Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.
Dalili za tezi dume.
1. Kwanza kabisa Mgonjwa anaweza kupata tatizo la kukojoa mkojo ukiwa pamoja na damu.
Kwa kuwepo kwa Maambukizi ambayo kwa kiasi kikubwa yanakuwa yameshambuliwa sehemu za tezi kwa hiyo mkojo ukitoka unakuwa na damu.
2. Pengine uume unashindwa kabisa kusimama au ukisimama ni kwa shida na hauchukui mda mrefu.
Kwa sababu sehemu za mishipa ambayo inakuwa imeshikilia uume ili usimame wakati wa kujamiiana ushambuliwa kwa hiyo inakuwa haina nguvu ya kufanya uume usimame.
3. Kuhisi kukojoa mara kwa mara hasa wakati wa usiku.
Hali hiyo utokea kwa sababu ya sehemu za kibofu na mishipa yake ambayo utumika kuruhusu mkojo kutoka nje huwa imelegea kwa sababu ya kuenea kwa Maambukizi kwenye mfumo wa utunzaji wa mkojo kwa hiyo Mgonjwa ukojoa sana hasa wakati wa usiku kwa sababu usiku kila mfumo unakua umetulia vizuri kabisa.
4. Pia wakati wa kukojoa mkojo utoka kwa mtiririko dhaifu.
Kwa sababu ya kuenea kwa Maambukizi na mishipa ya kibofu nayo ulegea kwa hiyo na spidi ya mkojo upungua.
5. Kupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo na kutilia kwa mkojo baada ya kukojoa .
Kwa hiyo utamkita mtu anahangaika anapokuwa anakojoa na pia kwa wakati mwingine mkojo unaweza kutiririka chini hata kwenye nguo na ukiwa kidogo kidogo.
6.Kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi mtu anapaswa kuwahi hospitalini mara moja ili kuweza kupata matibabu haraka kwa sababu kama shida haijakuwa kubwa walau matibabu yanaweza kusaidia chochote na pia tunapaswa kujua kuwa sio Dalili zote ni za tezi dume ili kuhakikisha ni lazima kwenda hospitalini.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi maumivu wakati wa hedhi, haya ni maumivu ambayo utokea wakati wa hedhi kwa wanawake walio wengi, wengine huwa hawayapati kabisa na wengine hutapata na kwa kiwango kikubwa kutegemea na matatizo mbalimbali kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutumia madawa ya kupunguza maumivu,ni madhara ambayo utokea kwa mtu anayetumia madawa ya kupunguza maumivu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uchafu unaotoka ukeni na rangi zake, kwa kawaida ukeni utolewa uchafu, uchafu huo unaweza kuwa kawaida na unaweza kuwa na rangi mbalimbali kutokana na kuwepo kwa Maambukizi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kuzuia mimba zisiharibike, kwa sababu kila mama anayebeba mimba anategemea kupata mtoto kwa hiyo na sisi hamu yetu ni kuhakikisha kwamba mtoto anazaliwa kwa kuzuia mimba kuharibik
Soma Zaidi...Kupungua kwa idadi ya mbegu za kiume kunamaanisha kuwa Majimaji (shahawa) unayotoa wakati wa kufika kileleni huwa na mbegu chache kuliko kawaida. Hesabu yako ya manii inachukuliwa kuwa chini kuliko kawaida ikiwa una chini ya mbegu milioni 15. Kuwa na idad
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi,kwa kawaida tumesikia akina mama wengi wanalalamika kuhusu kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi na wengine hawajui sababu zake kwa hiyo sababu zifuatazo ni za kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna unavyoweza kumtambua mtoto mwenye Ugonjwa wa Nimonia na tiba anayopaswa kupata mtoto mwenye Nimonia
Soma Zaidi...