Dalili za maambukizi kwenye magoti

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mtu anaweza kupata ikiwa Kuna maambukizi kwenye magoti, kwa sababu mbalimbali ambazo usababisha maumivu au maambukizi kwenye magoti Kuna dalili za mwanzo ambazo zinajitokeza kama tutakavyoona hapo chini

Dalili za maambukizi kwenye magoti.

1.  Kuwepo kwa maumivu wakati wa asubuhi au wakati wa baridi.

Kwa kawaida wakati wa asubuhi na wakati wa baridi kunakuwepo na hali ambayo usababisha mwili kusinyaa kwa hiyo kutokana na kusinyaa kwa mwili hivyo hivyo usababisha misuli ya magoti kusinyaa na kusababisha maumivu pale penye maambukizi hasa mtu akitaka kusimama au kutembea kwa hiyo watu wenye maambukizi upata shida sana.

 

2. Kuwepo kwa maumivu wakati wa kubeba mizigo.

Kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye magoti endapo mtu atabeba mzigo mzito maumivu yote yataishia sehemu Ile iliyoadhirika kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi na hivyo sehemu hiyo inakuwa imeathirka sana.

 

3. Kuwepo kwa maumivu wakati wa kutembea.

Kwa kawaida Mtu anapotembea kutoka hatua Moja kwenda nyingine usababisha na viungo vyote kubadilisha mwelekeo na kuelekea kwa mtu ambapo anaelekea kwa kufanya hivyo usababisha sehemu Ile yenye maambukizi kuumia kwa sababu ya msuguano kutoka sehemu Moja kwenda nyingine.

 

4. Maumivu wakati wa kuchuchumaa 

Kwa kawaida Mtu anapotaka kuchuchumaa ni lazima kuhusisha na magoti kwa hiyo akitaka kuchuchumaa usababisha maumivu makali kwenye magoti na vile vile kushindwa kuchuchumaa na wengine wanatumia choo  za kusimama kwa sababu ya kushindwa kuchuchumaa kwa sababu ya maumivu kwenye sehemu ya maambukizi.

 

5. Maumivu wakati wa kufanya kazi yoyote ile.

Hii nayo ni dalili Mojawapo inayowapata watu wenye maambukizi kwenye magoti akija kufanya kazi ni lazima kuhisi maumivu kwenye sehemu ya maambukizi na pengine watu wengine ushindwa kufanya hata kazi ndogo kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi.

 

6. Pia maumivu wakati wa kunyanyua vitu vizito.

Kuna wakati mwingine mtu akija kunyanyua vitu vizito anahisi maumivu makali kwenye sehemu ya maambukizi.

 

7. Maumivu wakati wa kusimama.

Na pia kama mtu amekaa chini unalalamika sana maumivu akija kuamuka kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye magoti.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/07/Thursday - 04:36:08 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1099


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-