DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA MKOJO KUSHINDWA KUTOKA KWENYE KIBOFU CHA MKOJO


image


Post hii inahusu zaidi dalili za mtu Mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.


Dalili za Mtu mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.

1. Kushindwa kukojoa kwa massa nane mpaka Kumi na mtu akiwa anakunywa  vinywaji vya kawaida.

 

Ukiona kuwa mtu anashindwa kukojoa kwa masaa nane mpaka Kumi na ukizingatia mtu anakuwa anakunywa vinywaji vya kawaida kama vile maji, juice, uji na mambo mengine yanayonyweka lakini mtu huyo hakojoi ndani ya maasaa nane mpaka Kumi anakuwa na shida kwenye kibofu Cha mkojo.

 

Kwa hiyo mtu huyo anapaswa kuwekewa kwenye uangalizi mkubwa Ili kuweza kuangalia shida Iko wapi na kumsaidia Ili aweze kutoa mkojo kwenye kibofu na kuendelea na maisha yake ya kama kawaida.na shida hii inaweza kutatuliwa kama kawaida.

 

2. Kuvimba kwa kibofu Cha mkojo mpaka hata ukimgusa mgonjwa sehemu ya chini ya tumbo unaweza kuhisi kibofu kama kimetuna.

 

Hali hii utokea pale ambapo mkojo mwingi huwa kwenye kibofu na uendelee kujikusanya ndani yake na hauwezi kutoka na baadae uendelea kujikusanya ndani ya kibofu Cha mkojo na hatimaye kibofu kuvimba na mtu akikigusa anaweza kusikia jinsi kulivyovimba na ukimgusa mgonjwa abatumia na kuhangaika sana kwa hiyo tunapaswa kuhakikisha kuwa mgonjwa anapona kabisa kwa kumpeleka mgonjwa hospitalini na kupata huduma muhimu inayostahili.

 

3. Magonjwa anakuwa na hamu ya kupitisha mkojo makini hawezi kufanya hivyo.

Hali hii utokea kwa mgonjwa pale anapokuwa na hamu ya kupitisha mkojo lakini hawezi kabisa na dalili zozote za kuwepo kwa mkojo kwenye kibofu zipo, hali hii utokea kwa sababu ya maambukizi kwenye kibofu Cha mkojo ambapo mkojo unakosa sehemu ya kupitia kwa hiyo wakati mwingine mgonjwa huwa na maumivu makali, kwa hiyo tukiona kitendo Cha namna hii mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi Ili aweze kuruhusu mkojo kupita  na kuendelea na maisha ya kila siku.

 

4.Mgonjwa anakuwa hatulii, anakuwa anasikia maumivu makali sana kwenye kibofu Cha mkojo.

Katika kipindi hiki mgonjwa anakuwa hatulii kwa sababu anatafuta njia yoyote Ili aweze kupitisha mkojo kwa hiyo kutulia ni shida, na mgonjwa anakuwa na maumivu makali kwenye kibofu Cha mkojo kwa sababu ya mkojo unazidi kujaa kwenye kibofu na misuli unaendelea kujaa na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa hali inayofanya mgonjwa kusikia maumivu makali sana . Kwa hiyo mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi kwa sababu ya hali ngumu aliyonayo.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    2 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    5 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Dawa ya vidonda vya tumbo
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

image Mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtu aliyepoteza fahamu, kama mtu amepoteza fahamu Kuna mambo muhimu yanapaswa kuangaliwa kwa makini kama ifuayavyo. Soma Zaidi...

image Fahamu Ugonjwa wa kifaduro kwa watoto chini ya miaka mitano
post hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa kifaduro ambao hujulikana Kama Pertussis pia inajulikana kama kifaduro ni maambukizi ya bakteria ambayo huingia kwenye pua yako na koo. Soma Zaidi...

image Dalili za mimba changa
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba changa Soma Zaidi...

image Upungufu wa vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini Soma Zaidi...

image Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini
Posti hii inahusu zaidi Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini, ni Ukosefu wa madini ya Shaba mwilini ambao usababisha madhara kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Dalili za maumivu yanayosababishwa na mtiririko mdogo wa Damu.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maumivu yanayosababishwa na mtiririko mdogo wa damu, kwa kawaida wakati wa mazoezi. Wakati mwingine huitwa upenyo wa vipindi, hali hii kwa ujumla huathiri mishipa ya damu kwenye miguu, lakini upenyo unaweza kuathiri mikono pia. Mara ya kwanza, labda utaona maumivu wakati tu unafanya mazoezi, lakini jinsi Ugonjwa huu unavyozidi, maumivu yanaweza kukuathiri hata wakati umepumzika. Soma Zaidi...

image Nini husababisha mdomo kuwa mchungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa mwenye kizunguzungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu Soma Zaidi...

image Tiba mbadala za vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukuletea tiba mbadala za vidonda vya tumbo Soma Zaidi...