image

Dalili za mimba ya watoto mapacha

Makala hii itakwenda kukupa dalili ambazo zinaonyesha kuwa mimba ni ya mapacha. Dalili hizi zitahitajika kuthibitishwa na kipimo cha daktari ili kujuwa kuwa ni kweli.

Mapacha hutokea endapo mbegu Mwanamke atatoa mayai mawili na yote yakarutubishwa mapacha wa aina hii ni mapacha ambao hawafanani. Na pia mapacha hutokea endapo yai lililorutubishwa nikajigawa sehemu mbili na kila moja katika sehemu hizo ikakuwa kama mtoto. mapacha wa aina hii hufanana.

 

Dalili za mapacha ni kawaida na zile za mimba za kawaida. hata hivyo kunakuwa na ongezeko la ukali wa dalili hizo. Pia kuna dalili baadhi ambazo hawezi kuzipata mwenye mimba ya mtoto mmoja. Dalili za kawaida za mimba ni kama:

  1. kukosa hedhi
  2. maumivu ya tumbo
  3. kupata kichefuchefu
  4. uchovu
  5. maumivu ya tumbo na kichwa

 

Dalili ambazo ni za kawaida za mimba lakini mwenue mappacha zinaweza kuwa kali zaidi:

  1. Kujaa sana kwa maziwa
  2. maumivu makali ya maziwa
  3. uchovu mkali sana
  4. kuhisi njaa kali na kupata hamu ya kula

 

Tofauti na dalili hizo sasa nitakwenda kukuelekeza daili za mimba mapacha. Hata hivyo dalili hizi zinahitaji kuthibitishwa na kipimo ili kuwa na uhakika kama ni mimba mapacha. Dalili hizo ni kama:-

  1. Mtoto kuanza kucheza mapema sana tofauti na mimba nyingine
  2. Mtoto anapocheza unahizi anacheza kwenye maeneo tofautitofauti ya tumbo na sio sehemu moja.
  3. tumbo huwa kubwa zaidi na hukuwa kwa haraka sana.
  4. kuongezeka kwa uzito haraka haraka
  5. mapigo ya moyo ya mtoto huwa ni zaidi ya mapigo ya mtoto mmoja.

 

Changamoto za mimba mapacha

Mwanamke mwenye mimba ya mapacha anaweza kupatwa na changamoto ambazo zinaweza kuwa kali zaidi ya asiye na mpacha. Changamoto hizo ni kama:-

  1. ongezeko la shinikizo la juu la damu (presha ya kupanda) wakati wa ujauzito
  2. Yupo hatarini kupata kisukari cha mimba
  3. uchache wa majimaji ya amniotic fluid
  4. kujifunguwa watoto njiti
  5. kupasuka kwa placenter

 

Changamoto za mimba mapacha sio tu sitaishia kwa mama bali pia zinaweza kumpata mtoto ama watoto. Matatizo yanayoweza kuwapata watoto ni pamoja na:-

  1. Ubongo kuvuja damu
  2. Kuzaliwa njiti
  3. kuzaliwa na uzito kidogo
  4. kuwa na tatizo la kupata baridi
  5. mtoto kushundwa kula
  6. mtoto kupata matatizo ya kuona

 

Nini kifanyike kumlinda mama na watoto

Kutokana na changamoto ambazo mama mwenye mimba mapacha anaweza kuyapata ama matatizo ambayo yanaweza kuwapata watoto, hapa nitakupa mambo ya kufanya kukabiliana na shida hizo:-

  1. kuhudhuria clinic kila inapofika tarehe ya kwenda bila kukosa
  2. onana na daktari kila unapopata tatizo la kiafya.
  3. kula vizuri
  4. pata muda wa kuoumzika
  5. fanya mazoezi hata ya kutembea
  6. kunywa maji mengi
  7. kuwa na furaha. epuka mambo ya kukuletea misongo ya mawazo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 15596


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Nini kinasababisha uume kutoa maji meupe bila muwasho,na tiba yake ni ipi
Je unasumbuliwa na Majimaji kwenye uume. Je unapata miwasho, ama maumivu wakati wakukojoa. Soma Zaidi...

Huduma kwa wasioona hedhi
Posti hii inahusu zaidi msaada au namna ya kuwahudumia wale wasioona hedhi na wamefikiwa kwenye umri wa kuweza kuona hedhi. Soma Zaidi...

Dalili za mimba changa
Zijuwe dalili 17 za mimba na mimba changa, kuanzia siku ya kwanza mpaka mwezi mmoja Soma Zaidi...

Dalili za mimba katika mwezi wa kwanza
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba katika mwezi was kwanza Soma Zaidi...

tuseme nilifanya ngono jana na leo nipata period,je kuna uwezekano wa kupata mimba
Mimba inatungwa katika siku maalumu na hazizidi 10. Sio kila ukishiriki tendo unaweza pata mimba. Je unaweza kupata mimba baada ya kushiriki tendo wiki moja kabla ya kuingia hedhi? Soma Zaidi...

Sababu za uvimbe kwenye matiti na dalili zake kiafya.
Soma Zaidi...

Dalili za tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume. Soma Zaidi...

Hatua Saba za kutibu au kuepuka uvimbe kwenye kizazi
Posti hii inahusu zaidi hatua ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kutibu uvimbe au kwa kitaalamu huitwa fibroids. Hizi hatua zikitumika uweza kusaidia kupunguza kiwango cha kupata au kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi. Soma Zaidi...

Nataka nijue Kuwa njia yakuzuia mimba wakati Wakufany tendo La ndoa
Je ungependa kuijuwa Njia ya kuzuia mimba wakati wa tendo la ndoa?. Posti hii itakwenda kukufundisha ujanja huu. Soma Zaidi...

Jinsi ya kupata mtoto wa kiume
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nadharia ya kupata mtoto wa kiume. Soma Zaidi...

Namna ya kutunza joto la mtoto mara tu baada ya kuzaliwa.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kutunza joto la mtoto mara tu anapozaliwa,tunajuwa wazi kuwa Mama anaweza kujifungulia sehemu yoyote ile kabla hajafika hospitalini kwa hiyo mtoto anapaswa kuwa na joto la mwili la kutosha i Soma Zaidi...