dalili za mimba changa ndani ya wiki moja

Je na wewe ni katika ambao wanahitaji kujuwa dalili za mimba ndani ya wiki moja? kama ndio makala hii ni kwa ajili yako. Utakwenda kuona dalili za mwanzo sana za ujauzito toka siku za mwanzoni.

Mimba huweza kutungwa baada ya mbegu ya kiume kukutana na yai na kulirutubisha. Mchakato huu kiasili hufanyika katika tumbo la uzazi katika mirija ya falopia ya mama. Siku hizi teknolojia imekuwa, mimba inaweza kutungishwa nje na baadaye yai kurudishwa kwa mama na tayari kukuwa kama mtoto. Watu wengi wamekuwa wakisumbuka na kutafuta ujauzito. Makala hii itakuwa na maada katika nyanja hii ya afya ya uzazi.

 

Dalili za mimba maana yake ni kuona mabadiliko katika mwili wa mwanamke baada ya kushiriki tendo la ndoa. Mabadiliko haya yawe yamesababishwa na kutungishwa kwa yai. Mabadiliko ya homoni katika mwili wa mwanamke huweza kuzungumza mabo mengi kuhusu afya ya mwanamke huyo. Miongoni mwa dalili za mwanzoni za ujauzito ni mabadiliko ya homoni. Mabadilko haya ndiyo baadaye yanasababisha kichefuchefu, kupata harufu, na mengineyo.

 

JE NI ZIPI DALILI ZA UJAUZITO NDANI YA WIKI MOJA?
Mwanamke anaweza kupatwa na mabadiliko ndani ya wiki moja ya ujauzito. Mabadiliko haya anaweza asiyahisi kwani yamekuwa yakifanana na hali za kawaida. Hii husababisha mwanamke ajegunduwa kuwa ana ujauzito hadi pale atakapokosa siku zake. Hapa nitakuletea baadhi ya mabadiliko ambayo huweza kuonekana mwanzoni sana mwa ujauzito ambayo huweza kuashiria dalili za mimba changa ndani ya wiki moja.


1.Kuona damu kidogo yneye rangi hafifu. Damu hii inaweza kuwa ni kitone ama mabadiliko ya rangi kwenye nguo ya ndani. Huwenda pia asigundue damu hii hadi wakati anapojisafisha. Damu hii kitaalamu hufahamika kama implantation bleeding. Kwa baadhi ya wanawake wanaweza kuiona damu hii mwanzoni kabisa katika wiki ya kwanza.

 

2.Maumivu ya tumbo. Maumivu haya yanafanana na tumbo la chango. Yanaweza kuuma kwamuda kama unachomwa kisha yanakata. Yanaweza kufanya hivikwa siku kadhaa kisha yanapotea. Kwa wanwake wengine yanaweza kuchukuwa muda mfupi sana hata kwa siku moja ama mbili hivi, ila wengine hata wiki.

 

3.Kichwa kuwa chepesi na kuwa na maumivu ya hapa na pale. Mwanamke anaweza kuhisi kizunguzungu yaani kichwa kinakuwa chepesi sana. Hali hii huweza kuambatana na maumivu ya kichwa ama joto la mwili kuongezeka.

 

4.Kuhisi uchovu. Uchovu ni hali za kawaida ambapo kila mtu anaweza kuihisi hali hii. Kuna sababu nyingi za kuwa na uchovu.lakni kwa mwanamke mwenye mimba hana sababu maalumu. Yaani ghafla anaweza kuhisi uchovu ambao hauna chanzo.

5.Tumbo kujaa gesi na kujaa nakuwa gumu. Hali hii inaweza kuambatana na kupungua kwa hamu ya kula na kukosa choo. Mwanamke atahisi tumbo kuwa limejaa, akila kidogo ameshiba hii ni kwa sababu ya gesi. Gesi hii hutokea kutokana na mabadiliko ya homoni aliyonayo.

 

Kwa ufupi hizo ni baadhi tu ya dalili za mwanzo sana za ujauzito. Mabadiliko haya pia yanaweza kuwa si ujauzito hivyo kuashiria shida nyingine za kiafya kwa mfano. Kuna baadhi ya maradhi yenyewe yanaweza kuwa na baadhi ya dalili za ujauzito kama:-
1.Mabadiliko ya homoni
2.UTI
3.PID
4.Fangasi
5.Shida kwenye kizazi

 

Je ni siku ipi ya kushiriki tendo la ndoa upate ujauzito?
Ujauzito huweza kupatikana katika siku chache sana zisizozidi 10 katika mzunguko wa siku za mwanamke. Siku hizi zipo ambazo nimujarabu sana kutafuta ujauzito na nyingine sio sana. Hivyo kama unataka kutafuta ujauzito zinagtia yafuatayo:
1.Shiriki tendo la ndoa katika siku hatari zote ama ruka kwa mojamoja
2.Shiriki tendo la ndoa siku ambayo una hamu sanna
3.Shiriki tendo la ndoa utakapoona majimaji ya ukeni yameongezeka
4.Shiriki tendo la ndoa utakapoona joto la mwili wako limeongezeka, si kwa sababu unahoama ama ulilala n.k.

Soma zaidi hapa

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: magonjwa Main: Afya File: Download PDF Views 84190

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Dalili za maambukizi kwenye uume

Post hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye uume, ni dalili ambazo ujitokeza pale maambukizi yanapotokea kwenye uume.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo

Posti hii inaonyesha namna ya kujizuia,Mambo ya Hatari,na na Mambo yanayopelekea Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo

Soma Zaidi...
Zijue sababu za moyo kutanuka.

Posti hii inahusu zaidi sababu za moyo kutanuka, Kuna kipindi ambapo moyo utoka kwenye hali yake ya kawaida na kutanuka hali ambayo usababisha madhara kwa mwenye tatizo hilo, ila Kuna sababu ambazo usababisha moyo kutanuka kama tutakavyoona.

Soma Zaidi...
Madhara ya minyoo

Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu. Yafuatayo Ni madhara ya minyoo;

Soma Zaidi...
Njia za kupunguza makali ya pressure au shinikizo la damu

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kupunguza ugonjwa wa pressure au shinikizo la damu kwa waliokwisha kupata wanaweza kupunguza na kwa wake ambao hawajapata ni nzuri inawasaidia kuepuka hatari ya kupata ppresha.

Soma Zaidi...
NINI SABABU YA VIDONDA VYA TUMBO

NENO LA AWALI Hapa utaweza kujifunza mambo mengi kuhusu vidonda vyatumbo.

Soma Zaidi...
Dalili za saratani ya mapafu

Saratani ya Mapafu ni aina ya Kansa inayoanzia kwenye mapafu. Mapafu yako ni viungo viwili vya sponji kwenye kifua chako ambavyo huchukua oksijeni unapovuta na kutoa kaboni dioksidi unapotoa nje.

Soma Zaidi...
Nini husababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa wanawake na wanaume

Somo hili linakwenda kukueleza vitu vinavyosababisha maumivu ya tumbo chini ya kitovu

Soma Zaidi...
Zijue dalili za maambukizi ndani ya sikio na madhara yake

Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu inayotumiwa kwa ajili ya kusikia, Kuna wakati mwingine hushambulia na bakteria na virusi

Soma Zaidi...