kupambana na kiungulia
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia kuaribika kwa figo, hizi ni njia zinazotumika ili kuweza kupunguza tatizo la kuaribika kwa figo na hasa wale ambao hawajapata tatizo hili wazitumie ili tuone kama tutaweza kupunguza tatizo hili.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake
Soma Zaidi...