Dalili za kujifungua hatua kwa hatua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za kujifungua hatua kwa hatua
DALILI ZA KUJIFUNGUWA HATUA KWA HATUWA:
Ni ndoto za wanawake wengi siku moja abebe ujauzito, azae mtoto kisha aitwe mama. Haswa hata wanaume hupendelea hivyo. Ila mwanamke anapofikia kujifunguwa hapa ndipo kizaazaa huonekana. Sasa makala hii itakwenda kukueleza dalili za kujifunguwa.
Daliili za kukaribia kujifunguwa kwa siku kadhaa1.Maumivu ya nyonga kuongezeka2.Uchovu kuongezeka3.Kutoa damu yenye utelezi4.Viungo kuachia5.Njia ya kuzalia kutanuka zaidi.6.Maumivu ya tumbo kuongezeka.7.Maumivu ya tumbi na kutungwa.8.Kuharisha9.Maumivu ya mgongo kuongezeka
Dalili za kujifunguwa kwa masaa machache:1.Mikazo ya tumbo inayotokea katika muda maalumu2.Kutokwa na damu yenye utelezi3.Kutokwa na utelezi kwa wingi4.Njia kuachia zaidi5.Mtoto kushuka karibu na njia ya kutokea.
Uchungu wa kujifunguwa:Uchungu wa kujifunguwa hauwezi kuelezeka kwa maandishi machache haya. Hata hivyo kuna machache naweza kukueleza ijapokuwa huwenda usiwe uhalisia. Kujifunguwa kunapitia hatuwa kuu tatu ambazo ni kama ifuatavyo:-
1.Katika hatuwa ya kwanzacevix (mlango wa mimba) hulegea na kufumguka kwa sentimita 10. hata hivyo kulegea kwa cevix kunaweza kuanza siku chache nyma, kidogo kidogo. Majimaji yanayotoka ukeni huongezeka baada ya kupasuka kwa utando uliomzunguka mtoto. Katika hatuwa hii mikazo ya tumbo la kujifunguwa yanaweza kuwa makali sana ndani ya sekunde 30 mpaka 60 kisha yanakata kwa dakika kama 4 ama 5 kisha huanza tena kama hivi.
Katika hatuwa hii maumivu yanaweza kuwa makali sana kiasi cha kuwa kama vile hayakati. Hapa mtoto anaanza kusogea kwenye njia ya kuzalia. Wakati huu atakuwa ana sukumana na njia ya haja kubwa na hapa mwanamke anaweza kujisikia kuenda haja kubwa. Baadhi ya wanawake walio mara ya kwanza kupata ujauzito wanaweza kwenda chooni na hatimaye anazalia chooni. Kumbuka mikazo ya tumbo haupoi hata kwa dawa za kukata maumivu.
2.Hatua hii ya piliHatuwa hii huanzia toka pale mlango wa kuzalia unapofunguka hadi mwisho (sentimita 10) mpaka mtoto atakapozaliwa. Mikazo ya tumbo katika hatuwa hii inazidi na kuwa katika mpangilio maalumu kwa kuachana. Kila mkazo unapokuwa mkubwa hapa mwanamke atajihisi kusukuma mtoto. Hapa mwanamke atahisi moto kwenye uke wake wakati mtoto anashuka ama atahisi kutanuka kwa uke wake hasa pale kichwa cha mtoto kinapoanza kutoka.
Kipindi hiki mama mamzito atakuwa anapewa maelekezo kuhuku kusukuma mtoto ili kuwezehsa kuzaa kwa haraka. Kuna mengi ambayo daktari ama anayezalisha atatakiwa kuyafanya hapa ili kuwezesha kujifunguwa kwa salama. Mtoto ataanza kutokeza kichwa kisha shingo ikifuatiwa na mabega na baadaye mwili kumalizia. Katika hatuwa hii wahudumu wa afya huwa makini zaidi maana ndio hatuwa yenye hatari sana. Hatuwa hii kwa wanawake ambao ndio ujauzito wao wa kwanza inaweza kuchukuwa lisaa limoja mpaka masaa mawili (1 - 2)
3.Hatuwa ya tatuHatuwa hii huanza pale mwanamke atakapojifunguwa. Hatua hii huhu huhusisha kutowa placent, ama kondo la uzazi. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka dakika 30. upotevu wa damu hapa utaendelea kuwepo ijaokuwa si mkubwa. Mikazo ya tumbo la uzazi itasaidia kupunguza upotevu wa damu. Kitukibaya zaidi katika hatuwa hii ni endapo damu itatoka kwa wingi.
