image

Cheetah

Posti hii inakwenda kukupa sifa za mnyama cheetah

.Cheetah

 

picHuyu ni katika wanyama jamii ya paka, na anafanana zaidi na mnyama anayeitwa puma. Cheetah ni mnyama mwindaji kama walivyo chui, simba na mbwa mwitu. Ijapokuwa cheetah wanafanana kwa sura na maumbile lakini unaweza kutofautisha mmoja kwa mwingine kwa kutofautisha rangi za kwenye mikia yao. Cheetah ni katika wanyama walio hatarini kwa kuuliwa kwani wapo wachache sana. Wataalamu wa wanyama na watafifi wanaeleza kuwa nchi ya Namibia ndio nchi pekee yenye cheetah wengi zaidi. Inakadiriwa cheetah wanaoishi maeneo haya wanafika 2500. Cheetah anaweza kufika uzito wa kilogramu 39 mpaka 65 (kg 29 - 65).

 

picTafiti zinaonesha kuwa cheetah ndiye mnyama anayekimbia kwa kasi zaidi kuliko wanyama wote wa porini. Cheetah anaweza kukimbia kwa mwendokasi wa kilomita 97 kwa lisaa (97 km/h) na anaweza kuendelea kukimbia kwa mwendokasi huu kwa umbali wa mita 300. Mwili wa cheetah hauna uwezo wa kutoa jasho hivyo anapokimbia kwa umbali huu wa mita 300 bila ya kukpata kiwindwa chake cheetah huachana nae kwa kuhofia mwili wake kupata joto ambalo linaweza kumpelekea kufa.

 

picWanyama hawa wanakaa kwenye makundi ya familia na mara nyingi madume wanapenda kupigana. Wanyama hawa wanapoteza asilimia 10 mpaka 13 ya vile walivyoviwinda kwa simba pamoja na fisi. Tafiti zinaonesha kuwa nusu ya mawindo yao wanafanikiwa kupata chakula. Cheetah ni katika wanyama waliop hatarini sana kwani wana windwa sana na binadamu kwa ajili ya kuuliwa. Mnyama huyu anapenda kuwinda kwenye maeneo yaliyo wazi pasiwe na miti mingia mabayo itamfanya akikose kiwindwa chake kwa urahisi.

 

Cheetah ni katika wanyama ambao wanaweza kuishi muda mrefu bila ya kunywa maji. Kwani anajipatia maji anayohitaji kutoka kwenye mwili wa kiwindwa chake. Pindi anapowinda humnyatio mnyama wake mpaka ukaribu wa mita 10 ndipo humkurupukia na kumkumbiza kwa mwendokasi wa zaidi sana, na hukata tamaa pindi akimkimbiza kwa umbali wa mita 300. 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1064


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

MAAJABU YA MBU
7. Soma Zaidi...

Historia fupi ya kuingia kwa wakoloni Tanzania
Hapa utakwenda kujifunza namna ambavyo ukoloni uliingia Tanzania na vipindi vyake. Utajifunza hatuwa ambazo ukoloni uliweza kupiti na hatimay kuitawala Tanzania Soma Zaidi...

Tembo ni katika wanyama wenye kushangaza sana.
Tembo wana maajabu makubwa kama utazingatia kwa umakini umbo lake zuri. Soma Zaidi...

Books
Vinjari ukiwa na vitabu vyetu ukiwa kwenye maktaba yetu Soma Zaidi...

TUNAKUTAKIENI RANADHANI MUBARAKA
Wikibongo inawatakia waislamu wote heri ya mfungo wa ramadhaji Soma Zaidi...

Mbu (mosquito)
Posti hii inakwenda kukupa sifa za mdudu mbu Soma Zaidi...

makataba
Soma Zaidi...

maktaba
Soma Zaidi...

mchango
Soma Zaidi...

Ndege kwenye ulimbo
Wahenga wanaelewa, enzi hizo unaambiwa ndege akinasa basi unakumbuka macho juu asije akayoke. Hukuchinib. hujali kama kuna mjimba ama nini Soma Zaidi...

Vitabu
VITABU: Karibu kwenye Maktaba yetu ya vitabu, hapa utaweza kusoma na kudownload vitabu vyetu bure. Soma Zaidi...

CONTACT US
Soma Zaidi...