image

Dalili za ugonjwa wa kaswende

Post hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kaswende kwa wajawazito, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa watu wote, kwa sababu ugonjwa huu una dalili ambazo upitia kwa hatua mbalimbali kama tutakavyoona.

Dalili za ugonjwa wa kaswende.

1. Kwa kuwa tangu mwanzoni nimejaribu kueleza kwamba ugonjwa huu upitia kwenye hatua mbalimbali,kwa hiyo tutaanza na hatua ya kwanza ambayo kwa kitaalamu huitwa primary symptoms, kwenye hatua hii mgonjwa anakuwa na vipele ambazo havina maumivu kwa kitaalamu huitwa chancres hivi vidonda hivyo ujitokeza baada ya wiki tatu baada ya maambukizi, hivi vidonda mara nyingi utokea sehemu ambayo sex imefanyiwa kama ni mdomoni vitajitokeza hapo kama ni kwa njia ya haja kubwa vitajitokeza hapo au kama ni kwa njia ya kawaida na penyewe vitajitokeza hapo, kwa hiyo vidonda hivyo kama havijapata matibabu utoweka ndani ya wiki tatu mpaka sita.

 

2. Kwa hiyo kama ikitokea mtu akapatwa na tatizo kama hili na anajua kabisa alifanya ngono bila kinga ni vizuri kabisa kupata matibabu mapema ili kuondoa tatizo kubwa kubwa zaidi, changamoto ni kwamba vidonda hivi mara nyingi huwa haviumi ndio maana watu wengi hawajishughulishi kupima badala yake ni kupotezea na ukizingatia havina maumivu yoyote, madhara ya kutotibu mapema usababisha hali ambayo sio nzuri kama tutakavyoona hapo baadaye.

 

3. Hatua ya pili utokea pale ambapo vidonda vya hatua ya kwaza kutotibiwa , hatua hiyo kwa kitaalamu huitwa primary symptoms,hivi vidonda ambavyo vilikuwepo vinatudi tena sio kwenye sehemu ambayo sex ilifanyika tu  bali ni katika sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye mikono hasa hasa kwenye sehemu ya viganja, kwenye miguu hasa kwenye ukanyagio,pia na rangi yake inakuwa kama ya nyekundu ila sio nyekundu iliyokaza, na pia vidonda hivi vinaweza kuwa hata mdomoni, hali hiyo utokea kwa sababu ya ugonjwa kueneza kwenye sehemu mbalimbali za mwili.

 

4. Katika hatua hii mgonjwa anaweza kushindwa kutembea kwa sababu ya kuwepo kwa vidonda kwenye nyayo za miguu na wakati mwingine hatua hii uambatana na homa, mwili mzima kuchoka,Madonda kwenye koo, kuvimba kwa lymph nodes kwa sababu ya maambukizi, pengine nywele kwenye kichwa unyonyoka , maumivu makali ya kichwa, kupungua uzito, na pia mwili kuishiwa nguvu. 

 

Pengine watu uchanganya dalili hizi na mgonjwa wa HIV kwa sababu dalili za mgonjwa wa HIV hatua ya nne na tatu huwa na dalili kama hizi, mtu kuja kufikia hatua hiyo ni kwamba ugonjwa huu unakuwa umemaliza miaka kama kumi na tano mwilini na ndipo dalili za hapo juu zinaweza kutokea.

 

5 . Kwa hiyo jamii inapaswa kuelezwa wazi kuhusu ugonjwa huu kwa sababu kuna wakati watu wanaenda kupima baada ya kuona dalili kama hizi wakidhani ni maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, na baadae unakuta mtua anapewa majbu kwamba hana maambukizi ya ukimwi na ni kweli anakuwa hana ila shida watu wengi hawapimi kaswende na yenyewe kama haijatibiwa inaweza kumfikisha mtu sehemu mbaya , kwa hiyo kupima kaswende ni lazima ili kuweza kuepukana na matatizo mbalimbali.

