Dalili za mtoto Mwenye UTI

Posti hii inahusu zaidi dalili za mtoto Mwenye UTI,ni dalili ambazo uwapata watoto wadogo chini ya umri wa miaka mitano.

Dalili za UTI kwa mtoto chini ya umri wa miaka mitano.

1. Mtoto anakuwa na njano

Mtoto mdogo mwenye chini ya umri wa miaka mitano akiwa na ugonjwa wa UTI akiwa na Maambukizi ya UTI anaweza kuwa na njano kama dalili mojawapo ya ugonjwa wa UTI.

 

2. Joto la mwili kushuka kuzidi kiasi

Mtoto mdogo akiwa na ugonjwa wa UTI joto lake la mwili kushuka kupitia kiasi, hii utokea hasa kwa watoto wenye Chini ya umri wa miezi miwili kwa hiyo mama akiona dalili hii anapaswa kumwangalia mtoto wake na kupima UTI.

 

3. Mtoto akiwa na UTI anaweza kuharisha na kutapika, hii utokea kwa sababu maambukizi yanakuwa yameenea sehemu mbalimbali za mwili na usababisha kutoa kila kitu ambacho uingia mdomoni na kumfanya mtoto aanze kutapika na kuharisha, lakini si kila mtoto anayeharisha na kutapika ni kwa sababu ya ugonjwa wa UTI lakini mama na mlezi wanapaswa kupima mtoto ikiwa ataonyesha dalili za kuharisha na kitapika.

 

4.Maumivu ya chini ya Tumbo.

Hii ni dalili ambazo ujitokeza kwa watoto kuanzia miezi miwili mpaka miaka mitano, kwa Sababu ya maambukizi kuenea sehemu mbalimbali tumbo uanza kuuma hasa chini ya kitovu kwa hiyo mtoto kama hawezi kuongea ukimgusa kwenye tumbo anasikia maumivu lakini wale wenye uwezo wa kuongea wanaweza kuponyesha dalili.

 

5.Maumivu wakati wa kukojoa

Hii ni dalili mojawapo kwa mtoto Mwenye dalili ya UTI, kwa Sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo na bakteria wameshaharibu kibofu mtoto usikia maumivu makali wakati wa kukojoa na pengine uanza kulia Lia kwa sababu ya maumivu.hapa mtoto kama anaweza kuongea atakwambia kama hawezi utaona analia wakati wa kukojoa.

 

6. Kiasi Cha kikohoa kwa mtoto kuongezeka.

Hii utokea kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo, kwa hiyo kibofu Cha mkojo hushindwa kutunza mkojo kwa mda mrefu na halimaye mkojo uanza kutoka mara kwa mara. Kwa hiyo hii Dalili ukolijitokeza mama inabidi awe makini kwenda kwenye vipimo Ili kuangalia kama Kuna UTI au la.

Angalisho: hapo juu ni Dalili za UTI kwa watoto iwapo mtoto atapatwa na dalili hizo usinunue dawa kumpatia ukadhani mara Moja ni UTI Bali inabidi kuchukua vipimo maana hizo Dalili uweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021/12/11/Saturday - 09:25:03 am     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 6139

Post zifazofanana:-

Maji pia yanawezakuwa dawa kwa akili
Umeshawahi kuumwa na dawa yako ikawa maji? Huwenda bado basi hapa nitakujuza kidogo tu, juu ya jambo hili. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al humazah
Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka. Soma Zaidi...

Tofauti za uke
Posti hii inahusu zaidi tofauti mbalimbali za uke, kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo mbalimbali kwenye mwili wa binadamu kuna tofauti mbalimbali za ute kutegemea na hali iliyopo. Soma Zaidi...

Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa. Soma Zaidi...

Hizi ni kazi za mapafu mwilini
Makala hii itakwenda kukufundisha kazi 5 za maafu mwilimi. Wengi tunajuwa tu kuwa mapafu yanafanya kazi ya kupumuwa. ila si hivyo tu yapo mengi zaidi. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula pera
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula pera Soma Zaidi...

Kuelekea bonde la uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

Maswali kuhusu hali ya bara arabu zama za jahiliyyah
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Dalili za kasoro ya moyo za kuzaliwa kwa watoto
Ikiwa mtoto wako ana kasoro ya moyo wa kuzaliwa, ina maana kwamba mtoto wako alizaliwa na tatizo katika muundo wa moyo wake. Baadhi ya kasoro za moyo za kuzaliwa kwa watoto ni rahisi na hazihitaji matibabu, kama vile tundu dogo kati ya chemba za moyo amb Soma Zaidi...

Sababu zinazopelekea kukosa Usingizi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kukosa usingizi. Usingizi ni ugonjwa unaoendelea ambao unaweza kufanya iwe vigumu kusinzia, vigumu kubaki usingizini au vyote viwili, licha ya fursa ya kupata usingizi wa kutosha.Ukiwa na kukosa usi Soma Zaidi...

Habari,mfano umekunywa dawa za chupa hizi halafu baadae unagundua chupa ilikuwa na UFA nn kofanyike
Kunywa soda ama dawa kwenyechupa zakioo ambayo ina ufa ama mipasuko ni hatari. Ni kwa sababu huwezijuwa huwenda kipande kikaingia mdomoni na umangimeza. Sasa nini ufanye endapo umeshakula? Soma Zaidi...

Nini husababisha kizunguzungu?
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo mbalimbali ambayo husababisha kizunguzungu. Soma Zaidi...