Dalili za kuaribika kwa mishipa ya retina.

Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kwa mtu ambaye ana tatizo kwenye mishipa ya retina,ni tatizo ambalo uwakumba wafu wengi wenye matatizo ya kisukari.

Dalili za kuaribika kwa mishipa ya retina.

1.Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa ili mtu aje kuona kitu retina inapaswa kupeleka ujumbe kwenye ubongo kupitia kwa mfumo wa kupeleka picha na mtu unaweza kutambua kitu kinachotokea kwa hiyo kuna kipindi mishipa hii uharibika ili tuweze kujua kama mishipa imearibika Dalili zifuatazo zinaweza kutokea.

 

2. Mgonjwa wa tatizo hili anaona vitu kwa rangi zisizoekewa na pengine anashindwa kutambua kubwa ni rangi gani na tatizo hili lisipotibiwa mapema upofu unaweza kutokea kwa hiyo mtu akipata tatizo hili Awahi mapema hospitalini kwa matibabu.

 

3. Na kwa wakati mwingine Mgonjwa anaona giza tu hali hii inaweza kutokea kwa ghafla au kwa mda na taratibu ikitokea mgonjwa anaanza kuona giza ni vizuri kuwahi hospitali ili kuweza kupata matibabu mapema .

 

4. Tatizo likidumu kwa mda mrefu bila kutibiwa Mgonjwa anaweza kuwa kipofu moja kwa moja kwa hiyo wapendwa tunapaswa kujua kuwa jicho likipata shida yoyote hata iwe ndogo ni vizuri kumpeleka mgonjwa hospitalini moja kwa moja ili kupata huduma na kuepuka madhara ya upofu kwa hiyo tatizo likipekekwa hospitalini likiwa dogo kutibiwa ni rahisi na madhara yanakuwa kidogo.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/07/Monday - 08:21:53 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 869


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-