Dalili za saratani kwa watoto.

Posti hii inahusu zaidi Dalili za saratani kwa watoto, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa watoto na ikiwa mlezi au mzazi akiziona tu anaweza kutambua mara moja kwamba hii ni saratani au la na kama bado ana wasiwasi anaweza kupata msaada zaidi kutoka kwa wataa

Dalili za saratani kwa watoto wadogo.

1.Kwanza kabisa mtoto anakuwa na uvimbe usio wa kawaida  na ambao hauna maumivu kwenye sehemu za mashavu,  kwenye shingo, tumbo, miguuni na sehemu zozote za mwili, kwa mara ya kwanza uvimbe huu unakuwa hauna maumivu hata kidogo lakini ikiwa  umetibuliwa au kuchokonolewa uvimbe huu unaweza kubadilika na kutengeneza kitu kingine na kusababisha maumivu kwa mtoto.

 

2. Kwa hiyo baada ya kuona uvimbe wa aina hii na mtoto anaendelea na maisha bila kuonyesha Dalili yoyote ya maumivu kwanza  kabisa mtoto anapaswa kupelekwa kwa wataalamu wa magonjwa ya saratani na epuka kabisa kutingisha uvimbe huu kwa kutumia waganga wa kienyeji ambao hawana utaalamu wowote au mzazi mwenyewe kuamua kuchokonoa uvimbe huu, mpeleke mtoto hospitalini ili aweze kupata utaratibu kutoka kwa wataalamu wa afya.

 

3. Macho ya mtoto kuwa mekundu kuvimba, kuongezeka, au upofu kwa ghafla.

Kwa kawaida kwa upande wa macho ya mtoto yanaanza kidogo kidogo kuwa mekundu na siku kwa siku wekundu unazidi  na hatimaye mtoto anashindwa kuona linaweza kuanza jicho moja na baadae likaingia la pili au yote mawili yanaweza kupata shida kwa wakati mmoja na kama mtoto hajapata huduma mapema upofu unaweza kutokea kwa mtoto .

 

4. Pia kwa wakati mwingine  damu utoka puani na kwenye fizi. 

Na pia hizi ni mojawapo ya Dalili za saratani kwa watoto wadogo kwa sababu damu zikianza kutoka puani uanza kidogo kidogo na uongezeka zaidi pale kama kuna joto la kwenye mazingira likiwa juu na pia mtoto damu uanza kupungua siku kwa siku na hata damu ikiongezwa inapungua na kwa upande wa fizi ikitokea mtoto kama amefikia wakati wa kupiga maswaki akipiga damu utoka kwa wangi kwenye fizi. Kwa hiyo walezi na wazazi wanapaswa kufika kwa wataalamu wa afya ili kupata matibabu zaidi.

 

5. Mtoto kukonda na kupungua uzito bila sababu.

Kwa wakati mwingine mtoto anaanza kukonda na kupungua uzito bila sababu na huku anakuwa anacheza kawaida ila anakonda na uzito unapungua kwa hiyo Mama anapaswa kumpeleka mtoto huyo kwa wataalamu wa afya ili kuweza kujua tatizo ni nini kwa mtoto, na kwa wakati huu hata mtoto akipewa lishe ya aina yoyote anaongezeka kidogo na baadae hali inakuwa kama kawaida yaani kukonds na kupungua uzito.

 

6. Maumivu ya kichwa kwa mda mrefu na kutapika.

Kwa kawaida kwa watoto wale ambao wanaweza kuongea anaweza kukwambia jinsi anavyojisikia mara nyingi utasikia analalamika kuhusu kichwa kwa wale ambao hawajui kuongea atakuwa analia mara kwa mara , na pia kwa upande wa kutapika mtoto anaweza kutapika kwa mda mrefu hata kama hajala lolote anatapika tu na pia kwa wakati mwingine matapishi huwa mengi kuliko chakula ambacho anakula hali ambayo uwatia wasiwasi pia wazazi  wengine wanaweza kuwa na imani potovu kuhusu hilo.

