Chanzo cha tatizo la mvurugiko wa hedhi.

Posti hii inahusu zaidi chanzo cha mvurugiko wa hedhi, Kuna kipindi hedhi uvurugika kabisa, pengine unaweza kupata hedhi mara mbili kwa mwezi au kukosa au pengine siku kuwa zaidi ya tano mpaka Saba au kuwa chache, hali hii utokea kwa sababu mbalimbali tut

Chanzo cha mvurugiko wa hedhi.

1.  Mtu kupata hofu, furaha au woga na mabadiliko ya kisaikolojia.

Kuna kipindi utokea mtu anaweza kupata furaha ya ghafla akafanya hata na mwili mzima kubadilika au akapata huzuni ya ghafla akasabisha hata mwili nao kubadilika kwa kufanya hivyo usababisha na hedhi kuvurugika au kwa wakati mwingine mtu anakuwa ametendewa ukatili wa hali ya juu na kuhisi hali isiyo ya kawaida na hiyo ufanya hedhi kubadilika.

 

2. Uwepo wa uvimbe kwenye kizazi.

Kuna wakati mwingine kunakuwepo na uvimbe kwenye kizazi na uvimbe huo unaweza husioneshe Dalili yoyote ile na mtu akawa anaendelea na maisha lakini dalili ya hedhi kuvurugika ni vizuri kabisa kupata vipimo Ili kuweza kuangalia kama ni uvimbe kwenye kizazi.

 

3. Matatizo katika mfumo wa homoni.

Kuna wakati mwingine na homoni ufanya mabadiliko au mvurugiko wa hedhi kwa sababu Kuna wakati mwingine hakuna hedhi kabisa Ina maana yai halikutoka kwenye ovaries, na Kuna wakati mwingine unapata hedhi mara mbili kwa mwezi Ina maana mayai mawili yaliyotokea, kwa hiyo na mabadiliko ya homoni ni tatizo kubwa.

 

4. Kuharibika kwa mimba zisizojulikana,

Kuna wakati mwingine mimba inaweza kutungwa ndani ya mwezi mmoja ikatoka kwa hiyo unaweza kupata damu ambazo hazina moangilio maalumu, 

 

5. Kwa hiyo baada ya kuona sababu za kufanya mabadiliko kwenye hedhi ni vizuri kabisa kumtambua kwamba kama Kuna tatizo lolote ambalo linaweza kutokea ni vizuri kupata vipimo na kugundua ni shida gani iliyofanya nipoteze damu mara mbili kwa mwezi,au damu isitokea au kuendelea kuwepo kwa tatizo la kutoka mimba mara Kwa mara , baada ya kufanya hayo yatakusaidia kuweza kuendelea na afya nzuri kabisa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/09/Saturday - 06:40:44 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2030

👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-