Dalili kuu za minyoo
Minyoo ni katika viume wanyonyaji, wanaoishi katika miili ya viumbe hai na kujipatia chakula humo. Minyoo wanaweza kuishi kwenye maeneo yenye majimaji kama kwenye maji, ndani ya viumembe hai kama mtu, ngombe, ngure na paka. Minyoo pia wanaweza kuishi kwen
DALILI ZA MINYOO
Aina za minyoo:
Kuna aina za minyoo ziatazo 300000 na kati ya hozo 300 tu ndio ambazo husababisha maradhi kwa binadamu. Minyoo imegawanyika katika aina kadhaa kulingana na tabia zao, jinsi wanavyozaliana na maeneo wanayoishi, pia na maumbile yako. Aina hizo za minyoo ni kama:-
- Trichinosis hawa tunaweza kuwapata kutoka kwa wanyama
- Pinworm (thread worm) hawa ni wadogo sana na unaweza kuwapata kwa kuyala mayai yao kutoka pale yalipo. Kama utakuwa unanawa mikono mara kwa mara, kabla ya kula na huna tabia ya kula vidole ni ngumu kuwapata hawa minyoo
- Hookworm (roundworm) minyoo hawa husambazwa kupitia udongo na kinyesi
- Fluke; (flatworm) hawa wanaishi kwenye utumbo mdogo na meneo mengine. Tunaweza kuwapata kwenye vyakula na mboga zisizooshwa vyema.
- Tapeworm (flatworm) unaweza kuwapata hawa kwenye maji machafu na kwenye vyakula.
Je ni wapi naweza kupata minyoo?
Minyoo tunaweza kuipata maeneo mengi. Na katika miili yetu pia inaweza kuingia kupitia njia nyingi. Njia kuu ni kwa kupitia mdomoni kwa njia ya chakula, ama kinywaji. Lakini pia inaweza kupitia kwenye ngozi. Hebu tuyaone maeneo ambayo monyoo ipo sana.
- Kwenye majimaji
- Ndani ya maji
- Kwenye udongo
- Kwenye nyama
- Kwenye chakula kisichopikwa kama matunda
- Kwenye mbog za majani
Ni kivipi naweza pata minyoo?
- kwa kugusa kitu chenye mayai ya minyoo, kisha ukapeleka mkono mdomoni bila ya kuosha
- Kunywa maji yenye mayai ya minyoo
- Kula chakula chenye mayai ya minyoo
- Kula udongo wenye mayai ya minyoo
- Unapotembea bila ya viatu maeneo machafu
- Unapokula vyakula visivyopikwa ama vilivyopikwa kwa uchache kama nyama ya ngurue
Ni ziipi dalili za minyoo?
- Maumivu ya tumbo
- Kuharisha, kutapika na kupata kichefuchefu
- Tumbo kujaa gesi ama kuunguruma
- Uchofu wa mara kwa mara
- Kupunguwa uzito bila ya sababu maalimu
- Tumbo kujaa na kuwa gumu
Ni vipi naweza kuepuka kupata minyoo?
- Osha mikono kabla ya kula ama kuingiza mdomoni
- Kula chakula kilichopikwa vyema
- Usile matunda bila ya kuosha
- Unapotembea kwenye ardhi chafu usitembee bila ya viatu
- Kama unaishi na paka ama mbwa hakikisha yupo salama
- Vinyesi vya wanyama kama paka, mbwa, na wanyama wafugwo wa nyama vihifadhiwe vyema.
- Kuwa makini na nyama ya nguruwe.
JE minyoo inatibika?
Ndio mimnyoo inatibika tena kwa muda mchache tu. Kama unasumbuliwa fika kituo cha afya kwa vipimo zaidi. Makala inayofata tutazungumzia kuhusu matibabu ya minyoo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Simulizi za Hadithi Audio π2 Bongolite - Game zone - Play free game π3 Kitabu cha Afya π4 Kitau cha Fiqh π5 ai web app π6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Sababu za Kichwa Kuuma Mara kwa Mara
βKichwa kuuma mara kwa mara ni changamoto inayomfanya mtu kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kila siku kwa ufanisi. Makala hii inaangazia sababu mbalimbali za maumivu ya kichwa ya mara kwa mara, jinsi ya kuyatofautisha, na wakati mwafaka wa kutafuta msaada wa kitaalamu
Soma Zaidi...Kukosa usingizi (Insomnia): Sababu na njia za kutatua.
Kukosa usingizi, au insomnia, ni tatizo linalomfanya mtu ashindwe kupata usingizi wa kutosha au usingizi wenye ubora, licha ya kuwa na fursa ya kupumzika. Hali hii haileti uchovu tu, bali pia huathiri umakini kazini, hali ya hisia, na afya ya jumla ya mwili. Makala haya yanachunguza visababishi vikuu vya ukosefu wa usingizi na kutoa mbinu za kisayansi unazoweza kutumia ili kurejesha utaratibu wako wa kulala
Soma Zaidi...Maradhi ya Pumu yanatokeaje?
Nini hasa kinatokea mpaka mtu anakuwa na pumu, ama anashambuliwa na pumu. Makala hii itakwenda kukufundisha jambo hili
Soma Zaidi...Vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer): Chanzo na vyakula vya kuepuka.
Vidonda vya tumbo ni vidonda wazi vinavyojitokeza kwenye utando wa ndani wa tumbo (gastric ulcers) au sehemu ya juu ya utumbo mdogo (duodenal ulcers). Hali hii hutokea wakati kinga ya utando wa tumbo dhidi ya asidi inapovunjika, na kusababisha maumivu makali, kiungulia, na kichefuchefu. Makala haya yanalenga kukupa uelewa wa chanzo cha vidonda hivi na orodha ya vyakula unavyopaswa kuviepuka ili kusaidia uponyaji wa kidonda na kupunguza maumivu.
Soma Zaidi...Jinsi ya kutambua mimba kwa vipimo vya kawaida vya mkojo.
Kujitambua mimba mapema ni hatua muhimu katika kuanza safari ya uzazi salama. Makala haya yanaelezea misingi ya kisayansi ya vipimo vya mkojo vya nyumbani (Pregnancy Test Strips/Sticks), njia sahihi ya kuvitumia, muda mwafaka wa kupima, na jinsi ya kusoma matokeo ili kupata usahihi wa hali ya juu.
Soma Zaidi...Dalili za jeraha la kawaida kwenye ubongo
Posti hii inahusu zaidi dalili la jeraha la kawaida kwenye ubongo, jeraha la kawaida utokea kwa sababu mbalimbali kama vile kupata ajali na kugongwa na kitu chochote kichwani,
Soma Zaidi...