image

Dalili za minyoo na sababu zake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za minyoo na sababu zake

Dalili za minyoo, sababu zake na kuiepuka minyoo.

 

 

Minyoo ni katika wadudu vimelea vinavyowapa shida watu wengi leo hii. Minyoo sio virusi wala bakteria kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakidhania.minyoo ipo katika makundi meengi na huishi katika maeneo mbalimbali kwenye miili yetu ikiwemo tumbo, ini, utumbo, ubongo na kwenye damu na maeneo mengine. Dalili za minyoo hutofautiana sana kulingana na aina ya minyoo na wapi ipo. Lakini zipo dalili zenye kufanana kwa minyoo wote. Katika makala hii nitakwenda kukujuza baadhi ya dalili za minyoo katika mwili wako, pia tutaona sababu za kupata minyoo, wapi minyoo inapatikana na vipi tutaizuia:-

 

Utaweza kupata minyoo katika hali zifuatazo:-

1.kula kitu kisichooshwa kwema kwa maji yaliyo safi na salama

2.Kunywa maji ambayo si masafi na si salama

3.Kula nyama ambayo haikuiva vyema, ama nyama mbichi

4.Kutembea pekupeku kwenye ardhi yeye minyoo

5.Kula udongo,

6.Kinyesi cha wanyama na binadamu

 

 

DALILI ZA MINYOO

Wakati mwingine ni vigumu sana kujua kama una minyoo, kwani minyoo wanaweza kukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu bila ya kuonesha dalili yeyote, ama madhara yeyote. Na dalili za minyoo pia hutofautiana sana, kulingana na aina za minyoo. Lakini zifuatazo ni katika dalili kuu:-

1.Kichefuchefu

2.Kukosa hamu ya kula

3.Maumivu ya tumbo

4.Kupungua uzito

5.Uchovu wa viungo

6.Kuona utelezi mwingi kama kamasi kwenye kinyesi

7.Kuona minyoo kwenye kinyesi.

8.Kuona damu kwenye kinyesi

9.Tumbo kujaa

 

Dalili hizi kama nilivyotangulia kusema kuwa zinatofautiana kulingana na aina ya minyoo. Sasa hebu tuone kwa ufupi dalili hizi kulingana na aina ya minyoo:-

 

1.minyoo aina na tapeworm dalili zao ni:

A.Kuvimba kwa ngozi ama kujaa ama kujaa kwa tumbo

B.Kuwa na alegi

C.Kuwa na homa

D.Matatizo katika mfumo wa fahamu, kama kifafa

 

2.minyoo aina ya hookworm dalili zao ni kama:-

A.Kuwashwa

B.Kupata ugonjwa wa anaemia (upungufu wa seli hai nyekundu kwenye damu) hivyo kukosa oksijeni ya kutosha mwilini

C.Kuwa na uchovu wa hali ya juu.

 

3.minyoo aina ya trichinosis, minyoo hawa wana dalili kama:-

A.Kupata homa

B.Kuvimba kwa uso

C.Maumivu ya misuli na kuchoka

D.Maumivu ya kichwa

E.Kutokupenda kupigwa na mwanga

F.Matatizo katika macho (conjuctivist)





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1693


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Dalili na ishara za shambulio la moyo
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Dalili na ishara za shambulio la moyo. Shambulio la moyo huzuia damu yenye oksijeni kufika kwenye moyo hivyo hupelekea tishu kufa. Na Ugonjwa huu mtu akicheleweshewa matibabu huweza kupata mshtuko wa moyo mpaka kifo. Soma Zaidi...

Dalili za coma
Coma ni hali ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu ambayo inaweza kusababishwa na matatizo mbalimbali Jeraha la kichwa , Kiharusi, Tumor ya ubongo, ulevi wa dawa za kulevya au pombe, au hata ugonjwa wa msingi, kama vile Kisukari au maambukizi. Soma Zaidi...

Magonjwa yanayowashambulia watoto wachanga
Watoto wachanga ni watoto wenye umri chini ya miaka mitano, watoto hawa hushambulia na maginjwa mara kwa mara na kusababisha ukuaji wao kuwa dunk, Soma Zaidi...

Je wiki 1 dalili zinaonyesha za maambukizi ya ukimwi na wiki 3 vipimo vinaweza kuonyesha Kama umeasilika
Muda ambao maambukizi ya virusi vya ukimwi kuonyesha dalili unaweza kutofautiana kutika mtu hadi mwingine. Soma Zaidi...

Tahadhari za ugonjwa wa UTI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu tahadhari za kuchukua ili kujikinga na UTI Soma Zaidi...

Huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum.
Posti hii inahusu huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum, ni wanawake ambao wana shida ya akili, walionyanyaswa kijinsia, wakimbizi na wote wenye matatizo mbalimbali. Soma Zaidi...

AINA ZA MINYOO: tapeworm, livefluke, roundworm, hookworm, flatworm
AINA ZA MINYOO Minyoo ambao wanaweza kuishi ndani ya mwili wa binadamu wapo aina nying, lakini hapa nitakueleza aina kuu tatu za minyoo hawa. Soma Zaidi...

Njia za kupambana na saratani
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na saratani Soma Zaidi...

Fahamu kuhusu Ugonjwa wa ukoma
Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa ukoma, ni Ugonjwa unaosababishwa na mdudu anayeitwa mycobacterium leprae, mdudu huyu kwa kawaida uathiri sana sehemu za ngozi na sehemu za Neva mbalimbali za mwili Soma Zaidi...

Kwani minyoo hukaa sehem gani ya mwili?
Minyoo ni katika parasite, yaani ni viumbe wanaokaa kwenye mwili na kujipatia chakula chake humo. Katika miili yetu minyoo huishi na kula kuzaliana na kukuwa. Kama unahitaji kujuwa wapi hasa wanakaa mwilini mwetu, endelea na makala hii Soma Zaidi...

Dalili na ishara za kuvimba kope.
Posti hii inaonyesha Dalili na ishara za kuvimba kope ambayo kitaalamu hujulikana Kama blepharitis. Soma Zaidi...

mfano mtu ametoka kusex, jana alafu Leo akikojoa mkojo una muhuma na Wa mwisho unatoka damu, itakuwa ugonjwa gani eti,
Soma Zaidi...