Dalili za kuwepo mwenyezi Mungu

Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Dalili nyingi zimedhihirishwa ndani ya Qur’an katika maeneo makuu matano ambamo uchunguzi wa kina na kutafakari vikifanyika vilivyo mtu atayakinisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pasina shaka yeyote. Maeneo hayo ni haya yafuatayo; 

  1. Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo.
  2. Nafsi (Dhati) ya mwanaadamu.
  3. Historia ya mwanaadamu.
  4. Maisha ya mitume.
  5. Mafundisho ya mitume.

 

  1. Umbile la Mbingu na Ardhi na Vyote Vilivyomo.

Maumbile mbali mbali kama vile udongo, milima, mabonde, maji, mimea, wanyama, jua, mwezi, nyota, n.k ambavyo ni ishara kubwa inayoonyesha uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w). Ishara hizo ni hizi zifuatazo; 

(a) Umbile la Mbingu na Ardhi;

Tukichunguza maumbile mbali mbali ya dunia na sayari zote jinsi yalivyoundwa na kupangika kwa namna iliyo maalum kama vile jua, mwezi, nyota, n.k ni ishara tosha kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (41:9-12), (7:54), (32:4-5), (70:4), (21:30), (46:33) na (79:30).

 

          (b) Jua, Mwezi na Nyota;

Kuwepo kwa mfumo wa ajabu uliopangika wa Jua, mwezi na Nyota na kila kimoja kina njia yake pasina kutokea mgongano au mvurugano wa aina yeyote kati yao ni ishara kubwa za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (6:96), (7:54), (2:29), (10:5), (14:33), n.k.

 

          (c) Usiku, Mchana, Mwanga na Giza;

Kupatikana na kubadilishana kwa usiku na mchana, mwanga na giza ni ishara tosha za kuthibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wenye akili.

    Rejea Qur’an (2:164), (3:190), (17:12) na (28:71-72).

 

(d) Bahari, Maziwa na Mito;

Wingi wa maji yasiyo na mfano, kutofautiana ladha yake, na kutengana kati ya maji matamu na chumvi bila ya kizuizi chochote na pia vyombo vizito na vikubwa kupita juu yake bila kuzama ni dalili nyingine ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w). 

Rejea Qur’an (25:53), (2:264), (10:22), (14:32), (16:14), (17:66), (22:65) na (53:12).

 

(e)  Milima na Mabonde;

Milima, majabali na mabonde ambavyo vinaifanya ardhi iwe madhubuti na isiyumbe  wakati wa mitetemeko na mzunguko kati ya jua, mwezi na nyota ni ishara kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (21:31), (13:3), (15:9), (16:15), (27:61), (31:10), (50:7), (77:27), (35:27), (78:7) na (88:19).

 

  1. Upepo, Mawingu, Mvua, Radi na Ngurumo;

Upepo, mawingu, radi, ngurumo na mvua ni vitu vinavyofanya kazi kwa ushirikiano wa ajabu unaopelekea mvua kunyesha sehemu inayohitajika. Vyote hivi ni dalili tosha juu ya kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w).

Rejea Qur’an (10:22), (13:17), (2:19-20), (2:164) na (25:48). 

 

  1. Matunda, Mimea na Vyakula (Riziki);

Mimea na matunda mbali mbali hustawi katika aina tofauti za udongo na kutoa mazao ambayo ni riziki (chakula) kwa viumbe hai na kila kimoja kinategemea kingine katika kustawi kwake. Hii ni ishara kwa wenye akili.

Rejea Qur’an (67:21), (11:6), (29:60), (6:95,99) na (13:4).

 

  1. Wanyama, Ndege na Wadudu;

Viumbe vyote hivi kutokana na kutembea, kuruka kwao na kupata kwao riziki bila ya wao kujipikia na kumiliki rasilimali yeyote, bado wanaishi bila shida yeyote. Hii ni kuonyesha kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye pekee anayewaruzuku.

Rejea Qur’an (16:5-7), (16:79) na (3:190-191).



