image

Dalili za upungufu wa homoni ya projestron

Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea iwapo Kuna upungufu wa homoni ya progesterone.

Dalili za upungufu wa homoni ya progesterone.

1. Kutokwa kwa mimba.

Kwanza kabisa Mama akiwa na upungufu wa homoni ya progesterone anaweza kutoka mimba kwa sababu homoni hii ni msaada mkubwa katika makuzi ya mimba kama homoni hii ni ndoo kutoka kwa mimba ni kugusa.

 

2.pre menstruation syndrome.

Hali hii inamkumba mwanamke wiki Moja Hadi mbili  kabla ya kuona siku zake za mwezi  Mama anakuwa na uchovu, miwasho sehemu za Siri, vipele vyekundu au vyeusi, pamoja na mabadiliko ya mood kama vile hasira au kuwa na furaha kupita kiasi.

 

3. Kuongezeka uzito kwa ghafla na kuwa na wasiwasi,Kuna kipindi ambapo Mama anaweza kuongezeka uzito kwa ghafla na kuwa na wasiwasi usio wa kawaida hali hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kidogo cha homoni ya progesterone.

 

4. Maumivu ya uvimbe  kwenye maziwa,

Kuna wakati mwingine mama anakuwa na maumivu yanayoambatana na uvimbe pamoja  kwenye matiti hali hii utokana kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kidogo cha homoni ya progesterone na kiwango kikubwa cha homoni ya estrogen.

 

5. Kupata kizungu zungu mara kwa mara.

Kwa kawaida Mama mwenye tatizo hili huwa anapatwa na kizungu zungu mara kwa mara kwa sababu ya kutokuwepo kwa usawia katika homoni ya progesterone kwa kiwango cha kutosha.

 

6. Vipele vyekundu na chunusi hasa usoni  na ngozi kuwa na mafuta mengi na ya kuzidi kiasi .

 

7. Kuwepo kwa maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara hasa kwa akina Mama wlio kwenye wakati wa kujifungua.

 

8. Kupoteza kumbukumbu na kuwepo kwa uzito wa kufikilia.

Kwa wakati mwingine mama anaweza kupoteza kumbukumbu mara kwa mara na kuwepo kwa uzito wa kufikilia mambo.

 

9. Kuwepo kwa ugumba.

Kwa sababu kazi ya homoni ya progesterone ni kusababisha uchevushaji wa mayai na pia kusaidia katika uzalishaji pamoja na kutungwa kwa mimba kwa hiyo homoni hii ikikosa inaweza kusababisha hali ikawa mbaya zaidi na Mama au dada kupata ugumba.

 

10. Pamoja na Daili tulizoziona si dalili zote utokea kwa sababu ya kukosa kwa homoni ya progesterone ni vizuri kabisa kupima au kuwaona wataalamu wa afya endapo umepatwa na tatizo hili hasa kutoka mimba au ugumba unaoendana na dalili kama tulivyoziona hapo juu.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2272


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Dalili za mimba kuanzia week mbili Hadi mwezi
Somo hili linakwenda kukueleza baadhi ya dalili za mimba kuanzia week mbili Hadi mwezi Soma Zaidi...

Kiungulia kwa wajawazito, dawa yake na njia za kukabilianannacho
Wajawazito wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiungulia, makala hii itakujulisha njia za kukabiliana na kiungulia, dalili zake na dawa zake Soma Zaidi...

KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA: kumwaga mbegu mapema
Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika. Soma Zaidi...

Dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za mimba kuanzia siku 7 Hadi 14 Soma Zaidi...

Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito Soma Zaidi...

Je matiti kujaa na chuchu kuuma inakua ni dalili za hedhi?
Kuunda na kujaa kwa matiti ni miongoni mwa dalili za ujauzito lakini pia ni dalili za kukaribia hedhi kwa baadhi ya wanawake. Posti hii itakwenda kufafanuabutofauti wa dalili hizi na kipi ni sahihibkatibya hedhi ama ujauzito. Soma Zaidi...

Namna ya kumtunza mtoto aliyezaliwa
Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa. Soma Zaidi...

Imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba
Posti hii inahusu zaidi imani potofu kwa mwanamke mwenye mimba, ni Imani ambazo zimekuwepo kwenye jamii kuhusu wanawake wenye mimba. Soma Zaidi...

Ongezeko la homoni ya estrogen
Posti hii inahusu zaidi ongezeko la homoni ya estrogen, kwa kawaida homoni hii ya estrogen inapaswa kulingana ikitokea ikaongezeka uleta madhara mbalimbali kwenye mwili na Kuna dalili ambazo zzz inaweza kujionesha wazi mpaka tukafahamu kuwa ni tatizo la o Soma Zaidi...

kunauwezekano wa darri ya kchefuchefu ictokee kabsa kwa mjauzito
Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu? Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia iwapo mimba imetoka.
Post hii inahusu zaidi mambo ya kuzingatia iwapo mimba imetoka mambo haya yanaweza yakawahusu akina Mama wenyewe, familia na jamii kwa ujumla. Soma Zaidi...

Hatari ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hatari za kutokwa na damu wakati wa ujauzito, hali hii utokea wakati wa ujauzito ambapo Kuna baadhi ya wajawazito utokwa na damu jambo ambalo hatupaswi kutarajia kwa sababu tunafahamu kabisa mama akishapata ujauzito na damu zinakom Soma Zaidi...