DALILI ZA MIMBA BAADA YA TENDO LA NDOA
Je unahitaji kujuwa kama umepata ujauzito baada ya kufanya tendo la ndoa? hakika sio rahisi ila kama utakuwa makini utaweza.
DALILI ZA UJAUZITO BAADA YA TENDO LA NDOA
Je umeshawahi kujiuliza ni zipi zinaweza kuwa dalili za kwanza za ujauzito baada ya kushiriki tendo la ndoa? Hakika hili ni swali zuri na hapa niyakujuza majibu yake. Ukweli ni kuwa ni vigumu kuona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa kama hutakuwa makini. Yes inawezekana kuzijuwa ila inahitaji uangalizi wa umakini kabisa. Mwanamke mmoja alishaniambia kuwa yeye ndani ya masaa matano baada ya kufanya tendo la ndoa anaweza kujuwa kama amebeba mimba ama laa. Nilipojaribu kumuuliza alikataa kabisa kunieleza.
Je naweza kuziona dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa?
Kabla ya kulijibu swahi hili inapasa kujuwa mabadiliko ya mwili wako kabla ya ujauzito ama kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwanza zingatia mabo haya kabla ya kushiriki tendo la ndoa:-
- Jeoto la mwili wako. Hakikisha unatambuwa vyema kama mwili wako joto lake lipo kiasi gani. Na hakikisha unaweza kutofautisha kati ya joto la homa na joto la kawaida.
- Zingatia majimaji ya kwenye uke wako. Zingatia kama uke wako upo katika majimaji ama upo mkavu. Pia angalia rangi za mashavu ya uke.
- Zingatia tarehe zako. Kabla ya kushiriki tebdo la ndoa hakikisha tarehe zako unazifahamu vyema, pamoja na siku zako za hatari ni lini.
Je nitazijuaje sasa hizo dalili baada ya kuzingatia mambo hayo?
Kujuwa kama umebeba mimba ama laa inaweza kuchukuwa hata wiki moja kuona mabadiliko kwenye mwili wako, mabadiliko haya yataweza kukuambia kwamba huwenda umebebe mimba. Ila pia kuna baadhi ya waanwake wanaweza kuyana mabadiliko hayo mapema kabisa. Ila tambuwa kuwa mabadiliko hayo yote yanaweza kuwa ni vyanzo vya sababu zingine na si ujauzito.
Mabadiliko hayo ni kama:-
- Kuongezeka kwa joto la mwili. Kama ulizingatia vyema joto la mwili wako wakati ukiwa katika siku za hatari linakuwa kubwa kulinganisha ziku za nyuma. Baada ya kushiriki tendo la ndoa angalia je joto litapunguwa ama kuongezeka. Kama litapunguwa baada ya kupita siku za hatari huwenda bado hujabeba ujauzito. Lakini endapo utaona joto halipungui na huwenda likaongezeka hii huonyesha kuwa una mabadiliko kwenye mwili wako ambayo huwenda ni ujauzito. Jifunze pia kutofautisha kati ya homa na joto la kawaida.
- Majimaji kwenye uke na njia ya kuelekea kwenye tumbo la mimba. Kikawaida wakati wa siku za hatari kiasi cha majimaji kwenye uke huongezeka, hii ni kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kuweza kubeba mimba. Zinapopita siku za hatari majimaji hupunguwa na hatimaye kurudi hali ya kawaida ya ukavu. Sasa endapo majimaji hayatapunguwa na vinginevyo yakawa yanabadilika na kuwa mazito kuliko hapo mwanzo hii huashiria huwenda amebeba ujauzito.
- Ok sasa zingatia ziku zako za hatari.kama ulishiriki tendo la ndoa katika siku hatari kisha ukaanza kuona mabadiliko kama kutokwa na damu chache iliyo tofauti na hedhi, ama maumivu ya tumbo ya ghafla, ama kichwa kuhisi chepesi mabadiliko kama haya na mengineyo huashiria ujauzito.
- Mabadiliko ya rangi kwenye chuchu na mashavu ya uke yanaweza kuwa n dalili ya ujauzito. Matiti kuuma ama kuwa magumu hii ni katika dalili wanayoiona wengi katka wanawake. Mashavu ya uke hubadilika kuwa na uweuzi ama uwekundu kutokana na mishipa ya damu kuja juu na kupitisha damu kwa wingi maeneo ya chini ili kuandaa ukuaji wa mimba.
NI ZIPI DALILI ZA MWANZO ZA MIMBA KUANZIA SIKU YA KWANZA?