 

  1. Nafsi (Dhati) ya Mwanaadamu.

Kutokana na nafsi ya mwanaadamu mwenyewe tukichunguza na kutafakari kwa makini kuna ishara nyingi zinazoonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) kama ifuatavyo;

 

(a)  Asili, Chanzo na mwisho wa uhai wa mwanaadamu;

Uhai, hatua alizopitia na mfumo wa maisha ya mwanaadamu, vipi na lini alianza atamaliza kuishi, nini sababu ya kifo chake na kitatokea wapi na nani anayedhibiti maisha yake yote ya kila siku, tunadhibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu (s.w). 

Rejea Qur’an (2:28), (30:20-21), (22:5), (75:36-40), (23:14) na (56:81-87).

 

          (b)  Mwanaadamu kutofautiana na Wanyama;

Wanaadamu kutofautiana na wanyama kimaumbile na kimalengo, ambapo lengo la mwanaadamu ni kuwa Khalifah, na wanyama ni kumtumikia mwanaadamu. Mwanaadamu amepewa akili, uhuru, vipawa na utambuzi kinyume na wanyama. 

Rejea Qur’an (2:29-30), (15:28-29), (95:4) na (16:78).

 

(c)  Kuumbwa wanaume na wanawake na kuwa na mapenzi baina yao;

Asili ya wanaadamu wote ni moja, lakini wanatofautiana kimaumbile, kihisia na kisaikolojia. Hii ni kwa ajili ya kutegemeana, kuhurumiana na kuvumiliana kimahitaji kati yao kimwili na kisaikolojia. Zote hizi ni ishara tosha za kuwepo Allah (s.w).

 

(d)  Mwanaadamu kutofautiana lugha, rangi, kabila na taifa;

Pamoja na wanaadamu kufanana katika viungo mbali mbali vya miili yao kama ulimi, mdomo, koromeo, n.k lakini wanazungumza lugha tofauti bila ya kufunzwa na mtu yeyote. Hii ni kuwa utofauti wao ni kwa ajili ya kujuana tu, na hii ni dalili tosha.

     Rejea Qur’an (30:22) na(49:13).

 

(e)  Kutofautiana vipaji na riziki na mgawanyo wake miongoni mwa wanaadamu;  

Vipaji vya wanadamu vimetofautiana mmoja na mwingine kama vile udaktari, uhandisi, ualimu, n.k. pia upatikanaji wa riziki miongoni mwao ambao hautegemei ujanja, fani au ujuzi wa mtu bali mgao maalum ili waweze kutegemeana. 

        Rejea Qur’an (80:24-32).




 

(f)  Ufanyaji kazi wa viungo vya mwili wa mwanaadamu;

Myeyusho wa chakula, mfumo wa damu na ufanyaji kazi wa figo, mapafu, n.k ni mashine za ajabu zisizohitaji utengenezaji na usimamizi wowote wa kibinaadamu. Hii ni ishara kubwa juu ya uwepo Mtengenezaji Mjuzi na Mwenye Hekima.

    Rejea Qur’an (30:30).

 

                 (g)  Usingizi, Umbo, sura na vazi la mwanaadamu;

Umbo au sura aliyonayo mwanadamu hana uwezo wa kuibadilisha na anaridhika nayo. Tofauti na wanyama wanaadamu wana mavazi ya kujisitiri uchi na kujikinga na baridi na pia kupata usingizi pasina yeye kutaka au kujua chanzo na mwisho wake.

Rejea Qur’an (7:26), (82:6-8), (95:4) na (45:4).

 

      (h)  Mwanaadamu kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) wakati wa matatizo; 

Wakati wa matatizo mwanaadamu ni mwepesi sana kurejea na kumkumbuka Mwenyezi Mungu (s.w) na kuhitajia msaada wake, hata wale wanaokana kuwepo kwake wanakiri uwepo wake bila ujanja. Hizi zote ni ishara za kuwepo kwake.

    Rejea Qur’an (6:63) na (10:90).


