Dalili za gonorrhea
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya dalili za gonorrhea
Dalilii za gonorrhea
Gonorrhea au gonoria ni moja kati ya magonjwa yanayoenezwa kupitia ngono. Huweza kusababishwa na bakteria na kuathiri wanaume na wanawake. Kuweza kuathiri mdomo, koo, mkundu na sehemu za siri kwa wanaume na wanawake. Huweza kuambukizwa kwa kupitia ngono ya mdomo, ngono ya ukeni ama kwenye mkundu. Kwa watoto huweza kuathiri macho. Gonorrhea (gonoria) huambukizwa kutoka kwa mama kuja kwa mtoto wakati wa kujifunguwa.
Dalili za gonoria (gonorrhea) zinaweza kuchelewa kuonekana kwa wanawake kuliko kwa wanaume. Wapo wengine hawaonyeshi dalili yeyote ile hadi hali itakapokuwa ni mbaya zaidi. Kwa mara nyingi dalili za gonoria (gonorrhea) huonekana kuanzia siku 2 mpaka 7 baada ya kuambukizwa. Na kwa wanawake inaweza kuchelewa zaidi hadi mwezi.
Ni zipi dalili za gonoria (gonorrhea)?
Dalili za gonoria (gonorrhea) unaweza kuwa na dalili tofautitofauti kulingana na jinsia. Dalili kwa wanawae na kwa wanaume zinaweza kutofautiana kulingana na maumbile ya jinsia hizi. Muda wa kutokea dalili hizi pia hutofautiana. Pia huweza kuahiri maeneo mengi mwilini.
Dalili za gonorrhea kwa wanaume:-
1.Maumivu wakati wa kukojoa
2.Kutokwa na majimaji kama usaha kwenye uume.
3.Kuvimba pamoja na maumivu ya korodani.
Dalili za gonorrhea kwa wanawake
1.Kutokwa na uchafu sehemu za siri
2.Maumivu makali ya maeneo ya nyonga
3.Maumivu makali wakati wa kukojoa
4.Kutokwa na damu kabla ya hedhi na baada ya hedhi
Dalili za gonoria (gonorrhea) katika maeneo mengine ya mwili:
1.Maumivu ya mkundu, na kutokwa na kama kinyesi pamoja na maumivu ya tumbo na mvurugiko.
2.Maumivu ya macho, kushindwa kuvumilia mwanga mkali, na macho kutoa kama usaha
3.Vidonga vya koo na kuvimba kwa tezi na lumph kwenye shingo
4.Maumivu ya viungio pamoja na kuwa na joto.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Fahamu Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inaonyesha mambo mbalimbali yanayoweza kusababisha Ugonjwa wa kifua kikuu kwa watoto chini ya miaka mitano.
Soma Zaidi...Dalili za Ugonjwa wa mapafu.
posti hii inahusu dalili za ugonjwa wa mapafu.ambapo kitaalamu hujulikana Kama Ugonjwa wa Acute Respiratory Distress Syndrome (ARDS) hutokea wakati Majimaji yanapojaa kwenye vifuko vidogo vya hewa nyororo (alveoli) kwenye mapafu yako. Majimaji mengi kw
Soma Zaidi...Mambo ambayo yanaweza kuongeza hatari ya Ugonjwa wa Homa ya ini yenye sumu.
Posti hii inazungumzia zaidi kuhusiana na Homa ya ini yenye sumu ni kuvimba kwa ini lako kutokana na kuguswa na vitu fulani ambavyo umeathiriwa navyo. Homa ya ini yenye sumu inaweza kusababishwa na pombe, kemikali, madawa ya kulevya au virutubisho vya lis
Soma Zaidi...ugonjwa wa Malaria dalili zake na chanzo chake.
Malaria ni moja ya magonjwa hatari yanayoongoza katika vifo vya watoto wengi duniani walio chni ya umri wa miaka 5. Katika post hii utakwend akujifunza kuhusuugonjwa huu jinsi unavyotokea, hatuwa zake na dalili zake.
Soma Zaidi...​Kupima HIV Nyumbani
Posthii inatoa mwongozo kamili kuhusu upimaji wa HIV nyumbani. Tutachunguza umuhimu wake, jinsi ya kutumia vifaa hivyo, faida zake, na hatua za kuchukua baada ya kupata majibu, ili kukuwezesha kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yako kwa usiri na utulivu.
Soma Zaidi...Faida za kufanya mazoezi ya viungo kwa afya ya akili.
Tunapofikiria kuhusu mazoezi ya viungo, mara nyingi akili yetu inaenda moja kwa moja kwenye kupunguza uzito, kujenga misuli, au kuzuia magonjwa ya moyo. Hata hivyo, faida kubwa zaidi ya mazoezi iko kwenye afya ya akili zetu. Makala haya yanachambua jinsi harakati za mwili zinavyoweza kuwa tiba asili ya msongo wa mawazo, wasiwasi, na sonona, na jinsi unavyoweza kuanza leo.
Soma Zaidi...