picha

Dalili za mimba katika mwezi wa kwanza

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza

DALILI ZA MIMBA KATIKA MWEZI WA KWANZA (Ndani ya siku 30)Dalili hizi huweza kuonekana kwa urahisi kuliko hizo ambazo zimetajwa hapo juu. Ijapokuwa dalili hizi zinatokea ndani ya mwezi mmoja lakini zinaweza pia kutokea nje ya mwezi mmoja, yaani mpaka miezi mitatu. Sasa hebu tuzione dlili hizo:-

 

1.Kukosa hedthi.Kama ujauzioto ulishika mwanamke hataweza kupata siku zake. Hii ni dalili ambayowanawake wengi wamekuwa wakiamini kama ndio dalili pekee. Yes hii ni katika dalili kubwa ambazo wanawake wengi wameitaja kuwa ndio dalili yao ya kwanza. Unajuwa ni kwa nini? Ni kwa sababu ndio ya pekee wanayoweza kuigundua. Ukweli ni kuwa kukosa hedhi pekee sio dalili ya ujauzito, hedhi inaweza kukosekana kwa sababu kadhaa kama zifuatazo:-

 

A.Mabadiliko ya homoniB.UjauzitoC.MaradhiD.PIDE.VyakulaF.Stress na misongo ya mawazoG.Matumizi ya madawaH.Mabadiliko ya hali ya hewa.

 

Nini mwanamke afanye baada ya kukosa hedhi?.Yes hili ni swali zuri sana. Mwanamke aliyekosa hedhi kwanza aanze kufikiria kama alishiriki tendo la ndoa katika siku hatari ama laa. Kisha aangalie uwepo wa dalili nyingine kama nitakavyozitaja hapo chini. Kama hana dalili yeyote basui aangalie kama anapata maumivu sehemu yeyote, ama uwepo wa maradhi. Kama vyote hana ni vyema apime ujauzito. Kipimo cha mkojo kinaweza kuchelewa kutoa majibu, hivyo kama atapima wiki ya kwanz na asione kitu basi ni vyema akarudia tena wiki inayofata. Maelezo zaidi juu ya kutumia kipimo nitayataja hapo chini.

 

2.Maumivu ya matiti na chuchu, kujaa kwa matiti na mabadiliko ya rangi za chuchu.Dalili hii huwapata wanawake wengi, hata hivyo wapo ambao hawaipati kabisa. Hebu tuanze kuona kwa ufupi dalili hii. Mabadiliko ya rangi ya chuchu na eneo la kuzunguka chuchu. Hii ipoje ni kuwa mwanamke aliyebeba ujauzoto chuchu zake zinaweza kubadilika na kuweka ukiza na weusi. Inaweza kuwa chuchu pekee na na eneo la chini kuzunguka chuchu.

 

Kwa baadhi ya wanawake wao matiti yanauma na yanakuwa kama yamejawa na kaugumu flani. Wakati mwimgine inaweza kuwa titi moja ama yanaweza kuwa yote ama yakapeana zamu. Ila maumivu haya ni maumivu ambayo yanavumilia si makali kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za kawaida. Kwa wanawake wengine maumivu haya hutokea pale anapoyaminya matiti yake.

 

Hata hivyo maumivu ya matiti pekee sio dalili ya moja kwa moja kuthibitisha ujauzito. Maumivu ya matiti yanaweza pia kusababishwa na maumivu ya kifua, shida katika homoni ama maradhi mengine. Hivyo bado itahitajika kupuma kupata uhakika.

 

3.Kukojoa mara kwa mara.Wiki kadhaa zimepita toka kuingia, homoni mbalimbali zimezalishwa ndani ya mwili,kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mama na mtoto. Homoni hizi zinapelekea mabadiliko mbalimbali ndani ya mwili wa mama, hivyo kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka, mchujo wa damu kuwa mkubwa na uzalishwaji wa mkojo kuongezeka. Hapa mama mjamzito ataanza kuhisi mabadiliko katika kukojoa kojoa. Dalili hii kwa baadhi yao inachelewa kuonekana hadi miezi ya mbele.

4.Mapigo ya moyo kuongezeka.Hapa mwanamke anaweza kujihisi moyo kwenda mbio. Ukweli nikuwa kuna ongezeko la mapigo ya moyo kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya mtoto aliyetumboni hayaathiriki. Dalili hii pia inaweza kuchelewa kuonekana ndani ya mwezi wa kwanza. Kwa baadhi ya wanawake watajihisi lamda ana presha lakini ukweli ni kuwa hii sio presa ni ongezeko tu la mapigo ya moyo.

 

5.Maumivu ya tumbo.Dalili hii inaweza kutokea hata katika wiki kadhaa za mwanzo. Ila mara nyingi hutokea ndani ya mwezi wa kwanza na ni endelevu. Yaani dalili hii inaweza kuendeea mpaka mtoto atakapozaliwa. Mwanamke awe makini sana na maumivu haya. Maana yanaweza kusababishwa pia na mambo mengine ikiwemo maradhi. Maumivu haya hayawezi kuwa makali kiasi cja kushindwa kufanya kazi za kawaida. Yanaweza kufanana na ya hedhi ama kuwa na uafadhali kidogo.

 

DALILI NYINGINE ZA UJAUZITO1.Uchovu wa mara kwa mara

2.Maumivu ya tumbo mara kwa mara

3.Kichefuchefu

4.Tumbo kukuwa.

5.Mtotockucheza

6.Kuongezeka kwa uzito

7.Kupata kiungulia mara kwa mara

8.Kukosa choo

9.Maumivu ya mgongo

10.Hasira za mara kwa mara

11.Maumivu maeneo ya nyonga

12.Kuharisha

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Uzazi Main: Post File: Download PDF Views 17161

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Nini husababisha uke kuwa mkavu

Post hii inakwenda kukupa sababu zinazoweza kupelekea uke kuwa mkavu yaani kukosa majimaji wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Soma Zaidi...
Madhara ya mtoto kuzaliwa akiwa na uzito mkubwa

Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kama mtoto alizaliwa na uzito mkubwa.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia Malaria kwa wajawazito

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuzuia Malaria kwa wajawazito na watoto wao wakiwa bado tumboni, tunajuwa wazi kuwa wajawazito wakipata Malaria inaweza kupelekea mimba kutoka kwa hiyo ili kuzuia tatizo hili zifuatazo ni njia zilizowekwa ili kuz

Soma Zaidi...
Njia za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha.

Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa au kuzalisha kwa sababu kuna familia nyingi zinakosa watoto sio kwa sababu ni tasa ila kuna njia mbalimbali za kuongeza uwezo wa kuzaa kama ifuatavyo.

Soma Zaidi...
Mimba iliyotungia nje, sababu zake na dalili zake. Nini kifanyike kuizuia?

Mimba hatari iliyotungia nje ya mji wa mimba, ni zipi dalili zake na ni kivipo mimba inatungia nje?

Soma Zaidi...