Dalili za upungufu wa homoni ya progesterone

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.

Dalili za upungufu wa homoni ya progesterone.

1. Pre menstrual syndrome ( ni hali ambayo uwakumba wanawake) kwa kawaida uanza wiki Moja Hadi mbili kabla ya kuona siku zake za mwezi , mwanamke anaweza kuona uchovu  miwasho ya ukeni uwepo wa vipele vyekundu na vyeusi na pengine vipele hivyo vinaweza kutokea kwenye sehemu zake za Siri pamoja na usoni na pia mwanamke anaweza kuwa na mabadiliko ya mood kama ifuatavyo.

 

2. Kutokwa na mimba .

Kama Mama ana mimba inaweza kutoka kwa sababu ya kutokuwepo kwa homoni ya projestron kwa sababu usaidia katika makuzi makubwa ya mtoto.

 

3. Kuongezeka uzito kwa ghafla.

Kuna wakati mwingine unaweza kuona mwanamke anaongezeka Uzito ghafla ukadhani labda maisha yamemkubali kumbe ni upungufu wa homoni aina ya progesterone.

 

4 . Kuwepo kwa wasi wasi ambao haukuwepo hapo mwanzoni hali hii utokea ghafla kwa wanawake kila kitu anachokifanya anakifanya kwa wasi wasi mkubwa sana.

 

5. Kukosa usingizi.

Hali hii utokea sana kwa wamama ambao Wana upungufu wa homoni hii hasa wale akina Mama walioingia kwenye menopause wanaopatwa na hali ya kukoka usingizi.

 

6. Maumivu au uvimbe kwenye maziwa 

Kwa kawaida maumivu kwenye maziwa utokea na kwa mara nyingine uvimbe, kwa upande wa uvimbe matibabu yanaoaswa kutolewa Ili kuepuka matatizo mengine yaliyo makubwa zaidi.

 

7. Kuwepo kwa kizungu zungu mara kwa mara.

Kama homoni hii ya progesterone imepungua utasikia akina Mama walio wengi Wanalalamika kuhusu kizungu zungu.

 

8. Kuwepo kwa ugumba.

Kwa kawaida homoni ya progesterone inasaidia sana kwenye makuzi ya mtoto kwa hiyo ikikosa usababisha Mama kukosa  mtoto inawezekana mimba ikawa imeshatungwa ikatoka au mimba haitungwi kabisa.Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/01/Friday - 09:41:31 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1426


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-