Dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku ya 7 Hadi ya 14
DALILI ZA MIMBA KATIKA WIKI YA KWANZA NA PILI (SIKU 7 MPAKA 14)1.Kuendelea kwa joto la mwili. Kama ulikuwa makini na siku ambayo joto la mwili wako lilikuwa kubwa, kama ulishiriki tendo siku moja ama mbili kabla ama siku ile, basi endapo joto la mwili litakuwa endelevu hii huashiria huwenda ulibeba ujauzito. Kwa nini, ni kwa sababu joto la mwili hutokea baada ya mabadiliko ndani ya mwili hususani homoni mpya huzaliwa kwa ajili ya kuandaa ukuaji wa ujauzito. Mabadiliko haya ya joto yasifananishwe na joto la homa.
2.Katika wiki hii ya kwanza unaweza kuona mabadiliko ya majimaji kwenye uke. Majimaji yaliyokuwa siku za nyuma kidongo yanaweza kuanza kuchukuwa sura ya mfanano wa majimaji meupe ya yai lililovunjwa. Halikadhalika matarajio ni kuwa uke unatakiwa urudi katika hali ya ukavu baada ya kupita siku hatari. Lakini kama ujauzito ulitungwa uke hautarudi katika hali yake ya kawaida ya ukavu hivyo huanza kuzalisha majimaji kwa wingi. Mabadiliko haya si rahisi kuyaona ila endapo utakuwa manini zaidi unaweza kugundua.
3.Kutokwa na damu kidogo (implantation bleeding). damu hii inaweza kutokea mwishoni mwa wiki ya kwanza ama katikati ya wiki ya pili. Damu hii ni kidogo na inaweza kuwa ni matone kadhaa. Haifanani na damu ya hedhi na wala haitoki na maumivu. Damu hii si endelevu inaweza kutoka kwa muda mchache na kukata. Mwanamke anaweza kuona nguo yake ya ndani inamadoa ya damu. Kwa damu hii mwanamke hatahitai kuvaa pedi.
4.Maumivu ya kichwa ama kichwa kuwa chepesi. Hali hii inaweza kuandamana na kizunguzungu. Hali hii si lazima kuipata, hata hivyo wanawake wengine wanaipata ila hawafikirii kuwa ni tatizo kwani hutokea na kuondoka bila ya kuathiri mwili kwa muda mrefu. Hapa anaweza kuona ni hali ya kawaida kama hatatilia maanani mabadiliko haya.
Kumbuka dalili hizo tajwa hapo juu ni ngumu kuziona mpaka uwe makini sana kwani zinaweza kuathiriwa na hali nyingine za kiafya. Kwa mfano joto la mwili linaweza kusababishwa na mambo mengi kama maradhi, uchovu na stress. Majimaji ya ukeni yanaweza kuongezeka kwa sababu ya njia za uzazi wa mpango ama mabadiliko ya homoni
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 web hosting 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Madrasa kiganjani 👉6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Dalili ninazoziona kwangu chuchu zinauma na sjapata period mwezi huu na nlishiriki tarehe 19 mwezi wa tisa
Nini humaanisha kama chuchu zinauma na hupati period mwanaidi mrefu.
Soma Zaidi...Namna ya kumpima mtoto uzito
Posti hii inahusu namna ya kumpima mtoto uzito, ni njia ambayo utumika kujua uzito wake na maendeleo ya mtoto.
Soma Zaidi...Dalili za kuziba kwa mirija ya uzazi
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kuziba kwa mishipa ya uzazi, ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya uzazi.
Soma Zaidi...Fahamu mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa
Posti hii inahusu zaidi mtoto aliyetanguliza matako wakati wa kuzaliwa, kwa kawaida tunajua kwamba mtoto wakati wa kuzaliwa ni lazima atangulize kichwa ila Kuna kipindi mtoto anatanguliza matako, kuna aina nne za mtoto kutanguliza matako.
Soma Zaidi...Mimba changa: Dalili za hatari unazotakiwa kuzijua.
Miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito (trimester ya kwanza) ni kipindi nyeti sana kwa ukuaji wa mtoto na mabadiliko ya mwili wa mama. Ingawa ni kawaida kuhisi uchovu au kichefuchefu kidogo, kuna baadhi ya dalili ambazo si za kawaida na zinaashiria dharura ya kitabibu. Makala hii inaangazia ishara za hatari unazopaswa kuzitilia maanani ili kulinda afya yako na ya kiumbe ulichobeba.
Soma Zaidi...