image

Dalili za ugonjwa wa upele

Posti hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa upele, ni dalili au mwonekano wa mgonjwa wa upele.

Dalili za ugonjwa wa upele.

1. Kwanza kabisa tunafahamu kabisa mdudu anayesababisha ugonjwa huu kwa kitaalamu huitwa mites sarcoptes scabies, huyu mdudu kwa kawaida akishakomaa utaga mayai kwenye vishimo vidogo vya mwili na kuanza kuishi Humo na kusababisha maumivu makali sana kwa mwathirika hasa kama ugonjwa huu haukutibiwa mapema kwa kuwepo kwa mayai kwenye ngozi usababisha na dalili nyingine kama vile 

 

2. Kuwashwa wakati wa usiku.

Tunajua wazi kuwa wakati wa usiku ni mda ambao unakuwa umetulia sana na mwili pia unakuwa kwenye utulivu Fulani hakuna jua Wala kitu chochote cha kukusumbua mwili kwa hiyo ndipo wadudu Hawa uwa active na kuanza kushambulia na kusababisha kuwepo kwa miwasho na mgonjwa uanza kujikuna mara nyingi na kukosa kusinzia.

 

3. Hali ya kukosa kusinzia usababisha watoto kusinzia wakati wa mchana au kama wamefikia hatua ya kwenda shule usinzia darasani na kusababisha kupoteza mda wa masomo kwa hiyo ni vizuri kuwatibu watoto kwa tiba Sahihi na kuwafanya watoto waweze kuhudhulia masomo ipasavyo kwa hiyo wazazi wawe mstari wa mbele Ili kulinda na kuwatunza vizuri watoto Ili waweze kuepuka magonjwa kama haya.

 

4. Kuwepo kwa mikwaluzo kwenye ngozi.

Kwa sababu ya kujikuna sana mara nyingi kunakuwepo na mikwaluzo kwenye sehemu za ngozi na wakati mwingine mikwaluzo uandamana na kutokwa na damu ,hali hii uwanyima Raha watoto kwa sababu mda mwingi wanaendelea na kujikuna sana na pengine wanaweza kuleta maambukizi kwa watoto wenzao na wale wanaoishi nao.

 

5.  Kuwepo kwa vidonda kwenye sehemu mbalimbali za mwili, pindi maambukizi yanapozidi yanasababisha kuwepo kwa vidonda kwenye sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye vidole, kwenye kiwiko, kwenye tumbo, kwenye kiuno, kwenye chuchu za matiti na sehemu mbalimbali za mwili kwa ujumla, kwa hiyo ni vizuri kutibu kwa sababu hizi dalili zikitokea kwa mtu mmoja kwenda familia ni lazima atawaambukiza na wengine

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1925


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Inakuwaje unafanya ngono na aliyeathirika na usipate UKIMWI?
Watu wengi wamekuwa na mawazo kuwa ili nipate ukimwi ninatakiwa nishiriki ngono zembe na aliyeathirika mara ngapi? Majibu ya swali hili ni mafupi tu, ni kuwa unaweza kuathirika kwa ngono zembe ya siku moja tu ndani ya dakika chache. Lakini jambo la kuzing Soma Zaidi...

Visababishi vya ugonjwa wa Varicose vein
Posti hii inahusu zaidi visababishi mbalimbali vya ugonjwa wa vericose veini, ni visababishi mbalimbali ambavyo utokea kwenye mtindo wa maisha kama tutakavyoona. Soma Zaidi...

Nini chanzo cha malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu chanzo cha ugonjwa wa malaria Soma Zaidi...

Presha ya kushuka na matibabu yake
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu presha ya kushuka na matibabu yake Soma Zaidi...

Masharti ya vidonda vya tumbo
Haya ni masharti ya mwenye vidonda vya tumbo. Mgojwa wa vidonda vya hatumbo hatakiwi kufanya yafuatayo Soma Zaidi...

Visababishi vya maambukizi kwenye milija na ovari
Posti hii inahusu zaidi visababishi vya maambukizi kwenye milija na, ni mambo yanayosababisha maambukizi kwenye milija na ovari. Soma Zaidi...

Dalili za mtu aliyekula chakula chenye sumu
Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo. Soma Zaidi...

Dalili za Kufunga kwa ulimi (tongue tie)
Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kufunga kwa ulimi (Tongue-tie) kuanzia Mtoto anavyo zalia mpaka navyokua ni hali inayotokea wakati wa kuzaliwa ambayo kitaalamu hujulikana kama ankyloglossia. Soma Zaidi...

Mtu mwenye maumivu ya tumbo upande wa kushoto anaweza kutumia tiba gani ya asili ambayo inaweza kumsaidia kupunguza maumivu?
je na wewe ni mmoja katika wenye maumivu ya tumbo upande mmoja?. Basi post hii ni kwa ajili yako. Soma Zaidi...

Dalili za mawe kwenye kibofu Cha mkono
Mawe ya kibofu ni mkusanyiko mgumu wa madini kwenye kibofu chako. Mawe kwenye kibofu hukua wakati mkojo kwenye kibofu chako unapokolea, na kusababisha madini katika mkojo wako kung'aa. Soma Zaidi...

Dalilili za tetekwanga
posti hii inazungumziaTetekuwanga . Tetekwanga(varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, kama vile upele. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya mara kwa mara Soma Zaidi...

TIBA YA MINYOO AU DAWA YA MINYOO: praziquantel (biltricide) mebendazole (vermox, emverm) na albendazole (albenza).
TIBA YA MINYOO Moja katika sifa za minyoo ni kuwa wanatibika kwa urahisi pindi mgonjwa akipewa dawa husika. Soma Zaidi...