Dalili za Saratani ya utumbo mdogo.
Posti hii inaonyesha ishara na dalili za Saratani ya utumbo mdogo
Dalili na ishara za saratani ya utumbo mdogo ni pamoja na:
1. Maumivu ya tumbo
2. Ngozi kuwa na manjano na weupe wa macho (jaundice)
3. Kuhisi dhaifu au uchovu usio wa kawaida
4. Kichefuchefu
5. Kutapika
6. Kupungua uzito
7. Damu kwenye kinyesi, ambayo inaweza kuonekana nyekundu au nyeusi
8. Kuhara kwa maji
Jinsi ya kujizuia na ugonjwa wa Saratani ya utumbo mdogo.
1. Kula aina mbalimbali za matunda, mboga mboga na nafaka. Matunda, mboga mboga na nafaka nzima zina vitamini, madini, nyuzinyuzi ambayo inaweza kusaidia kupunguza hatari ya saratani na magonjwa mengine.
2. Punguza kunywa pombe kupita kuasi ikiwezekana acha kabisa. Ukichagua kunywa pombe, punguza kiwango cha pombe unachokunywa kisizidi kinywaji kimoja kwa siku .
3. Acha kuvuta sigara Tafuta njia mbadala ambazo zitakutengenezea mazingira ya kuacha kabisa kuvuta sigara au kutumia tumbaku.
4. Fanya mazoezi . Jaribu kupata angalau dakika 30 za mazoezi.
5. Punguza uzito wako. Ikiwa una uzito mzuri, fanya kazi ili kudumisha uzito wako kwa kuchanganya chakula cha afya na mazoezi ya kila siku.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 Dua za Mitume na Manabii 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 web hosting 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Ugonjwa wa Saratani ya ini.
Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.
Soma Zaidi...Ni bakteria gani husababisha ugonjwa wa pumu
Post hii inakwenda kujibu swali linalosema je ni bakteria aina gani husababisha igonjwa wa pumu.
Soma Zaidi...Nini husababisha Fangasi sehemu za Siri
Katika somo hili tutaeleza sababu kuu zinazopelekea kupata fangasi sehemu za siri, mazingira yanayochochea kuongezeka kwa fangasi, pamoja na vitu vinavyochangia maambukizi na kurudia-rudia kwa tatizo.
Soma Zaidi...Dalili za Mimba Kabla ya Kukosa Hedhi
​Siku za mwanzoni baada ya kutunga mimba, mwili wa mwanamke huanza kuonyesha mabadiliko madogo ya homoni. Post hii inaangazia ishara za awali ambazo zinaweza kujitokeza hata kabla ya siku ya hedhi inayotarajiwa, ikielezea sababu zake na jinsi ya kuzitofautisha na dalili za kawaida za kabla ya hedhi (PMS).
Soma Zaidi...tatizo la kushindwa kujaza misuli ya mwilini na kusinyaa kwa misuli mwilini
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa kusinyaa kwa Misuli. Ni maradhi yanayopelekea uzalishwaji hafifu wa misuli, hivyo kupelekea misuli kukosa protini, kushunwa kukuwa na kusinyaa.
Soma Zaidi...Mambo yanayosababisha kiuno au mgongo kuwa na maumivu
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kusababishwa mgongo wAko au kiuno kwa na maumivu, Mgongo ukiwa na maumivu makali Sana yanaweza kusababishwa shida kubwa ata utakapokaa au ukilala au ukitumia bado maumivu yanakuwepo.
Soma Zaidi...