Hali hii inaweza kupelekea tatizo lijulikanalo kama postpartum haemorrhage na kupelekea upungufu wa damu na uchovu. Hivyo wakunga na wahudumu wataendelea kuwa makini sana katika hatuwa hii. Katika hatuwa hii ndipo mtoto atatenganishwa na placenter.
NINI UFANYE UKIWA KATIKA UCHUNGU WA KUJIFUNGUA KATIKA1.Kunywa maji ama juisi kwa wingi ama chai2.Unaweza pia kula kitu kitamu cha kufyonza kama utaruhusiwa. Hii ni kwa ajili ya kukuongezea nguvu3.Badilisha mikao kuaa, kulala, ubavuubavu, chalichali, kusimama na kukaa na kadhalika)4.Kama utaweza kuoga maji ya moto fanya hivyo kabla ya kuingia leba5.Mwambie msimamizi wako kama ataruhusiwa kuingia akufanyie maseji mgongoni ana akusuguesugue6.Jitahidi kurilax kati ya mikazo ya tumbo usisukume mtoto mpaka uambiwe kufanya hivyo7.Unaweza kuomba dawa za maumivu kama utaruhusiwa.8.Usione aibu hata kidogo ukiwa katika leba. Hao unaowaonea aibu wameshaona kila kitu kwako na kwa watu wengine. Kama unataka kulia lia sana, tambuwa kuwa kila kitakachokutokea hapo ni siri na katu hakuna atakayehadithia, hata hivyo kila kitu ni kawaida sana katika leba.9.Fuata maelekezo kama utakavyoambiwa na wahudumu wako. Kosa lolote utakalofanya kumbuka linaweza kuhatarisha maisha yako na ya mtoto wako.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 ai web app 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Dalili za Mimba ya Siku 7 kwa Mwanamke
Kipindi cha siku saba baada ya kurutubishwa kwa yai (karibu wiki moja tangu kutunga kwa mimba) ni hatua ya mwanzo kabisa ambapo kijusi kinaanza kujipandikiza kwenye mji wa mimba. Ingawa mara nyingi ni mapema mno kwa vipimo vya mkojo kuonyesha matokeo chanya, mwili wa mwanamke unaweza kuanza kuonyesha dalili fiche za kibaolojia. Makala hii inaelezea kile kinachotokea mwilini mwako katika kipindi hiki cha siku saba.
Soma Zaidi...Je chuchu zikiwa nyeusi Nini kinasababisha,, kando ya kuwa mjamzito? Na Kama sio mjamzito sababu ya chuchu kua nyeusi ni nini
Chuchu kubadilika range ni mojavkatika mabadiliko ambayo huwapa shoka wengi katika wasichana. Lucinda nikwambie tu kuwa katika hali ya kawaida hilo sio tatizo kiafya.
Soma Zaidi...Maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maumivu wakati wa tendo la ndoa na baada
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa kondo la nyuma
Kondo la nyuma ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamziti,kondo la nyuma husaidia katika kazi mbalimbali katika ukuaji wa mtoto.
Soma Zaidi...dalili za mimba baada ya tendo la ndoa na changa ndani ya wiki moja
Utajifunza dalili za mwanzoni za mimba changa kuanzia wiki moja baada ya tendo la ndoa
Soma Zaidi...Umuhimu wa uzazi wa mpango kwa Mama
Posti hii inahusu zaidi faida za uzazi wa mpango kwa akina Mama, tunajua wazi kubwa kuna faida kubwa za uzazi wa mpango kwa akina Mama pindi watumiapo njia hizi kwa uhakika zaidi.
Soma Zaidi...