 

6. Pia hatua ya mwisho ni hatua ya tatu ambayo kwa kitaalamu huitwa latent phase, ni hatua ya mwisho utokea mara nyingi kama hatua ya pili haijatibiwa na kama matibabu hayajafikiwa mgonjwa anaweza kupoteza maisha, kwa hiyo kupima kaswende ni lazima ili kuweza kuepukana na vifo vya akina mama na watoto wao, twende hospitali dawa ipo na watu wengi wanapona.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1311


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu (gangrene)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na tatizo la damu kutokufikia tishu baada ya kutokea jeraha kwenye tishu ambao hujulikana Kama gangrene inahusu kifo cha tishu za mwili kutokana na ukosefu wa mtiririko wa damu au maambukizi ya bakteria. Ugonjwa wa gangre Soma Zaidi...

Kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ya kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI Soma Zaidi...

Tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nina minyoo
Mie ni kijana wa kiume umri 33, nna tatizo la kujaa mate mdomoni nimeambiwa nna minyoo lakini hata nikinywa dawa sioni afadhali, niliona labda ni pombe nikapumzika kunywa tatizo lipo pale pale japo nisipokunywa haliwi kwa ukubwa ule ila lipo. Soma Zaidi...

Mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu
Posti hii inahusu zaidi mlo kwa wagonjwa wa figo wanaochujwa damu, ni wagonjwa ambao figo zao zimeharibika na zimeshindwa kufanya kazi au pengine kuna uchafu mwingi mwilini ambao uchujwa kwa hiyo kuna vyakula muhimu ambavyo wagonjwa wa figo wanapaswa kutu Soma Zaidi...

Saratani ya Matiti ya wanaume.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Saratani ya matiti ya Mwanaume ni Saratani nadra ambayo hutokea katika tishu za matiti za wanaume. Ingawa saratani ya matiti hufikiriwa zaidi kuwa ugonjwa wa wanawake, saratani ya matiti ya mwanaume hutokea. Saratani y Soma Zaidi...

Fahamu sababu za ugonjwa unanipeleka Kuvimba kwa mishipa ya Damu
posti hii inazungumzia kuhusiana na ugonjwa wa kuvimba kwa mishipa ya damu katika mwili wako wote. Kuvimba kwa Mishipa ya Damu hujulikana Kama Behcet amboyo husababisha dalili nyingi ambazo hapo awali zinaweza kuonekana kuwa hazihusiani. Dalili na ish Soma Zaidi...

Fangasi aina ya Candida
Huu ni ugonjwa wa fangasi wanaosababishwa na mashambulizi ya fangani aia ya yeast waitwao candida. Soma Zaidi...

Madhara ya utapia mlo (marasmus)
Utapiamlo Mkali sana (Marasmus) hufafanuliwa kama aina kali ya utapiamlo ambayo ina sifa ya kupoteza. Utapiamlo uliokithiri umeainishwa katika Utapiamlo Mkali sana (SAM) na Utapiamlo Uliokithiri wa Wastani (MAM), kulingana na kiwango cha kupoteza na kuw Soma Zaidi...

Maambukizi ya H.pylori (Vidonda vya tumbo)
Maambukizi ya H. pylori hutokea wakati aina ya bakteria inayoitwa Helicobacter pylori (H. pylori) inapoambukiza tumbo lako. Hii kawaida hutokea wakati wa utoto. Sababu ya kawaida ya Vidonda vya tumbo, maambukizi ya H. pylori yanaweza kuwa katika za Soma Zaidi...

Walio katika hatari ya kupata magonjwa ya ngono
Posti hii inahusu zaidi watu walio kwenye liski ya kupata magonjwa ya ngono, ni watu wanaofanya mambo yanayosababisha kupata magonjwa ya ngono. Soma Zaidi...

Sababu za miguu kufa ganzi.
Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali,za miguu kufa ganzi,ni tatizo ambalo uwakumba watu wengi na walio wengi hawafahamu kabisa ni sababu zipi ambazo uleta tatizo hili. Soma Zaidi...

Hernia
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa hernia Soma Zaidi...