Dalili za ugonjwa wa Bawasili
Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa Bawasili, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa mgonjwa ambaye ana ugonjwa wa Bawasili.
Dalili za ugonjwa wa Bawasili.
1. Dalili ya kwanza ni maumivu wakati wa kujisaidia.
Kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye sehemu ya haja kubwa au tayari mishipa midogo kwenye haja kubwa ishapasuka Mgonjwa uhisi maumivu makali wakati wa kujisaidia haja kubwa.
2. Kutokwa na damu wakati wa kujisaidia.
Kwa sababu mishipa ya sehemu ya haja kubwa ishapasuka kwa hiyo Mgonjwa anapojisaidia damu utoka wakati wa kujisaidia.
3. Kuwepo kwa miwasho kwenye sehemu ya haja kubwa.
Kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye sehemu ya haja kubwa miwasho inakuwepo mingi na kunakuwepo na kishawishi cha kujikuna mara kwa mara hali inayosababisha kuenea kwa magonjwa mengine kama vile minyoo na Typhoid.
4. Kuwepo na uvimbe na kinyama kwenye sehemu za siri,
Hali hiyo Usababishwa na kupasuka kwa mishipa midogo sehemu ya haja kubwa hali inayopelekea kuota vinyama au uvimbe kwenye sehemu mbalimbali za haja kubwa.
5. Haja kubwa kujitokeza kwa mda wowote.
Kuna wakati mwingine haja kubwa uja mara kwa mara kwa sababu ya kuwepo nafasi ndogo sehemu ya kuhifadhiwa haja kubwa kwa sababu ya kuota kwa vinyama au uvimbe sehemu hizo.
6. Choo juwa kigumu au mara nyingine kukosa kabisa kwa siku tatu na pia uambatana na Maumivu makali ya kiuno na mgongo.
7. Tumbo kujaa gesi mara kwa mara kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi.
8. Kuhisi njaa mara kwa mara, hali hii utokea kwa sababu ya kutoa haja kubwa mara kwa mara au wakati mwingine kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi.
9. Baada ya kuona dalili kama hizi ni vizuri kabisa kuhakikisha kuwa matibabu ya mapema ni lazima ili kuepuka madhara makubwa zaidi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 kitabu cha Simulizi 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Simulizi za Hadithi Audio 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Mimba ya Uongo ni Nini?
Makala hii inaangazia hali ya kisaikolojia na kimwili inayojulikana kama "Mimba ya Uongo" (Pseudocyesis). Tutaelezea maana yake, dalili kuu ambazo mwanamke anaweza kuzihisi, sababu za kitaalamu zinazosababisha hali hii, na umuhimu wa kupata msaada wa kitabibu na kisaikolojia
Soma Zaidi...Dalili za maumivu ya jino
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za maumivu ya jino
Soma Zaidi...Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo
Posti hii inaonyesha namna ya kujizuia,Mambo ya Hatari,na na Mambo yanayopelekea Ugonjwa wa ukosefu wa mkojo
Soma Zaidi...Dalili za ugonjwa wa UTI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ugonjwa wa UTI
Soma Zaidi...Sababu za kuumwa na tumbo, chini ya kitomvu ama upande wa kulia
Post hii inakwenda kukutajia baadhi tu ya sababu zinazopelekea kuumwa na tumbo. Hali hizi zinawweza kuwapata watu wa jinsia zote katika umri wowote ule. Ijapokuwa nyingine si kwa wote ni kwa baadhi ya watu. hapa nitakuletea sababu 5 tu.
Soma Zaidi...Namna ya kutoa huduma kwa mgonjwa wa Dengue.
Posti hii inahusu zaidi huduma anayopaswa kupata mgonjwa wa ndengue, kwa sababu tunafahamu wazi Ugonjwa huu hauna dawa ila kuna huduma muhimu ambayo anaweza kupata na akaendelea vizuri.
Soma Zaidi...