Yes kama tulivyoona hapo juu, mabadiliko hayo sio rahisi kutokea kutoka siku ya kwanza, ila yes mwili huanza kuonyehsa mabadiliko ya ndani punde tu mimba inapoingia, lakini kwa mwanamke kuhusi mabadiliko hayo inaweza kuchukuwa muda. Sasa hapa tutaziona kwa ufupi orodha ya dalili za mimba changa:
- Kuingezeka kwa joto la mwili
- Kuongezeka kwa maimaji ya ukeni
- Kutoka na damu kidogo nyepesi
- Maumivu ya matiti na kujaa ama kuwa magmu
- Mabadiliko ya rangi kwenye matiti na mashavu ya uke
- Kutoziona siku zako
- Kichwa kuwa chepesi
- Maumivu ya kichwa, tumbo na kizunguzungu
- Kichefuchefu na kutapika
- Kukojoa mara kwa mara
- Maumivu ya tumbo
JE KAMA SIO MIMBA NINI KITAKUWA.
Si kila dalili za mimba zinamaanisha ni kweli una ujauzito. Unaweza kuona dalili za mimba lakini ukawa huna. Sababu zinazoweza kupelekea hali hii ni kama:-
- Mabadiliko ya homoni
- Mashambulizi ya bakteria na virusi kwenye ufumo wa mkojo na mfumo wa uzazi
- Vyakula
- Mazingira
- Maradhi mengineyo yahusuyo mfumo wa uzazi
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Madrasa kiganjani π2 web hosting π3 Dua za Mitume na Manabii π4 Bongolite - Game zone - Play free game π5 kitabu cha Simulizi π6 ai web app
Post zinazofanana:
Je, kuna vyakula vya kuepuka wakati wa ujauzito?
Lishe bora ni msingi wa ukuaji wa mtoto mwenye afya na ustawi wa mama mjamzito. Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kuwa na vimelea hatari, sumu, au kemikali zinazoweza kusababisha madhara makubwa kama vile maambukizi ya bakteria, kuharibika kwa mimba, au matatizo ya ukuaji wa mtoto. Makala hii inaorodhesha vyakula unavyopaswa kuepuka ili kulinda afya yako na ya kiumbe ulichobeba.
Soma Zaidi...Matatizo ya kisaikolojia yanayosababishwa na matumizi ya mtandao.
βGundua athari za kisaikolojia zinazotokana na matumizi ya mtandao, ikiwemo wasiwasi, msongo wa mawazo, na uraibu. Pata maarifa ya kitaalamu ya jinsi ya kulinda afya yako ya akili katika ulimwengu wa kidijitali.
Soma Zaidi...Dalili za mtu mwenye wasiwasi (anxiety)
Post hii unahusu mtu mwenye ugonjwa wa akili ambao huitwa ugonjwa wa wasiwasi Kwa kitaalamu huitwa anxiety,ni pale mtu anapokuwa na wasiwasi Kwa vitu nafasi mbali mbali kama tutakavoona.
Soma Zaidi...Tabia za kujidhuru (Self-harm): Nini cha kufanya?
Tabia ya kujidhuru kimakusudi ni ishara ya wazi ya maumivu makali ya ndani ya kihisia ambayo mtu anashindwa kuyastahimili. Makala haya yanachambua kwa nini hali hii hutokea, jinsi ya kuacha unyanyapaa, na hatua za vitendo unazoweza kuchukua ikiwa wewe mwenyewe au mtu unayemjali anapitia changamoto hii.
Soma Zaidi...Sababu za Kuchoka Sana Mwilini
βUchovu wa mwili (fatigue) ni hisia ya kukosa nguvu, kutaka kulala mara kwa mara, na kuhisi mwili ni mzito, hali ambayo haiishi hata baada ya kupata mapumziko. Ingawa mara nyingi ni matokeo ya mtindo wa maisha, wakati mwingine inaweza kuwa ishara ya tatizo la kiafya linalohitaji uangalizi. Makala hii inaangazia sababu kuu za uchovu huu na hatua za kurejesha nguvu zako.
Soma Zaidi...Ugonjwa wa kichaa cha mbwa: Dalili na hatua za haraka.
Kichaa cha mbwa (Rabies) ni ugonjwa hatari wa virusi (Zoonotic disease) unaoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu kupitia mate. Ugonjwa huu huathiri mfumo mkuu wa neva na, mara tu dalili zinapoanza kuonekana, huwa hauna tiba na husababisha kifo kwa asilimia karibu 100. Makala hii inaelezea utaratibu wa maambukizi, dalili za awali na za hatari, na hatua za dharura za kuokoa maisha pale mtu anapong'atwa na mnyama mwenye maambukizi.
Soma Zaidi...