Dalili na ishara za shambulio la moyo
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo.
DALILI
1. Shinikizo, kujaa au maumivu ya kufinya katikati ya kifua ambayo hudumu kwa zaidi ya dakika chache
2. Maumivu yanayoenea zaidi ya kifua chako hadi kwenye bega lako, mkono, mgongo, au hata kwenye meno na taya yako
3. Kuongezeka kwa vipindi vya Maumivu ya Kifua
4. Maumivu ya muda mrefu kwenye tumbo la juu
5 Upungufu wa pumzi
6. Kutokwa na jasho kwa wingi sana
7. Kuzimia na kupoteza fahamu.
8. Kichefuchefu na kutapika.
9.kuhisi mapigo ya moyo yanaenda haraka.
10.maumivu ya kichwa.
11.maumivu ya kifua
Namna ya Kuzuia
1.Kuacha kuvuta sigara
2.Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
3.Kupunguza unywaji wa pombe
4.Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
5.Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)
6.Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.
Mambo ya hatari
1.Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
2.Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo ambayo hatimaye hupelekea kifo
3.Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
4.Kifo cha ghafla.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 web hosting 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
Sababu za kuwa na afya ya akili
Afya ya akili ni hali ya mtu kuwa na akili timamu kiroho,kimwili ,na Kwa mazingira yake yote yaliyomzunguka na anaweza kuamua kitu akiwa katika ukamilifu, zifuatazo ni sababu za kuwa na Afya ya akili.
Soma Zaidi...Dalili za Ugonjwa wa mapafu.
posti hii inahusu dalili za ugonjwa wa mapafu.ambapo kitaalamu hujulikana Kama Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu yako. Majimaji mengi kw
Soma Zaidi...Kazi ya Ini: Jinsi ya kulilinda dhidi ya sumu.
Ini ni kiungo kikubwa zaidi cha ndani mwilini na kinafanya kazi kama "kiwanda cha kusafisha sumu" cha mwili wako. Kazi yake ni muhimu sana kwa uhai, kuanzia kuchuja damu hadi kuyeyusha chakula. Hata hivyo, kutokana na mtindo wa maisha wa kisasa, ini linaweza kulemewa na sumu, jambo linalopelekea maradhi kama ini la mafuta (fatty liver) au uvimbe wa ini (hepatitis). Makala haya yanachambua kazi kuu za ini na mbinu madhubuti za kulilinda dhidi ya uharibifu.
Soma Zaidi...Maumivu, kizunguzungu, kichefuchefu na kutoka na damu ni dalili zamimba?
Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.
Soma Zaidi...Huduma kwa wenye Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia Watu wale ambao wana Maambukizi kwenye tumbo na utumbo mdogo.
Soma Zaidi...