 

7. Mtoto anaweza kudhoofika na kuacha kucheza pamoja na watoto wengine.

Kwa upande mwingine mtoto anakosa raha anaanza kudhoofika na anashindwa kucheza na wengine kwa wakati mwingine Mama au walezi wanaweza kuchukulia kubwa ni sehemu ya maisha kubwa mtoto huwa hachezi kumbe kuna tatizo ndani yake kwa hiyo uchunguzi kwa mtoto ni lazima ili kuweza kuona kuna tatizo gani, kwa hiyo wazazi au walezi wanapaswa kuwa pamoja na watoto ili kuangalia mabadiliko katika makuzi yao.

 

8. Kwa wakati mwingine mtoto akipata ajali kidogo anatokea na damu nyingi ukilinganisha na kidonda chake kwa hiyo unakuta damu inapungua mwilini na kwa mara nyingine Dalili za wazi ujitokeza ambapo mtoto akipata ka jeraha na damu zikitoka anabadilika rangi na kuwa na rangi nyeupe fulani hivi kwenye mwili.

 

9.Kwa hiyo kitu ambacho tunapaswa kuelewa kubwa saratani kwa watoto pengine uonyesha dalili mbalimbali ambazo zinaweza pengine kuleta mashaka kwa wazazi kwa hiyo basi wazazi na walezi wanapaswa kuwa makini ili kuepukana na Imani za kishirikina na kuweza kujua wazi kuwa ni magonjwa ambayo yako kwenye jamii mbalimbali.

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/03/10/Thursday - 09:56:01 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1494

Post zifazofanana:-

Matibabu ya VVU na UKIMWI
Somo Hili linakwenda kukuletea matibabu ya VVU/UKIMWI Soma Zaidi...

Watu walio hatarini kupata fangasi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya watu walio hatarini kupata fangasi Soma Zaidi...

Maelekezo muhimu kwa Mama au mlezi wa mtoto mgonjwa
Posti hii inahusu zaidi maelekezo muhimu kwa mama au mlezi wa mtoto mgonjwa. Ni maelekezo muhimu hasa wakati wa kutoa dawa kwa mtoto. Soma Zaidi...

Napenda kuuliza mke wangu anamuda wa wiki moja . tumbo na maziwa vinauma je dalili hizo zinawekuwa ni ujauzito...?
Maumivu ya tumbo kwa mjamzito huweza kuanaa kuonekana mwanzoni kabisa mwaujauzito, ndani ya mwezi mmoja. Ikabidi si dalili pekee ya kuwa ni mjamzito. Soma Zaidi...

Sababu zinazopelekea kukosa Usingizi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Sababu zinazopelekea kukosa usingizi. Usingizi ni ugonjwa unaoendelea ambao unaweza kufanya iwe vigumu kusinzia, vigumu kubaki usingizini au vyote viwili, licha ya fursa ya kupata usingizi wa kutosha.Ukiwa na kukosa usi Soma Zaidi...

Upungufu wa homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni ya estrogen na dalili zake, aina hii ya homoni ikipungua mwilini uleta madhara na matatizo mbalimbali kwenye mwili. Soma Zaidi...

Faida za apple kwa Mama mjamzito
Posti hii inahusu zaidi faida za apple kwa mama mjamzito, ni faida anazozipata mama akiwa mjamzito kwa sababu ya kuwepo kwa vitamini mbalimbali kwenye apple ambavyo usaidia katika makuzi ya mtoto.I Soma Zaidi...

Dalili za ugonjwa wa Saratani.
Saratani inahusu ugonjwa wowote kati ya idadi kubwa ya magonjwa ambayo yanaonyeshwa na ukuaji wa seli zisizo za kawaida ambazo hugawanyika bila kudhibitiwa na kuwa na uwezo wa kupenya na kuharibu tishu za kawaida za mwili. Saratani mara nyingi ina uwezo Soma Zaidi...

Zijue sababu za kutobeba mimba
Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinamfanya mama au dada kutobeba mimba. Kwa hiyo tutaziona hapo chini kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za vyakula vya vitamini Soma Zaidi...

Namna ya kugundua mtu mwenye kaswende.
Post hii inahusu zaidi njia za kumgundua mgonjwa wa kaswende, njia hizi utumika baada ya kuongea na mgonjwa kuhusu maisha yake hasa kujamiiana na watu mbalimbali. Soma Zaidi...

Je inaweza ukaingia period wakati unaujauzito?
Ukiwa mjamzito unaweza kushuhudia kutokwa na damu. Je damu hii ni ya hedhi? Soma Zaidi...