Dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.

Posti hii inahusu zaidi dalili za kupasuka kwa mfuko wa uzazi,ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama ambaye anakuwa amepasuka mfuko wa kizazi.

Dalili za mama aliyepasuka mfuko wa uzazi.

1. Kwanza kabisa Mama anayepasuka mfuko wa uzazi mara nyingi anakuwa kwenye uchungu, ila mfuko wa uzazi unapopasuka tu na uchungu unapungua kabisa badala ya kuendelea hiyo inakuwa ni mojawapo ya Dalili ya kupasuka kwa mfuko wa uzazi.

 

2. Pia Mama anakuwa na maumivu ya kupita kiasi , hasa hasa ukigusa kwenye tumbo la Mama ,yeye anakuwa na maumivu na analalamika sana kuhusu tumbo kwa hiyo hii ni Dalili mojawapo ya Mama mwenye tatizo la kupasuka kwa mfuko wa uzazi.

 

3. Pia na msukumo wa damu unapungua na kuipima unakuta uko chini kabisa na pia mapigo ya mtoto yanayopungua au kwa upande mwingine kama mtoto amashafariki yanakuwa hayapo kabisa.

 

4. Pia kwa upande wa mama na mapigo ya moyo yanapungua yaani sauti inasikikia kwa shida sana , kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi ni vizuri kabisa mama kama yuko kwenye vituo vya afya apelekwe kwenye hospitali kubwa kwa uangalizi zaidi.

 

5. Pia na Mama anaay kutokwa na damu kwenye sehemu za siri kwa kawaida damu hiyo utegemea inaweza kuwa nyingi au ya kawaida.

 

6. Pia  na  mtoto ukishika kwenye tumbo ni rahisi kuhisi kwa mikono na unapokuwa unapapasa tumbo la Mama Maumivu yanakuwa ni makali mno na mama anakuwa analalamika sana.

 

7. Kwa hiyo kwa wauguzi na wataalam wa afya baada ya kuona hayo yote ni vizuri kabisa  kumsaidia Mama ili asije kupoteza maisha kwa sababu hii ni Dalili mojawapo ya hatari kwa Mama wajawazito kwa hiyo ni vizuri kabisa kugundua mapema kabisa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/05/Sunday - 10:48:23 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2371


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-