 

  1. Historia ya Maisha ya Mwanaadamu.

 

Mchakato wa maisha na historia ya mwanaadamu tangu zama za kale hadi zama hizi umeambatana na matukio makubwa yaliyovunja na kusambaratisha falme na dola mbali mbali zilizotikisha dunia vita na majeshi. Yafuatayo ni baadhi tu ya matukio hayo;

 

(a)  Kuangamizwa watu wa (kaumu ya) Lut, Thamud, Ad na Firauni;

Pamoja na nguvu kubwa za kijeshi na ulinzi imara waliokuwa nao watu hawa, haikuwa chochote ilipofika muda wa kuangamizwa kwao. Mwenyezi Mungu mwenye nguvu zisizokifani aliwafutilia mbali kwa kutumia majeshi yake ya upepo, maji, n.k.

        Rejea Qur’an (89:6-13), (30:9), (20:128) na (22:45-46).


 

    (b)  Kuangamizwa kwa  jeshi la Abraha, Gavana wa Yemen;

Abraha aliandaa jeshi kubwa la askari na tembo waliofunzwa barabara kwa ajili ya kwenda kuibomoa Al-Ka’abah (Nyumba Tukufu ya Makka), lakini alisambaratishwa na jeshi dogo na dhaifu kabisa la ndege, na hatimaye ikawa ndio mwisho wao. 

    Rejea Qur’an (105:1-5).

 

(c)  Kufutika na kutoweka Viongozi na Wafalme maarufu Duniani;

Viongozi na wafalme wengi waliowahi kuitawala na kuitikisa dunia na kusababisa uharibifu, mauaji, kutokana nguvu kubwa ya kijeshi waliokuwa nayo na hata wengine kufanywa miungu. Mfano akina Hitler, Mussolini na wengineo ambao mwisho wao walifutika duniani na kushindwa kujinusuru pamoja na majeshi yao.

    Rejea Qur’an (56:81-87) na (67:20).


 

  1. Maisha ya Mitume;

 

Kwa kuzingatia maisha ya mitume hasa waliobainisha nadni ya Qur’an, jinsi walivyofikisha ujumbe kwa watu wao kinadharia na kimatendo ni ishara tosha juu ya uwepo wa Allah (s.w). Baadhi ya mambo hayo ni haya yafuatayo;

 

(a)   Kuwepo na kujieleza kwao kwa watu wao kuwa wao ni mitume wa Allah (s.w);

Mitume wote walithibitisha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w), na vile vile wote walitoa dai lilelile la kuwa wao ni mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w) ijapokuwa walikuja nyakati na sehemu tofauti.

Rejea Qur’an (7:59-61), (7:65-67), (16:36), (40:78) na (35:24).

 

      (b)  Mwenendo wao mwema kutoathiriwa na mazingira ya jamii;

Mitume wengi walizaliwa na kulelewa katika jamii za kijahili, kishirikina na kuabudu masanamu, lakini na walikuwa na mienendo na tabia nzuri isiyo kuwa na mfano katika jamii husika. Hii ni ishara kuwa yupo Mlezi na Mjuzi, naye ni Allah (s.w).

Rejea Qur’an (57:25).

 

(c)  Miujiza kuthibitisha utume wao;

Mitume walikuja na miujiza tofauti tofauti ya kuthibitisha utume wao kwa watu wao. Kila mtume alikuja na miujiza kutoka kwa Allah (s.w) kama ishara ya kufikisha ujumbe kwa watu wake iliyokuwa tofauti na uchawi, viini macho na mazingaumbwe.

Rejea Qur’an (57:25), (28:29-32), (5:110), (15:9) na (4:82).

 

(d)  Kuhimili na kujitoa kwao muhanga;

Mitume walikuwa wavumilivu na wenye subira dhidi ya mateso, kupigwa, kufungwa gerezani, kutiwa kizuizini au kuuawa na kupata madhila, lakini hawa kukata tama na kufikisha ujumbe wao. Hii ni yupo alikuwa anawaliwaza, naye ni Allah (s.w).

Rejea Qur’an (3:21), (3:181), (4:157-158), (21:69) na (59:8).

