DALILI ZA UGONJWA WA DONDA KOO


image


Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa Donda Koo ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea viitwavyo kwa kitaalamu corynebacterium diphtheria, ugonjwa huu ushambulia Koo na unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya hewa, mate na mate kutoka kwenye maambukizi.


Dalili za ugonjwa wa Donda Koo.

1. Kuwepo kwa vidonda kooni.

Hali hii utokea kwa mgonjwa mwenye Donda Koo kw kuwepo kwa vidonda kooni ni kwa sababu ya maambukizi ya bakteria ambao ushambulia Koo na kusababisha vidonda na kwa kiwango kikubwa ugonjwa huu uwashambulia hasa watoto wenye Chini ya umri wa miaka mitano kwa hiyo baada ya kutambua Dalili hii mgonjwa anapaswa kumpelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

 

2. Mgonjwa huwa na makamasi yaliyochanganywa na damu.

 

Hii ni mojawapo ya dalili ya  Dondakoo kwa watoto tukumbuke kuwa ugonjwa huu ushambulia sana sehemu za mfumo wa hewa baada ya bakteria kushambulia sehemu za mfumo wa hewa usababisha michubuko kwenye mfumo na kwa sababu ya maambukizi mafua uwepo yakiandamana na damu iliyotoka kwenye sehemu za maambukizi.

 

3. Kuwepo kwa utando kwenye Koo.

Kwa sababu ya kuwepo kwa bakteria usababisha utando kwenye Koo la mtoto ambapo hali hii usababisha mtoto hashindwe kunyonya  au kumeza kitu chochote na mtoto upumua kwa shida, kwa hiyo tunaona ugonjwa huu ulivyo mbaya kwa watoto tunapaswa kuwapeleka watoto kwenye chanjo Ili kuepusha madhara makubwa zaidi kama kuwepo kwa utando kwenye Koo. Ambao huzuia mtoto ashindwe kumeza.

 

4, Maumivu makali ya shingo.

Kwa upande wa mtoto kunakuwepo maumivu makali ya shingo kwa sababu ya kuenea kwa bakteria ambao usambaza maumivu kwenye sehemu mbalimbali kama vile kwenye shingo na Mtoto uhisi maumivu makali na pengine kushindwa kugeuka kwa hiyo tunapaswa kuzingatia chanjo kwa ajili ya kuepuka madhara makubwa kama hayo.

 

5. Kuvimba kwa shingo na kusababisha shingo kuwa kubwa ambayo umnyima mtoto amani na kumfanya mtoto aanze kulia mda wote na kitendo Cha mgonjwa kuvimba shingo huitwa shingo ngoti Ili kuitofautisha  na matimbwitimbwi kwa hiyo jamii inabidi kupewa elimu kuhusu ugonjwa huu na kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo Ili kuepusha madhara mbalimbali yanayotokea kwa mtoto.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    4 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    5 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    6 Hadiythi za alif lela u lela    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa walioingiliwa na uchafu puani.(foreign body).
Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa alieye ingiwa na uchafu puani (foreign body) Soma Zaidi...

image Dawa ya Isoniazid na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi dawa ya lsoniazid nA kazi zake, ni dawa ambayo inasaidia kutibu kifua kikuu kati ya madawa yaliyoteuliwa na kuwa na sifa ya kutibu kifua kikuu. Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu anayetokwa na damu ya pua Soma Zaidi...

image Namna ugonjwa wa herpes simplex unavyosambaa.
Posti hii inahusu zaidi namna ya ugonjwa wa vipele kwenye midomo na sehemu za siri unavyoweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Soma Zaidi...

image Sifa za siku za kupata mimba
Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya sifa za siku za kupata mimba Soma Zaidi...

image Hernia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa hernia Soma Zaidi...

image Dalili za Homa ya uti wa mgongo (meningitis)
Posti hii inahusu zaidi dalili za Homa ya uti wa mgongo, ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye maambukizi kwenye uti wa mgongo. Soma Zaidi...

image Choo kisichokuwa cha kawaida
Posti hii inahusu zaidi Aina ya choo kisichokuwa cha kawaida, ni dalili za choo ambacho siyo Cha kawaida, Ina maana ukiona dalili za choo Cha Aina hii ni vizuri kwenda hospitalini Ili kupata matibabu. Soma Zaidi...

image Mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo
Posti hii inahusu zaidi mambo ya kuangalia kwa mtoto mdogo chini ya umri wa miaka mitano ili kuweza kuweka afya yake kwenye njia safi. Soma Zaidi...

image Mambo yanayopunguza nguvu za kiume
Posti hii inaelezea kuhusiana na nguvu za kiume zinavyopungua na Ni Mambo gani yanayofanya zipungue Soma Zaidi...