Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa inni, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye ugonjwa wa inni, Dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.
Dalili za ugonjwa wa inni
1. Macho na ngozi ya viganja, na nyayo za miguuni kubadilika rangi na kuwa ya njano.
Kwa mtu Mwenye maambukizi kwenda ini rangi ya viganja na nyayo za miguuni kubadilika na kuwa na rangi ya njano hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye ini maambukizi haya uenea sana kwenye sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha baadhi ya sehemu ya mwili kuwa ya njano, kwa hiyo baada ya mtu kuona dalili kama hizi zinatokea anapaswa kwenda mapema hospitalini kwa ajili ya kuchukua vipimo kwa hiyo jamii inapaswa kujua Dalili za mtu Mwenye Homa ya inni kwa kuangalia dalili ya Aina hii.
2. Mara nyingine na rangi ya mkojo ubadilika na kuwa na rangi ya njano.
Kwa watu walio wengi ambao wamashambuliwa na ugonjwa huu rangi ya mkojo nayo ubadilika na kuwa na rangi ya njano, hali hii ni kwa sababu ya maambukizi hasa kama yameingia sana kwenye mwili usambaa mpaka kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha rangi ya mkojo kubadilika kuwa na rangi ya njano, kwa hiyo kitu ambacho tunapaswa kufanya ni kwamba baada ya kuona dalili kama hii tunapaswa kwenda hospitalini kupima Ili kujua uhakika kama ni maambukizi kwenye ini au ni magonjwa mengine na kwa wale ambao hawanywi maji pengine wanaweza kupata na tatizo hili la rangi ya mkojo kuwa ya njano kwa hiyo tunapaswa kupima Ili kujua afya zetu mara kwa mara.
3. Kwa watu wenye maambukizi kwenye inni kinyesi Chao uwa na utando mweupe mweupe ambao ufanana na Ute , kwa hiyo baada ya kuona dalili kama hizi zinaambatana mtu anapaswa kumpelekwa hospitalini kwa ajili ya kupima na kuhakikisha kuwa kama ni maambukizi ya ugonjwa wa inni, kwa hiyo vipimo ni vya lazima kwa sababu kwa vipimo tunaweza kujua maambukizi ya gonjwa hili la inni na kuchukua tahadhari Ili kuepuka kuwaambukiza wengine.
4. Dalili nyingine ni kama vile kupoteza hamu ya chakula kwa sababu maambukizi yanakuwa yameenea sehemu mbalimbali za mwili ambapo mtu upoteza na Ile hamu ya Kawaida ya kupata chakula hali hii ya kupoteza hamu ya kula usababisha na mgonjwa wa Homa ya inni kuishiwa nguvu mara kwa Mara na pengine anapotaka kula chakula uhisi kichefuchefu na kutapika hai hii usababishwa na kitendo Cha kuongezeka kwa maambukizi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Shinikizo la chini la damu (hypotension) litaonekana kuwa jambo la kujitahidi. Hata hivyo, kwa watu wengi, shinikizo la chini la damu linaweza kusababisha dalili za Kizunguzungu na kuzirai. Katika hali mbaya, shinikizo la chini la damu linawez
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili na sababu zinazopelekea Ugonjwa wa kuziba kwa Njia ya machozi yaani kukosa machozi ambayo husababishwa na maambukizi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI
Soma Zaidi...Post hii fupi inakwenda kukujuza juu ya tatizo la fangasi na nini ufanye.
Soma Zaidi...Maambukizi ya H. pylori hutokea wakati aina ya bakteria inayoitwa Helicobacter pylori (H. pylori) inapoambukiza tumbo lako. Hii kawaida hutokea wakati wa utoto. Sababu ya kawaida ya Vidonda vya tumbo, maambukizi ya H. pylori yanaweza kuwa katika za
Soma Zaidi...Fangasi wanaojulikana kama Blastomyces, hawa ni fangasi wanaosababisha maradhi yajulikanayo kama blastomycosis.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za mtu mwenye ugonjwa wa kupungukiwadamu, ni dalili zinazoonekana kwa mtu Mwenye tatizo la upungufu wa damu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa ya koo, ni ugonjwa unaoshambulia sana sehemu ya koo la hewa, na na huwa na dalili zake kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Kaswende ni maambukizi ya bakteria kawaida huenezwa kwa kujamiiana pia ugonjwa huu hujulikana kama syphilis. Ugonjwa huu huanza kama kidonda kisicho na maumivu kwa kawaida kwenye sehemu zako za siri, rektamu au mdomo
Soma Zaidi...Fangasi hawa ni maarufu sana kwa mapunye ya kichwani ama kwenye ngozi mikononi ama miguuni.
Soma Zaidi...