 

          (e)  Ujasiri wa mitume mbele ya viongozi na jamii za kishirikina;

Pamoja na vitisho na viburi vya wafalme na watawala wa kishirikina, mitume hawakumchelea mtu yeyote katika kumfikishia ujumbe wao. Hii ni ishara kuwa Mwenyezi Mungu ndiye waliokuwa wanamtegemea. 

Rejea Qur’an (19:42-46) na (21:57-67).

 

     (f)  Ushindi wa mitume dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w);

Mitume na wafuasi wao walikuwa wachache, dhaifu na wanyonge mbele ya maadui wa Allah (s.w) waliokuwa wengi na wenye nguvu, lakini katika mapambano mitume na wafuasi wao ndio waliopata ushindi kwa msaada kutoka kwa Allah (s.w).

Rejea Qur’an (71:25), (7:72), (26:60-68) na (8:9-10).

 

        (g)  Mitume kutohitaji malipo kutoka kwa watu wao;

Mitume walifanya kazi ngumu na nzito bila ya kuhitajia malipo yeyote kutoka kwa watu wao kinyume na viongozi wengi ambao huhitajia malipo kwa jamii zao. Mitume walikuwa na uhakika wa kupata ujira tu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w) pekee.

Rejea Qur’an (26:127).



 

  1. Mafundisho ya Mitume.

Hili ni eneo jingine linaloonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu (s.w) katika vipengele vifuatavyo;

 

(a)  Umoja wa ujumbe wa mitume;

Mitume walitumwa sehemu na nyakati tofauti lakini ujumbe wao ulifanana, kila mtume alifundisha Tawhiid, lengo la kuumbwa kwao, kuwahofisha na adhabu na kuwabashiria malipo mema pia. Hii ni kuwa ujumbe wao ulitoka kwa Allah (s.w).

            Rejea Qur’an (7:59, 65, 73, 85, 158), (16:36) na (19:36).

 

      (b)  Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira;

Mitume karibu wote walitokea katika jamii za kishirikina na kijahili, lakini kamwe hawakuwahi kuchanganya mafundisho yao na utamaduni wa kijahili hata kama jamii nzima ilisimama dhidi yao.

Rejea Qur’an (109:1-6).

 

          (c)  Upeo wa Elimu waliokuwa nayo Mitume;

Mitume walikuwa na upeo, fikra na hekima ya hali juu katika kutatua na kuendea mambo kuliko mtu yeyote katika jamii zao, japokuwa hawakupitia vyuo au taasisi zozote za elimu. Hii ni dalili kuwa ni Mwenyezi Mungu (s.w) ndiye aliyewafunza.

Rejea Qur’an (34:10-12), (27:15-19), (43:2-3) na (25:53



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/01/15/Saturday - 07:25:32 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 875


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Kutoa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtume Muhammad s.a. w akutana na Bahira
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 11 Soma Zaidi...

Shahada mbili
Kwenye mada hii tutajifunza shahada mbili,tafsiri ya shahada kstika maisha ya kila siku. Soma Zaidi...

Tofauti kati ya Quran na vitabu vingine vya mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo) Soma Zaidi...

Mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mara moja
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko ya matiti yanayopaswa kutolewa taarifa mapema, kwa sababu ya kuwepo kwa saratani ya matiti, kuna dalili ambazo zikijitokeza zinapaswa kutolewa taarifa mara moja bila kuchelewa kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat Al-Kawthar
Sura hii ni miongoni mwa Sura fupi sanya huwenda ndiosura yenye aya chache kuliko sura zote katika Quran. Soma Zaidi...

Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Mtume Muhammad s.a.w analelewa na Babu yako ikiwa na umri wa miaka 6
Sura na historia ya Mtume Muhammad s.a. w sehemu ya 9. Soma Zaidi...

Nguzo za uislamu:Shahada
Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Misingi ya fiqh
Kwenye kipengele hichi tutajifinza vyanzo mbalimbali vya sheria ua kiislamu. Soma Zaidi...

Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...